Haya matukio yamenifanya nijitafakari upya tabia zangu

Mke wa tatu wa babu mkubwa hakubahatikaga kupata uzao. So babu alivyofariki, wajomba wakawa wanapeleka chakula tu lakin hakuna alietakaga kumchukua kuishi nae. All this kwa sabbu ya migogoro ya kifamilia.

Siku katika kukutana kimisiba, mtu akamuuliza hivi bibi unaishi mwenyewe kweli? Bibi akajibu " ndio naishi mwenyewe hata siku nikifa nitakutwa mdomo wazi haujajifunga maana hakutakuwa na wa kuufumba." Ikaishia hapo. Mwaka mmoja baada ya bibi kutamka hayo maneno kweli ikatokea kama alivyosema. Mwili wake ulikutwa ndani baada ya majirani kutomuona kwa siku tatu. Mlango kuvunjwa, akakutwa alishafariki kitambo mwili unatoa harufu.

Kuna mjomba wangu mmoja nae anapiga mishe za machimbo ya madini. Aliwahi pata shangazi lakin akaachana nae maana alimzingua. So mpaka sasa na miaka yake 65 hanaga mke. Anaishigi mwenyewe tu. Sasa kuna siku katoka mihangaikoni, akawa kanunua nyama. Akaingia ndani akaibandika kwenye jiko la gesi. Akakaa kitandani akapitiwa na usingizi.

Anaishi chumba kimoja. Ile nyama ikachemka mpaka ikaungua. Mara watu wanaona moshi. Gonga hodi sana no reponse. Wakaona hapa tutaungua wote. Ndo mlango kuvunjwa, moto ulikua ushashika kwenye vikaratasi vya kwenye chumba. Ndo watu kumuamsha, kuzima jiko, kulitoa nje. Almanusura nyumba ingewaka na yeye angefia ndani. Mpaka leo maisha yake its still a puzzle.

Yes kuwa introvert ni vizuri lakini atleast uwe na mmoja wa kukufahamu kiundani. Kila kitu ni risky. Choose your danger wisely...
 
Oshey Mrs 💰
 
Mwaka 2021 nlipoteza rafikiangu mkubwa sana wa utotoni adi ujanani wetu.
Nakumbuka alifia geton kwake kajilaza kwenye sofa lake, niliumia sana
Miezi sita mbele mama yake akamlazimisha kaka wa marehemu kuoa kwa lazma ili yasmkute ya kufia geto huku unajiona
 
Atakayeweza kufanya hivi ni mpenzi wako
 
Aiseee msitutishe basi daah kwaiyo sisi tunaojifungia wiki hatutoki itakuwaje sasa daaah 😔😑
 
Ukweli ni kwamba uwe introvert au xtrovert utakufa tu!!!!

Uwe unaishi pekeako au uishi na mke/mume still ukifa utaoza tu

nothing exceptional,,, yaan uishi na mtu eti kisa atoe taarifa siku ukifa,, vp yeye ndo akatangulia kufa??? Vp ukifa yy akiwa kasafiri??????
 
Ni kweli kilamtu ataonja umauti, ila upweke sio kitu kizur katika maisha haya tunayoishi
 
Mie sioni cha ajabu hapo maana either utambulie mapema na watu kuwa umefariji au ichukue muda vyote sawa tu maana at the end history yako inakoma na unafukiwa shimoni.

Unaigopa hicho.kidogo vipi wanaoliwa na samaki ziwani na baharini au wanaoliwa na wanyama
 
Kingine hupendi kuoga ndio maana ukajiita SipeNDI kuoGA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…