Hi post yako haina ukweli wowote. Kwa kifupi ni upotoshaji.Hawa jamaa leo wanataka kufanya jambo la kihistoria yaani kumwingiza Ukraine kwenye umoja wa Ulaya kama V.I.P membership wiki hii, kumbuka kuwa membership huchukua had miaka 5, hivyo Ukraine anapita directly bila mlolongo.
Kwa nini wanafanya hivi? Nia kubwa ni kutaka kuingia kumchapa mrussi direct, hili liko wazi kabisa, Mrusi anatafutwa akae kwenye Target.
Tuombe sana Mungu moyo wa Putin ashushe ghadhab dhid ya Ukraine maana itakua vita ya kihistoria.
Kumbuka Mkuu wa Majeshi wa Uingereza alitangaza majuzi kuwa ni wakati wa Ulaya kujiandaa kwa vita.
Mungu atusaidie tu maana tunawategemea sana Urusi na Ukraine kwa chakula na nishati.
Kwanza EU haina jeshi hivyo kuingia kwa Ukraine EU hakuwezi kuleta tishio la kijeshi kwa Urusi. EU ni mambo ya kiuchumi na jamii.
Pili, wenye jeshi na ambao ukijiunga nao na ukawa na vita inakuwa vita ya wote ni NATO na sio EU.
Tatu, watakachopewa Ukraine sasa ni candidacy status, yaani haki ya kujiunga kuwa mwanachama. Tokea unapata hii status mpaka kupata uanachama huchukua zaidi ya miaka 10.
Ila tu EU ndio muhimu maana inaongozana na maisha bora, uchumi bora na uhuru mkubwa kwa watu wake. Hao wanaotaka kujitenga na Ukraine leo, miaka 10 ijayo Ukraine ikiingia EU, wao wenyewe watataka kurudi Ukraine. Kwani nani anapenda njaa? Kule Russia umaskini wa watu utaendelea kwa muda mrefu sana. Udikteta ni majanga.