Hayati Magufuli alijenga vituo vya afya 44 kwa miaka mitatu, Rais Samia anajenga 220 kwa miezi mitatu

Hayati Magufuli alijenga vituo vya afya 44 kwa miaka mitatu, Rais Samia anajenga 220 kwa miezi mitatu

What goes around comes around!!
Ndicho mlichokuwa mnakifanya Team Chattle enzi za Mwendazake, tulieni hivyohivyo na "Atake Asitake" wenu!!!
Records ziko wazi Jpm hamna wa kumfananisha nae kwenye utekelezaji miradi
 
RAIS MAGUFULI VITUO VYA AFYA 44 MIAKA 3 | RAIS SAMIA VITUO VYA AFYA 220 MIEZI 3

Ukisoma "Kitabu Cha Hali ya Uchumi Tanzania " cha mwaka 2018 ukurasa wa 60,utaona wakati Rais Kikwete anaondoka madarakani mwaka 2015 vituo vya afya vya serikali vilikuwa 507,Mpaka 2018|19 jumla ya Vituo vya afya vya serikali ilifikia 551 sawa na Ongezeko la Vituo vipya 44 ambazo ni 9% chini ya Hayati Rais Magufuli,

Kwakutumia tozo hizi za Kizalendo Rais Samia anajenga vituo vya afya vipya 220 kwa miezi mitatu ( 3 ) tu sawa na ongezeko la 43.4%,Nakwa lugha rahisi kabisa,Tunasema kasi ya Ujenzi wa vituo vya afya ya Rais Samia kwa miezi mitatu ni X5 zaidi ya kasi ya Ujenzi wa vituo vya afya ya Rais Magufuli kwa miaka mitatu mfululizo,

Jumla ya vituo vyote vya Serikali vipya na alivyokarabati Hayati Rais Magufuli kwa miaka mitano vilifikia 487 ( soma Hotuba yake ya mwisho bungeni ukurasa wa 24 ),Hii inamaana gani, Rais Samia kwa muda wa miezi hii michache atajenga karibu nusu ya vituo vyote vilivyojengwa|kukarabatiwa na Hyt Rais Magufuli kwa miaka mitano aliyokaa madarakani,Mama anastahili pongezi kama kweli tunamwogopa Mungu,

Na kwa andiko hili,Itusaidie kutambua faida ya tozo kwenye kuwahudumia na kuwafikia kwa haraka watoto wa masikini wa nchi hii wanaokufa kila dakika kwa kukosa huduma za afya hasa hasa akina Mama na Watoto huko vijijini,

Att |Isionekane napinga kazi nzuri ya Hyt Rais Magufuli hapana, ni katika kuangazia Mwanzo wao wote kwenye hili la vituo vya afya na Samia hakamatiki kwani namba hazidanganyi,

|[ Hili ndio Jibu la kwanini leo tozo na Sio zamani ]|

|WANAOULIZA RAIS SAMIA SULUHU ANATUPELEKA WAPI | HERE IS WHERE WE GO BRO'S & SISTERS KUWENI NA AMANI NCHI YENU IKO MIKONO SALAMA & SHUPAVU YA MAMA|



...Kazi iendelee...

Screenshot_20210903-084345.png


Screenshot_20210903-144451.png
 
Takwimu na hoja zako ni chanya na za kujenga nyumba moja bila kunyang'anyana fito. Timu nzuri ya mchezo wa kupokezana kijiti (relay) , kila apokeaye kijiti, kasi yake inataikiwa kuwa zaidi ya aliyemkabidhi kijiti. Ikiwezekana ongeza wigo wa takwimu zako kuanzia awamu ya pili. Je kila rais wa awamu husika aliridhi vituo vingapi na aliridhisha vingapi?

Mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan ni nyota ya alfajiri na mawio yenye nuru njema. Atawapiku waliomtangulia kwa ubunifu wa vyanzo vya mapato ndiyo maana atafunga awamu yake na vielelezo vingi. Lakini ni vyema kuwe na uhusiano chanya na vyanzo vya mapato. Mei 2021 mfumuko wa bei ulikuwa 3.3%, Juni 2021 ulikuwa 3.6% kutoka 3.3% Mei 2021 na Julai ulikuwa 3.8%.

Tafisiri yake maisha yameanza kuwa magumu. Mamlaka ya Hali ya Hewa imetabili kuwa mvua za vuli zitatkuwa chini ya wastani na wastani. Maana yake uzalishali wa chakula na mazao ya biashara vitashuka na kuzidi kuongezeka mfumuko wa bei. Tutajenga vituo vya afya vingi katika jamii ambayo ni masikini zaidi ya Mei 2021 na gharama ya huduma za afya kupanda.

Itakuwa vizuri kupitia bajeti ya 2021/2022 baada ya miezi sit na kuona kama kutakuwa na nguzu za kiuchumi kuierekebisha bajeti husika.
 
anajitahidi kiasi chake, ila kwa kuwa wanajenga nyumba moja sioni sababu ya kushindanisha shindanisha kwani kufanya hivyo tutakuwa tunarudi kulekule kwenye majisifu na majigambo.
 
