Hayati Magufuli alifanikiwa kutengeneza kundi lililomuamini na kumtii mithili ya wafia Dini

Hayati Magufuli alifanikiwa kutengeneza kundi lililomuamini na kumtii mithili ya wafia Dini

Haya alishakufa miaka 2 sasa ilitosha kusifiwa akiwa hai. Mtu akifa na bado akaishi mioyoni mwetu hakika hakulazimisha kupendwa ila alipendwa kwelikweli. Tanzania watu waliowahi kupendwa wa kwanza ni magufuli akifuatiwa na nyerere
Well mkuu
 
Kuna mambo yanafurahisha sana kwenye siasa!!

Hivi unaanzaje kumsema Mwamba yule kuwa hakuwa na ushawishi wowote majukwaani!?

Labda nikusaidie tu. Kuelekea uchaguzi wa 2025 tutajua kama Magufuli hakuwa na ushawishi wowote kwa Watanzania kama unavyotaka kutuaminisha hapa. labda ungesema Magufuli hakuwa mwanasiasa mzuri bali alikuwa Rais anayejituma, kufanya kazi kwa bidii na aliipenda nchi yake. Huenda alikuwa na madhaifu yake lakini yule mzee tuacheni unafiki alikuwa anapiga kazi. Na hadi vizazi na vizazi atabaki kwenye historia.

Sasa nyie mnaojiita wana demokrasia shangilieni sasa kwani sasahv hakuna rushwa, maisha ya wananchi yamekuwa mazuri, demokrasia imeleta watalii nchini, kodi na tozo hakuna tena, umeme na maji vinapatikana kwa wingi, deni la taifa limepungua na pia demokrasia imeimarisha uwajibikaji kwa mawaziri na watumishi wa serikali. Sasa hivi ukienda maofisini watu wanachapa kazi.

Ama kweli demokrasia imefungua nchi. Ripoti ya CAG inafanyiwa kazi kwani demokrasia imesababisha wala Rushwa wachukuliwe hatua za haraka. Machinga wanafanya biashara kwa uhuru. Nani kama Wapinzani walioleta maridhiano????

Magufuli kwakweli aende zake in Peace!
Umepiga panapouma aisee
 
Hakuna utawala ambao haujawahi kuua, kuteka wala kupoteza watu kwa africa

Katiba zetu mbovu ndiyo zinawafanya watawala wafanye wanavyotaka

Kwani Dr mwamboka alitekwa kwenye utawala wa Magufuli? Na Mawazo aliuwawa kwenye utawala wa Magufuli?!
Alikutwa baharini kwenye kiroba ?
 
Mimi siyo mwanasiasa,Ila ukweli Ni kwamba hata mbowe ni mungu wenu pale chadema.

Na ameisimika vema ideology yake maarufu ya "Mimi ndiye chadema na chadema ndiyo mimi. Nitakufa nikiwa mwenyekiti,Mimi ndiyo mbowe".

Hiyo ni ibada kamili, vinginevyo neno ibada umelipa maana yako ya kujitungia,tofauti na uhalisia wake.

Toeni kwanza hilo boriti kabla hamjamtaja Magufuli kila saa.

Siasa zenu bongo mmeweka unafiki mbele.
Dah! Umepiga panapouma akikujibu nitag
 
Kuna mambo yanafurahisha sana kwenye siasa!!

Hivi unaanzaje kumsema Mwamba yule kuwa hakuwa na ushawishi wowote majukwaani!?

Labda nikusaidie tu. Kuelekea uchaguzi wa 2025 tutajua kama Magufuli hakuwa na ushawishi wowote kwa Watanzania kama unavyotaka kutuaminisha hapa. labda ungesema Magufuli hakuwa mwanasiasa mzuri bali alikuwa Rais anayejituma, kufanya kazi kwa bidii na aliipenda nchi yake. Huenda alikuwa na madhaifu yake lakini yule mzee tuacheni unafiki alikuwa anapiga kazi. Na hadi vizazi na vizazi atabaki kwenye historia.

