Haya Mambo ya Viongozi wa Kisiasa Kwenda na Viti Vyao Kwenye Nyumba za Ibada Yasitishwe

na hili ni la kujadiliwa? tunakoelekea tutaomba kujua Rais ananunua nguo viwanda vya ndani au uturuki
 

Inaonekana hujaelewa hoja ya mleta mada. Suala siyo kwa sababu kiongozi wa Marekani kafanya. Hoja ni kuwa kwenye nyumva za ibada, kwa msingi wa imani zote, uislam na ukristo, uingiapo ibadani hustahili kufanya kito chochote cha kujitofautisha na watu wengine kwa kuonesha kuwa wewe ni bora zaidi. Ni mahali pa kujishusha na kuonesha kuwa kwenye utukufu na ufalme wa Mungu, huna tofauti na mtu mwingine yeyote.

Mifano ya marais wengine ameitoa kuonesha tu jinsi hata marais wa nchi nyingine wanavyotii misingi hii ya kiimani. Ukiona wewe ni tofauti na wanadamu wengine, usiende. Fanya ibada yako kama yule mfarisayo aliyenena kuwa yeye siyo sawa na mtoza ushuru, lakini Mungu anasema unakuwa hujasali.
 
Hayo mabenchi ya mbao yanaumiza jaman..so wanaweka kiti chenye sponji ili awe comfortable

Kama ana tatizo la kiafya asiloweza kulivumilia, ni sahihi, anaweza kuwekewa kiti kinachoendana na afya yake, lakini si vema kuwa kiti cha ikulu. Kiti cha ikulu kina nembo. Ile nembo ni alama ya ufalme na mamlaka. Ndani ya nyumba ya ibada, ufalme ni wa Mungu pekee, hatustahili kupeleka ufalme mwingine ndani ya nyumba yake.
 

Umekosea sana kusema eti kila mmoja kwenye nyumba ya ibada anasema anachokitaka. Kuna miongozo ya wazi kabisa, na imesisitizwa. Kunaweza kukawa na tofauti ya namna ya kunena na lugha inayotumika, lakini mantiki lazima iwe moja. Na hayo yamesemwa wazi kabisa kwenye vitabu vya neno la Mungu.

Kama ana tatizo la kiafya, anaweza kuwekewa kiti tofauti, lakini hakitakiwi kuwa na nembo yoyote inayoashiria mamlaka, maana kanisani mamlaka ni ya Mungu pekee yake.
 
Mbona viongozi wa kanisa wanakaa mbele na Wana viti vyao?
 
Sasa unatoa mfano wa marais wa marekani, kwanini hukutoa mfano wa marais wetu? JPM, Nyerere, Kikwete, Mkapa, Mwinyi walivyokuwa wanaenda makanisani walienda na viti vyao?
Tuige hata Kenya ambapo Rais hatembei na kiti maalum kila mahali.
 
Kwenye Urais wa kifalme hiyo ni muhimu.
 
Africa kuna mambo mengi ya ajabu, Museveni yeye hutembea na choo chake maalumu cha kutumia.
 
Mtu kukalia kiti Chake inaruhusiwa katika ibada hata msikitini. Wapo tele wanakalia viti vyao, tembelea tu misikitini utaona.
Msikitini waumini hawatumii viti
 
Isitoshe hata kwenye Biblia sidhani kama Wafalme waliingia mahekaluni na kwenye masinagogi na kukaa pamoja na commoners. Eti Mfalme Sulemani au babake Daudi wakalie mabenchi ya hekaluni. Aaaa wapi!
Usifananishe mambo ya Ufalme na Jamuhuri. Kwenye ufalme ndio kuna tofauti kati Royal blood na commoners.
 
Huwa inaanza viti inakuja misafara mirefu inayosimamisha shughuli za watu kwa masaa.
 
Ibada yako wewe Bw. Joseph inaathirika vipi na uendaji wa raisi na kiti chake mwenyewe???
 
Kama kanisa liko kwenye ujenzi bado, au halijajitosheleza kwa viti ni sawa waende na viti vyao. Lakini kama kuna viti vya kutosha, halafu wewe uende na kiti chako kwa kuona vile vya pale kanisani havina hadhi inayolingama na wewe, unamkufuru Mungu.
Kwa hiyo Bora usiende kabisa !??
 
Mbona viongozi wa kanisa wanakaa mbele na Wana viti vyao?

Kiongozi wa Kanisa awapo ibadani anakuwa kuhani, mchungaji na mwalimu. hufanya kazi ya ukuhani, kazi ya kufundisha na kazi ta kuwachunga kondoo wa Bwana. Yeye, tuwapo ibadani ndiye kiongozi mkuu, wengine wote ni kondoo aliopewa kuwaongoza. Huwezi kuwachunga kondoo, na wewe ukiwa umekaa katikati ya kondoo. Vile vilivyopo ndani ya hekalu, kanisa au pale madhabahuni, havipo kwaajili ya utukufu wa kiongozi wa ibada bali kwaajili ya utukufu wa kile anachokifanya. Na huwezi kusikia padre au mchungaji, baada ya ibada anachukua kiti au meza ya altareni kwenda kuitumia nyumbani kwake. Na pale atoleapo sadaka au amwombapo Mungu, hawezi kukaa kwenye kiti, husimama au kupiga magoti, kuonesha kuwa naye si chochote mbele ya ukuu wa Mungu. Wala hakuna kiongozi wa dini anayeingia kanisani na kiti au meza yake. Atatumia kile alichokikuta.
 
Kwaiyo Rais akiwa kanisani anakuwa sio Rais Tena na je huyo kuhani wako akitoka nje ya kanisa anakuwa sio kuhani Tena?
 
Kwahiyo kiroho unatakiwa kukalia benchi? Hebu acheni hekaya za kijima hizi.

Kiti cha rais au benchi la kanisani haviingiliani kwa vyovyote vile na mchakato wa maombi. Mtu anaweza hata akaja na godoro lake kanisani na wala hakuna shida. Msikariri.
Godoro labda msikitini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…