Hili ndilo soko kuu la samaki Moshi Kwa sasa lililopo eneo la Mailisita katika wilaya ya Hai
Wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa samaki waliohamishiwa eneo hilo walikabidhiwa eneo hilo lisilokuwa na miundombinu yoyote inayoendana na aina hiyo ya biashara.
Hakuna miundombinu ya vyoo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara hao, bali hutumia vyoo vilivyopo jirani na eneo hilo.
Mfumo wa maji safi na taka hakuna kutokana na. Kuwa magari huleta samaki wabichi na wengine huoshea eneo hilo hilo kabla ya kukaanga hapo na Kusafirisha.
Miundombinu ya jiko hakuna bali kila mtu hukaanga samaki hapo hapo anapoona Panafa.
Mvua na jua vinawaathiri kutokana na kuwa ni eneo la wazi na halijajengwa kwa namna yoyote ile ili liweze kuwangika na mvua wafanyabiashara hao.
Wakati huo huo hutozwa ushuru kila siku wa soko.
View attachment 2554409View attachment 2554410View attachment 2554411