Sasa nyie mnaojiita wana demokrasia shangilieni sasa kwani sasahv hakuna rushwa, maisha ya wananchi yamekuwa mazuri, demokrasia imeleta watalii nchini, kodi na tozo hakuna tena, umeme na maji vinapatikana kwa wingi, deni la taifa limepungua na pia demokrasia imeimarisha uwajibikaji kwa mawaziri na watumishi wa serikali. Sasa hivi ukienda maofisini watu wanachapa kazi.

Ama kweli demokrasia imefungua nchi. Ripoti ya CAG inafanyiwa kazi kwani demokrasia imesababisha wala Rushwa wachukuliwe hatua za haraka. Machinga wanafanya biashara kwa uhuru. Nani kama Wapinzani walioleta maridhiano????

Magufuli kwakweli aende zake in Peace!
Nimependa ulivyoiweka. Waulize kwamba ni kwa nini wanataka kuua legacy ya Magufuli? Sababu iko wazi, wanataka ikifika 2025 asiwe anatajwa tena mana itawapa tabu dhidi ya wananchi ambao wameshatambua kila kinachoendelea na watalinganisha. CCM inakosea sana kuacha JPM abomolewe hivi, watataka kumtaja vizuri wakati wa uchaguzi lkn itakuwa too late!
 
Nchi ilizizima Kwa furaha alipokufa watu mabaa yalifunguliwa upyaaaaa na yaliyobakiza wanywaji wawili kufumba na kufumbua kukawa na wateja kama wote Arusha mbeya dar acha kabisa Arusha ngombe na mbuzi walichakaa!
Mlevi mbwa! unashabikia ulevi kwenye kifo cha mtu. Ndiyo tabia kama zako za uvivu na unywaji pombe kumkomoa mtu zinazoturudisha nyuma kama taifa
 
Magufuli alikuwa dikteta. Madikteta wote duniani sifa yao ni kuwa na watu wa kuwatukuza na kuwasifu. Ndiyo maana alifanikiwa. Namfananisha Magufuli na Chavez. Wote walikuwa populist waliodhani wanasaidia nchi zao kumbe wanaziletea majanga makubwa.

Kama Chavez alivyofia madarakani Magufuli naye alifia madarakani. Tofauti ndogo kati ya hawa wawili ni kuwa Chavez alikuwa na mrithi anaeendeleza ujinga wake. Magufuli alikuwa bado hajaanda mrithi wa kueendeleza udikteta wake
Madikteta wote huitwa kwa sababu tu ya propaganda ya vyombo vya Magharibi. Huyu JPM ni nyumbu tu ndo walimwita hivyo kutokana kasi yake ya kuleta vitu vya maendeleo binavyoonekana. Wao waliamua tu wamchafue kwani aliwafunika hawana la kusema, yale yote waliyowish yafanyike magu aliyafanya so mwishowe walikosa hoja. Huyo ndo JPM
 
Erythrocyte sijui ulishindaje tuzo ya JF mpaka ilibidi niulize, kumbe kusifia chadema tuu ht kama wanafanya upumbavu kunaweza kukupa tuzo.
Usishindane na aliyejaaliwa , halafu wala hata sikumbuki kama nilishinda chochote JF , lengo la mimi kuandika jf ni kuelimisha tu , sikulenga kushinda chochote
 
Usishindane na aliyejaaliwa , halafu wala hata sikumbuki kama nilishinda chochote JF , lengo la mimi kuandika jf ni kuelimisha tu , sikulenga kushinda chochote
Kuelimisha ni kwenye jambo la upande mmoja tuu ht kama upande mwingine ukifanya mazuri.?
 
Usishindane na aliyejaaliwa , halafu wala hata sikumbuki kama nilishinda chochote JF , lengo la mimi kuandika jf ni kuelimisha tu , sikulenga kushinda chochote
Na siwezi kushindana na aliyejaliwa
 
Kwa mfano uzi huu si ni wa ccm na Magufuli , au umeona Chadema hapa ?
Ww jamaa bhana dah, sasa hy ccm na huyo Magufuli umezungumziaje.? Ww huon kuwa umeweka chuki.? Kwan hakuna mazuri yao.?
 
Huu ulikuwa uwezo wa kipekee sana Sijapata kuona ! Inafahamika kwamba Viongozi karibu wote wa ccm wanatengeneza Makundi , lakini Mara zote viongozi hao hutengeneza makundi ya kampeni , yaani wanatengeneza wapambe wa kufanya kampeni , kwamba angalau pamoja na kuiba kura , angalau viongozi wa ccm waliopita waliunda hata timu ya kushawishi wananchi ili wawachague .

