Ungeweza kuuliza swali kwa akili zaidi. Swali lako ni upuuzi mtupu.
Hivi hata wanaposema Hitler aliua wayahudi, ni marehemu wa kiyahudi ndio waliotamka? Hata polisi wanaposema kuwa kuna raia fulani ameuawa na majambazi, ni yule marehemu ndiyo huwa anatamka kuwa, mimi nimeuawa na majambazi? Hivi huyo unayemwuliza, kuwa alimwua yeye, kwa akili yako unaamini kuwa kama ingekuwa ni yeye ndiye aliyeuawa, angekuja kufufukia JF aje kulalamika? Kuuliza swali la kijinga kama hilo, unaonekana ama JF ina wagonjwa wa akili au huna swali, umeamua kuandika tu. Jifunzeni kujenga hoja na siyo kuropoka, mnaharibu jukwaa.
Ukiuuliza swali kama hili unaonekana ni mtu aliyekosa kabisa uelewa hata ule wa binadamu mwenye akili ndogo kabisa.
Tafuta swali lisilodhalilisha ubinadamu wako.