Hayati Magufuli alikuwa Rais mwovu, Samia Suluhu ni Rais dhaifu. Binafsi heri Rais dhaifu kuliko mwovu

Hayati Magufuli alikuwa Rais mwovu, Samia Suluhu ni Rais dhaifu. Binafsi heri Rais dhaifu kuliko mwovu

Bado hamjachoka na propaganda za kumchafua marehemu?
Kila mkipima mnaona bado anapendwa hivyo kuongesa kasi ya uongo wenu.
Eti Rais wa ovyo na mwovu.

Kipindi cha Magu ndiyo sheria ziliheshimiwa kupita vipindi vyote! Siyo sheria za barabarani, sheria za kulipa kodi, sheria za kazi nk. Ndiyo kipindi nilishuhudia hata mahakimu wanahakikisha kesi zinaisha ndani ya muda waliowekewa! Polisi walikuwa na nidhamu! Ukiingia ofisi za umma unasikilizwa. Magu tutamkumbuka daima.

Akiongea dunia inasikiliza. Siyo Afrika tu, Ulaya na marekani, walifuatilia mwamba anaongea nini. Ni kutokana na umakini wake na kutokubali kuchezewa chezewa. Watanzania wengi walimpenda ndiyo maana alichaguliwavkwa wingi kwenye uchaguzi ukiacha hizo porojo zenu za wizi wa kura za akina Mdee!
Eti marehemu anapendwa, labda kama anapendwa na mamako. Where is 1.5T?
 
Tulishawaomba ushahidi wa uovu wake, cha ajabu kinachoelezwa ni tetesi tu na uzushi.
Hebu tuambieni kwa ushahidi halisi (vivid evidence) kwamba alikuwa mwovu

Ushahidi wa mwenye udhaifu najua uko dhahiri hata watoto wadogo wanaweza kuuonesha
Jiwe alikuwa muuaji!!!!!!!!!!!!
 
Kila mwenye akili timamu anajua kuwa Magufuli alikuwa Rais wa hovyo na mwovu. RAIS ambaye alikuwa anakiri hadharani kuwa pesa za serikali ni pesa zake. Alikuwa akisema "pesa zangu". Alikuwa na uhuru wa kuchota mihera ya serikali na kuigawa kwa siri na hadharani ili ajiimarishe kisiasa.

RAIS Samia ni Rais muadilifu haswa , tatizo ni kwamba amekuwa dhaifu kupitiliza.

Kitendo cha kuongea na waajiriwa wake wezi na kuwaambia wampishe nao kumgomea hiyo ni dhahiri kuwa Samia ni dhaifu dhaifu dhaifu. Alishindwa hata kuwataja majina au vyeo vyeo.

Na wasaidizi wake bila shaka hawajitambui au yawezekana nao wanakula pamoja na mafisadi. Walishindwa hata kuandika barua za kuwatengua ambao Samia alisema wampishe.

Power ya Samia ni ndogo sana yawezekana ni ndogo kuliko ya OCD wa wilaya ya Kaliua au Ubungo.
Yes magufuri alikuwa mwovu/shetani

Yes Samia muadilifu lakini sio dhaifu anafuata utawala wa sheria
 
Mnavomsema jiwe ni kama hamuoni ujinga unaofanyika saivi pesa zinaliwa walaji wanaambiwa wale kwa urefu wa kamba zao hawawajibishwi wanaitwa wapumbavu tu na wanasonywa basi wakati walipa kodi hamtakiwi hata kufanya u machinga barabarani. Mnavoambiwa kwamba swala la Uhuru wa miiliyenu lisiwahusishe watoto yan kwamba ni green light to #LGBTQ

Mko apa mnamjadili marehemu tu na hamna fact za kueleweka asa kama alikua na weakness na hamkuzisema kipindi kile na weakness za huyu pia mtazisema akishakufa Akhii nji nzima itavaa pedi
 
Kwa hili la kuchaguliwa napinga, Magufuli aliua mihimili yote ikawa vibogoyo, bunge kibogoyo, mahakama kibogoyo, yeye tu akawa jeshi la mtu mmoja, hakuna utawala wa aina hiyo ukawa mzuri.
Kwaiyo utawala wa kuruhusu watu kuiba ma bilioni ya pesa Ili Hali wengine wakifa Kwa kukosa maji safi umeme wa uhakika.
 
Kwaiyo utawala wa kuruhusu watu kuiba ma bilioni ya pesa Ili Hali wengine wakifa Kwa kukosa maji safi umeme wa uhakika.
Watu hawajali as long as circle zao hazipati madhara na sio kwamba hazipati madhara sijui n upofu wa kifikra labda
 
Ungeweza kuuliza swali kwa akili zaidi. Swali lako ni upuuzi mtupu.

Hivi hata wanaposema Hitler aliua wayahudi, ni marehemu wa kiyahudi ndio waliotamka? Hata polisi wanaposema kuwa kuna raia fulani ameuawa na majambazi, ni yule marehemu ndiyo huwa anatamka kuwa, mimi nimeuawa na majambazi? Hivi huyo unayemwuliza, kuwa alimwua yeye, kwa akili yako unaamini kuwa kama ingekuwa ni yeye ndiye aliyeuawa, angekuja kufufukia JF aje kulalamika? Kuuliza swali la kijinga kama hilo, unaonekana ama JF ina wagonjwa wa akili au huna swali, umeamua kuandika tu. Jifunzeni kujenga hoja na siyo kuropoka, mnaharibu jukwaa.

Ukiuuliza swali kama hili unaonekana ni mtu aliyekosa kabisa uelewa hata ule wa binadamu mwenye akili ndogo kabisa.

Tafuta swali lisilodhalilisha ubinadamu wako.
Mnaoneka hayawani nyie mnaosema JPM ni muuaji Kwa Sababu mnasahau hata awamu ya kikwete hata mkapa watu wengi tu waliuawa.ndo maana hapa mnapata negative comments nyingi Kwa maoni yenu yaliyo ovyo.nafuu mnyamazr Tu msijiaibishe.
 
Back
Top Bottom