Dr Magufuli aliunda kikundi cha hiyari cha "kumuabudu" nasema cha hiyari maana sikuwahi kuona watu wakilazimishwa kujiunga nacho , hiki kikundi hakikuwa cha Kampeni , maana Magufuli hakuwahi kuamini katika demokrasia , hili kundi lilikuwa kama zile Praise team za makanisa , ni kulinda imani kufa na kupona , kwamba chochote atakachokifanya hata kama kilikuwa hatari kwa nchi , kama kuvunja kienyeji mikataba na wawekezaji wa kimataifa , jambo ambalo ni hatari lakini kikundi hiki kilishangilia kufa na kupona .

Kilikuwepo hata kikundi cha kutukana Wazee , wastaafu na Wanasiasa wa vyama vyote ikiwemo ccm , hakuna yoyote aliyepingana na Magufuli hata kwenye mambo ya msingi ambaye hakushambuliwa na kikundi hiki , mmemsahau Musiba na yale Magazeti yake yaliyodaiwa kuchapishwa na Usalama wa Taifa ?

Inasemekana Magufuli alipenda sana kusifiwa , kwahiyo jamii inatambua wako waliokuwa wanamsifia na kujikuta wakiingizwa kwenye praise team na kuteuliwa .

Sasa mshangao wangu ni huu , Mtu huyu ambaye hakuwa na ushawishi wowote Majukwaani aliwezaje kutengeneza kikundi cha kumuabudu na kumtii mithili ya Machifu wa enzi za Ujima ?
Mkuu 'Erythro'; nimekuja kutambua uwezo wako mkubwa wa kuibua mada zenye uzito mkubwa sana, hata pale inapokuwa wewe umelalia upande wa pili, tofauti kabisa na mada unayoianzisha.

Hii ni mada yako ya pili, nzito sana katika muda mfupi tu, baada ya ile nyingine iliyojadiliwa sana hapa JF.

Sijasoma kikamilifu hadi mwisho kuhusu uliyoandika humo ndani ya mada, lakini kutokana na niliyosoma mwanzo wa mada yenyewe, nimepata msukumo niweke machache tu kuhusu mada yako hii hapa kama ifuatavyo.

Magufuli alikuwa na ukichaa wake wa ajabu sana, ambao baadhi yetu ulitutisha sana juu yake na kuamua kumkataa moja kwa moja mapema kabisa.

Hilo nililolisema hapo juu, halina maana kwamba hapakuwa na mambo yaliyoeleweka na wananchi vizuri sana katikati ya ukichaa huo.

Tahadhari ninayowapa watu kama wewe, mkuu 'Erythro' na baadhi ninaowaheshimu sana katika misimamo yenu kuhusu hatmna ya nchi yetu, ni katika kushindwa kwenu katika kuwaelewa waTanzania.

Hapa kuna funzo muhimu sana mnalotakiwa kujifunza namna waTanzania walivyo (baadhi, wengine watasema wengi wao).
Kundi hili unaloliona wewe sasa hivi na kudhani walikuwa ni wafuasi wa Magufuli, pamoja na ukichaa wake wote ule, inalazimu ukae chini na kuelewa maana ya kundi hili ni nini. Usilibeze. Lisome kwa makini kabisa, na kwa sehemu kubwa utaanza kuelewa hawa waTanzania wanaopewa kila aina ya majina ya kudhalilisha ni watu wa aina gani.

Nilisema nitasema machache. Nimalizie kwa kukuomba uweke mlinganisho wa hali za uongozi, uliopo sasa na huo wa Magufuli. Utaona kwamba kuna uhusiano mkubwa sana katika hayo unayoyaona toka kwa hilo kundi unaloliita "wafuasi wa Magufuli." Siyo lazima wote wanaokataa haya yaliyopo sasa wawe ni wafuasi wa Magufuli, kama unavyohitimisha/rahisisha wewe.

Ninakuomba unisome vizzuri, pengine sitaeleweka kirahisi kuhusu jambo hili.

Pongezi kwa mada fikirishi sana siku hizi chache zilizopita.
 
Back
Top Bottom