Hawa watoto wameweza kuishi kwenye Msitu wa Amazon kwa siku 40 bila chakula wala malazi

Hawa watoto wameweza kuishi kwenye Msitu wa Amazon kwa siku 40 bila chakula wala malazi

Kila mtu ana matamanio.

Sitaki kwenda kwenye mbuga za kawaida. Mimi ni mfugaji, nimeishi katika mazingira ya porini sehemu kubwa sana ya utoto wangu.

Nataka kuishi kwenye msitu mnene, uliojazana na kutisha. Ambao bado binadamu hawajauingilia kwa kiwango kikubwa. Wenye maji tiririshi yasiyokatiza katika uchafu wa binadamu. Eneo tulivu lisilo na kelele za watu na magari.

Eneo lenye kivuli asilia, chakula kiwe cha asili pia. Maji yawe hayo yasiyochujwa na kemikali.

Mkuu, ni tamanio langu. Na nitalitimiza. Mungu aniweke hai.
Nenda kwenye misitu yacongo kuna eneo kubwa tu lamsitu huko congo nivirgin kabisa
 
Wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.

Hawa watoto wa wameweza kunusurika na mazingira hatarishi ya msitu mkubwa wa Amazon kwa siku 40 bila chakula wala malazi yoyote hadi walipopatikana leo kutoka kwenye kikosi cha waokoaji.

Watoto hao 4 walipotea mwanzoni mwa mwezi wa 5 baada ya ndege waliyokua wakisafiria kupata hitilafu ya injini na kuanguka kwenye msitu wa Amazon na kuua watu 3, rubani 2 na mama yao na hao watoto.

Baada ya jeshi la uokozi kufika eneo la tukio la ajali ya ndege wakakuta miili 3 lakini hakuna watoto, mtoto mkubwa ambae ni binti ana miaka 13 na mdogo kabisa ana mwaka 1.

Watoto hao ni jamii ya watu wa asili ya msitu wa Amazon. Hii ndio sababu inayosemekana kuchangia watoto hao kuweza kuishi siku 40 msituni kutokana na kujua mbinu za asili ya kuishi, survival skills toka wakiwa wadogo.

Watoto hao wamepatikana wakiwa wazima ila wenye afya iliyodhoofu hasa mkubwa wa miaka 13 ambae inadaiwa alikua akiwapa wadogo zake chakula chote wanachokipata wale kwanza kisha yeye anakula kitakachobaki.

Tukumbuke. Amazon imejaa nyoka wakubwa na wakali kama Anaconda, Chui wakali wanaoitwa Jaguar na mamba wakali pamoja na wale samaki wanaopiga shoti za umeme ukiingia kwenye himaya yao.

Je ikitokea ukajikuta kwenye mazingira magumu kama hayo can you survive?

Achana na ZE STOLI BUKU itakupoteza
 
Sema serikali iliwambia waseme walikuwa wanakula vyura kumbe ilikuwa mwenzao akikata kamba wanakata nyama yake wanakula kwahiyo ilikuwa mwenzao akifa wanamchomachoma wanaanza kumla.Dunia ina mengi sana.
😳😳Na hizi siri mkazijua na hamkutuambia wapenda simulizi. Nashukuru lakini nimejua leo, dunia hii dunia.
 
Naam.

Nataka niwe mpya..niondoe uchafu wote niliouvaa katika dunia hii. Kuna makabila mawili natamani sana kuyafikia. Kuna kabila la Sentinelese na Awa.

Hawataki watu wa nje. Wanaua. Ila hata nikifia huko nitakufa kwa amani.

Napatamani mno.
Bora uende Vanuatu kisiwani, kuhusu kujiondoa uchafu mtazamo wangu si kweli maana huko unaeenda kujichafua kwa mila zao unajiingizia spirits wageni.
 
Ni kweli tunaipenda Tanzania ila kusema Amazon iko overated nachekea kua na mashaka na uwezo wako wa akili.

Niambie msitu wowote Tanzania ambao unaweza kutembea zaidi ya kilomita 500 na bado hujafika sehemu ya makazi ya watu.
Tanzania hatuna misitu, mara milion Congo
 
Ni kweli tunaipenda Tanzania ila kusema Amazon iko overated nachekea kua na mashaka na uwezo wako wa akili.

Niambie msitu wowote Tanzania ambao unaweza kutembea zaidi ya kilomita 500 na bado hujafika sehemu ya makazi ya watu.
uwezo wa akili. Jiulize kupitia hapa nani hana uwezo wa akili kati ya mimi na wewe?. Kwa sababu
1. Hakuna mahala tumezungumzia au kutafuta ukubwa wa eneo la misitu.
2. Ninaeongea nae hajasema anahitaji ukubwa wa eneo la kilomita nyingi za msitu zaidi ya kutaka eneo la msitu mkubwa wa kutisha. Wenye nyoka n.k. sasa hilo eneo la ukubwa huo wapi tumelihitaji? Ndio ujione wewe una akili kujua ukubwa wa eneo!!!
3. Muda mwingine jiulize Kwanza unachotaka kumjibu mwingine ni sahihi. Sio ujanja kumtusi mwingine bila sababu yoyote,ndio ujione wewe una akili. Hata kama nilichokiongea hakiko sawa au ksbb zako hakijakupendeza
 
Ukidandia kitu kwa mbele utagongwa kwa nyuma, sitaki nikugonge nyuma.
 
Back
Top Bottom