Pre GE2025 Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Pre GE2025 Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Watanzania tupo warahisi sana kuchezewa akili zenu. Lakini acha tu tuchezewe kwani huwa hatutaki kutafakari. Hivi jambo kama ni hili ni la utekelezaji au ni la kusemea kwenye majukwaa! Tuna idara za usalama, upelelezi na ulinzi. Kama wamegundua kuna watu wa aina hii kwa nini wasiondolewa kwanza? Rais kila siku ni lazima apewe briefing kuhusu masuala mbali mbali ya nchi, ina maana hawakumwambia huko kwenye vikao? Kwangu mimi hili ni suala la utekelezaji zaidi na siyo suala la kusemea jukwaani. Otherwise, kuna jambo fishy linataka kufanywa na huu ni mwanzo tu wa kulihalalisha.
Hapo kuna mtu anatafutwa

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mkimbizi alichukua uraia wa Tanzania au kateuliwa akiwa Mkimbizi bila kuchukua uraia?

Maana mtu anaweza kuwa mkimbizi, akachukua uraia wa Tanzania. Tanzania imetoa uraia kwa malaki ya wakimbizi.

Mwaka 2014 Tanzania ilitangazwa kuwapa uraia wakimbizi 162,000 wa Burundi kwa mkupuo.

Idadi ya watu waliopeea uraia ilifikia 200,000, rekodi ambayo haijawahi kutokea mpaka muda huo kwa mujibu wa shirika la wakimbizi wa Umoja wa Mataifa UNHCR.

Huo mkupuo mmoja tu wa mwaka 2014 tumetoa uraia kwa wakimbizi 200,000.

Sasa wote hao wanyimwe nafasi za kuongoza hata kama wananuwezo kwa sababu wakipata uraia wakiwa wakimbizi?

Pamoja na wao wenyewe kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi kwa idadi hiyo kubwa bado wananyanyasa wananchi wa mkoa wa Kigoma.
Baada ya kuwatumia kuongeza idadi ya kura na kukivusha chama kikongwe wanaleta wimbo mwingine kabisa....
Nchi hii imejaa unafiki wa kiwanga cha Guiness. 😳
 
Mimi ni mtanzania halisi, vizazi na vizazi. lakini wakati mwingine ninaamini hii dunia sio ya mtu mmoja, ni ya wote, hata Tanzania sio ya kwako peke yako ni ya wote, ni wakoloni tu walitutenganisha hasa sisi waafrika. sasa mtu kama mkimbizi aliyekimbia Rwanda au Burundi miaka ya 60, amekuja hapa akiwa mtu mzima, amezaa watoto, na watoto wamezaa watoto. wamesoma hapa, wamekulia kila kitu hapa, hawajui kwengine kwa kwenda ila hapa, mnataka waende wapi? warudi Rwanda, Burundi au Congo ambako hawajawahi hata kufika na hata wakienda wanafikia hotelini? wangekuwa wanawajua ndugu zao huko labda, au kama wanazipenda hizo nchi labda, ila huko kwenye asili yao hawakujui, hawajawahi kwenda, wengine hata baba zao hawajawahi kwenda, mnataka wafanye nini? wamekua wakijua hapa ndio kwao hawana kwao kwengine wanakokujua, na wamepapenda.

watusi kwa mfano, walianza kukimbilia Tanzania hata kabla ya uhuru kwenye first Hutu Revolution ya mwaka 1952 ambapo wahutu wali rise up against tutsi ambao ndio walikuwa kabila la kifalme Rwanda, kwasababu hiyo watusi wengi sana walikimbilia congo (ndio wale banyamulenge), na wengi walikimbilia Tanzania. ukienda mikoa kama ya kigoma, Tabora, Mwanza hadi Rukwa, kuna watu wenye sura za kitusi kabisa ila babu zao walikuja hapa kabla ya uhuru wa Tanzania, na wameishi wakibaguliwa tangu miaka hiyo hadi leo. mnataka waende wapi? nchi yenyewe hii ya Tanzania mnaishi mnakufa na kuiacha hapahapa, mtu kama haleti madhara, mwacheni. Kina Obama hao mbona baba zao ni wakenya ila wamekuwa marais wa Marekani? mnachotakiwa kufanya ni kuweka vizuri mifumo ya intelijensia ili mtu awe na asili ya moja kwa moja ya hapa Tanzania au la, asilete madhara, kwasababu hakuna guarantee kwamba hao mnaowaona kama ni asili ya wakimbizi ndio wataidhuru nchi, kuna uwezekano threat kubwa ikatoka miongoni mwetu sisi wenyewe tunaojiita wazalendo. dunia hii mmeikuta na mtaiacha, hamjaiumba kwanza ni mali ya Mungu hapa ametuweka kama mifugo tu tuishi, achaeni ubinafsi na ubaguzi.
🔨🔨🔨
 
Back
Top Bottom