Hayati Magufuli alikosea kwenye mambo mengi mno. Kubwa mojawapo ni kumchagua huyu mtu

Alilazimishwa na nani? Kikwete?

Ndio na Kikwete mwenyewe juzi kati akiwa Arusha kwenye mkutano na vijana alikili wazi kuwa ndie aliempendekezea Magu juu ya Makamu wa Rais kuwa Mwanamke na akampendekeza Samia
 
Hakuna statement inaniudhi kama hiyo eti anapotoshwa na walio mzunguka, ila kadiri wanavyozidi kuihubiri ndo wana admit alichokisema mtoa mada kwamba ndugu yetu ni empty set maana anapelekeshwa tu yeye hana anachokijua
Chuki zenu za yeye kuwa mwanamke zitawatesa mpaka uzeeni.
 
Chuki zenu za yeye kuwa mwanamke zitawatesa mpaka uzeeni.
Kuna muda ni vizuri ukajitahidi sana hata kama unasikia unawashwa sana basi funga na kumuomba Mungu wako akusaidie usionyeshe ujinga wako kwa watu. Tunajadili kiongozi wala sio jinsia yake ila kwa sababu wapambe na walamba nyayo wake mmekosa hoja za kujibu mnaibukia kwenye jinsia mara dini n.k. Waambieni waliowatuma kwamba kazi ya kumtetea ni ngumu kama kuuza nguo za jeshi sokoni maana haziuziki.
 
Kwanini amchague mtu anayemtaka yeye?. Hakuna rais aliyeweza kuweka mrithi wake anayemtaka mwenyewe.

Alishindwa Mwalimu Nyerere kumuweka Salim Ahmed Salim angeweza JPM ambaye hakuwa na misingi ndani ya CCM?.
Ni misingi ipi hiyo ndani ya CCM?

Mtu amekaa CCM na serikalini miaka zaidi ya 20 wasema hakuwa na misingi?

Na pili, mgombea wa uraisi huchagua mwenyewe makamu wake au huchaguliwa na watu maalum au hupewa mapendekezo ya orodha ya majina?

Tufafanulie uzuri mkuu.
 
Kazi ya kumtetea haina ugumu wowote. Yupo tofauti sana na mtangulizi wake.

Anasikiliza matatizo ya watu kwa ukaribu, mtangulizi hakutaka kupingwa alijiona yupo sawa muda wote.

Anaruhusu ubunifu wa wasaidizi wake ufanye kazi kwa faida ya nchi na matunda yanaonekana. Hataki kila kitu kukifanya yeye tu akidhani anajua kila kitu.

Biashara zinastawi sana awamu hii kwani hakuna unyanyasaji wala uporaji wa mali za watu.

Awamu iliyopita ilisababisha vifo vya baadhi ya wafanyabiashara kwa kuendekeza upuuzi wa kunyanyasa na kupora mali za watu kwa kutumia TASK FORCE.

Huo ujinga ulimnyang'anya mali hayati Mbughuni mjasiriamali mzalendo alizochuma kwa jasho kwa miaka mingi na akapewa Musiba na kwa mbwembwe akawa anawatukania wazee wa CCM!.

Mbughuni mpaka anaaga dunia alikuwa kwenye michakato ya kurudisha mali zake kutoka mikononi mwa chama.

Samia anaweza kuwa na udhaifu lakini hana unyama kama huo nilioutaja hapo juu, hivyo awamu yake ni nyepesi kulinganisha na hizo za wajuaji.
 
Uliona wapi mtu anachagua msaidizi smart kuzidi yeye
Uko sahihi Kabisa mkuu...

Siku zote lazima uchague mtu ambae mnaendana kimtazamo lakini unae mmudu kwa mambo mengi mkuu,

Ni ngumu na hatari kuchagua mtu anaekuzidi uwezo kwa mambo mengi kifikra, n.k.
hapo umenena💪
 
Kikwete kathibitisha hilo. Maza alikuwa ni chagua la JK. As we all know, JK huwa anaangalia sura kuliko uwezo. Hasa kwa hiyo jinsia. Teuzi zake nyingi zilisababisha kudilute hai ya ngazi nyingi serikalini hasa Ukuu wa Wilaya.
Na Magufuli alikuwa chaguo la nani.?
 
Nakubaliana na wewe 100 %. Hawa failures wa O level hawawezi kuwa na akili au uwezo ya kuongoza Taifa.
 
Ilikuwa makosa kumweka Magufuli kwenye Urais, mama ndiyo anasafisha madudu ya Magufuli. Hii ni kama Mwinyi alivyosafisha madudu ya nyerere, na Kikwete akaja kusafisha ya Mkapa.

Watende wao ya wenzao huwa mwao.
 
Huu ni mtazamo wako tu kama ambavyo wapo wanaokuona wewe ni mjinga tu na mtu anaejifanya mjuaji ilhali huna la maana ulilofanya katika nchi hii au jamii yako.
 
Alaumiwe kikwete.ndo aliyemleta huyum saa100
 
Anamsikiliza nani wakati watu wamekataa bandari isiuzwe hajawasikiliza? Mara ngapi watu wanaomba kumwambia kero zao anawafukuzia mbali kwa kishindo kikuu? Au ana ka kikundi kake anakokasikiliza? Awamu iliyopita iliwasikiliza na kuwajali wote
Ubunifu gani unausemea ubunifu wa umeme kupanda bei na wakiulizwa kila siku wanakuja na ngonjera, ubunifu wa bando kupanda bei bila maelezo ya msingi? Ubunifu sasa umekuwa nchi kuwa kama ukoo wa kambale.
Wafanya biashara gani wana amani wakati wanagoma kila siku kisa rushwa kutoka kwa kwenye mamlaka? Kariakoo iwe case study.
Kwamba hujui machinga, mama ntilie na wafanya biashara wadogo wadogo ambao wakilala usiku wanaamka na kukuta biashara zao zimevunjwa na kutupiliwa mbali kwa lugha tamu ya kuwapanga? Wengi wao wameshindwa kuendesha maisha yao huku mali zao zikiuzwa na mabenki sababu biashara zao zimeharibiwa na hawawezi kulipa mikopo. Au wewe mwenzetu wafanya biashara unawazungumzia kina MO na GSM tu?
Mbona huzungumzii masai waliotimuliwa Loliondo kumpisha mwarabu? Mbona huzungumzii kukopa kopa kulikopitiliza huku hatujui kinacho kopwa kinatumikaje? Mbona huzungumzii safari za nje zisizohesabika lakini zenye matokeo sifuri huku ziara za ndani zikiishia Mwanza na Arusha kila siku?
 
Magufuli hakuchagua bali alipewa. BTW around 2017 - 2018 Mama alitaka kujiuzulu na JPM alimkubalia ila mzee wa busara alituliza anga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…