Mmeanza ujinga kama wa mataga, una uhakika gani kama atafanikiwa? Mnaabudu watu kuliko uhalisia
 
anajitahidi kiasi chake, ila kwa kuwa wanajenga nyumba moja sioni sababu ya kushindanisha shindanisha kwani kufanya hivyo tutakuwa tunarudi kulekule kwenye majisifu na majigambo.



Bila kulinganisha tunajuaje nani zaidi?
Wananchi lazima waelewe nani ni nani?
Tulidhani kifo cha MAGUFULI tungerudi nyuma ila Mama ndio kaja juu zaidi,
 
Gwaji Boy oyeeee. Wabunge wameachiwa bonge la msala walijikomba mishipa ya shingo ikawatoka wakitegemea wanamfurahisha Mama kumbe Mama ana roho ya msamaha hana kabisa kinyongo. Siasa ugumu wake ndio mazingira kama haya.
 
Gwaji Boy oyeeee. Wabunge wameachiwa bonge la msala walijikomba mishipa ya shingo ikawatoka wakitegemea wanamfurahisha Mama kumbe Mama ana roho ya msamaha hana kabisa kinyongo. Siasa ugumu wake ndio mazingira kama haya.
kubishana kuhusu chanjo si muhimu kuliko uhitaji wa tozo. mama amemtumia huyo huyo gwajima wenu (kiujanja kabisa) kujitangazia msimamo wake wa tozo kiulaiiiini kabisa kwa taifa lote na ameeleweka hivyo kelele za tozo zimeshajifia. nimependa sana hii, wengi hawajaelewa kuwa jana kaupiga mwingi hatari.
 
Hebu tuoneshe picha japo ya misingi ya hivyo vituo vya afya?
Pesa zimeenda hata wiki 3 bado afu unataka msingi? Unadhani Kazi za serikali ni kama kujenga vibanda vyako?

Waziri alishasema ndani ya mwezi michakato iwe imeisha na ujenzi umeanza kwa hiyo be patient by the end of this month utaona misingi hadi utashindwa kuhesabu.
 
Analysis yako ni shallow sana.

Magufuli alisema vituo ambavyo walikuwa wamekamilisha, hakusema kuwa kuwa hapo ndipo walikuwa wameishia bali kuna ambavyo vilikuwa vinaendelea kujengwa vvikiwa hatua mbalimbali. Huyu mama anaendeleza vitup ambavyo alivikuta vikiwa katika hatua mbalimbali kabla havikamilika.

Sasa wewe unakuja analysis iliyokuwa skewed kama kuwa vituo wanavyosema vyote vilifanyiwa upembuzi yanikifu na kuanza kujengwa miezi hii mitano tu kabla hata bajeti yake haijapitishwa. Mama alikuta bajeti iliyoachwa na Magufuli ndiyo aliyendelea nayo kwa miezi minne, hivyo miradi yote aliykuwa anasimamia katika kipindi hicho ni ile aliyokuta kwenye bajeti hiyo; sasa hivi ndiyo ameanza na bajeti yake mwenyewe na miradi yake.
 
kubishana kuhusu chanjo si muhimu kuliko uhitaji wa tozo. mama amemtumia huyo huyo gwajima wenu (kiujanja kabisa) kujitangazia msimamo wake wa tozo kiulaiiiini kabisa kwa taifa lote na ameeleweka hivyo kelele za tozo zimeshajifia. nimependa sana hii, wengi hawajaelewa kuwa jana kaupiga mwingi hatari.
Mama yupo very strategic kuliko anavyoonekana. Anawajua wabongo wengi wanaangalia kurasa ya juu kabisa sio wazuri kusoma kilichoandikwa kurasa za ndani.

Gwaji Boy oyeeeee
 
Mama alikuta bajeti iliyoachwa na Magufuli ndiyo aliyendelea nayo kwa miezi minne, hivyo miradi yote aliyokuwa anasimamia katika kipindi hicho ni ile aliyokuta kwenye bajeti hiyo; sasa hivi ndiyo ameanza na bajeti yake mwenyewe na miradi yake.
Sio kuishia swala ni miaka aliyotumia na idadi ya alivyojenga
 
mama akitulia vzur katika matumizi ya hzo pesa kwakua mkali katika kila shilingi na ufutiliaji makini na kuwajibisha watakao chezea hd 2025 atakua amefanya makubwa sn
tatz wapigaji watakua wengi alafu miradi mingi itadoda haijaisha hela hazieleweki ziko wapi

watanzania kwa ss tunaamini kwakuona hadith tumezichoka
 
Sio kuishia swala ni miaka aliyotumia na idadi ya alivyojenga
Inagemea alianzia wapi; ukianza kuchimba msingi ndipo ujenge, na mwenzio akakuta msingi uko tayari na nusu ukuta, spidi ya kumaliza haitalingana. Halafu ujenzi siyo miradi ya vituo vya afya tu; kuna miradi mingine pia.
 
uzi mmoja una urudia rudia mara3 mpaka 4 kweny comment
vipi mbona hamjiamini
 
Back
Top Bottom