Bado hamjachoka na propaganda za kumchafua marehemu?Kila mwenye akili timamu anajua kuwa Magufuli alikuwa Rais wa hovyo na mwovu. RAIS ambaye alikuwa anakiri hadharani kuwa pesa za serikali ni pesa zake. Alikuwa akisema "pesa zangu". Alikuwa na uhuru wa kuchota mihera ya serikali na kuigawa kwa siri na hadharani ili ajiimarishe kisiasa.
RAIS Samia ni Rais muadilifu haswa , tatizo ni kwamba amekuwa dhaifu kupitiliza.
Kitendo cha kuongea na waajiriwa wake wezi na kuwaambia wampishe nao kumgomea hiyo ni dhahiri kuwa Samia ni dhaifu dhaifu dhaifu. Alishindwa hata kuwataja majina au vyeo vyeo.
Na wasaidizi wake bila shaka hawajitambui au yawezekana nao wanakula pamoja na mafisadi. Walishindwa hata kuandika barua za kuwatengua ambao Samia alisema wampishe.
Power ya Samia ni ndogo sana yawezekana ni ndogo kuliko ya OCD wa wilaya ya Kaliua au Ubungo.
Kila mkipima mnaona bado anapendwa hivyo kuongesa kasi ya uongo wenu.
Eti Rais wa ovyo na mwovu.
Kipindi cha Magu ndiyo sheria ziliheshimiwa kupita vipindi vyote! Siyo sheria za barabarani, sheria za kulipa kodi, sheria za kazi nk. Ndiyo kipindi nilishuhudia hata mahakimu wanahakikisha kesi zinaisha ndani ya muda waliowekewa! Polisi walikuwa na nidhamu! Ukiingia ofisi za umma unasikilizwa. Magu tutamkumbuka daima.
Akiongea dunia inasikiliza. Siyo Afrika tu, Ulaya na marekani, walifuatilia mwamba anaongea nini. Ni kutokana na umakini wake na kutokubali kuchezewa chezewa. Watanzania wengi walimpenda ndiyo maana alichaguliwavkwa wingi kwenye uchaguzi ukiacha hizo porojo zenu za wizi wa kura za akina Mdee!