Habari wana-JF
Kama mnakumbukumbu vizuri wakati wa awamu ya Magufuli kipindi cha mwanzoni kulikuwa na uhuru mkubwa sana wa kuongea na hata vyama vya upinzani vikawa vinafanya shughuli za mikutano ya kisiasa unajua nini kilibadilika baadae?
Ni pale ambapo badala ya vyama vya upinzani vijikite kwenye hoja kushambulia awamu yake badala yake wakaanza kumtukana matusi mara wanamwita nyapara wa barabara n.k , walimzomea bungeni na kutoka nje wakati wa kuhutubia bunge, maneno yalikuwa mengi kwa upinzani kupinga uraisi wake.
Kupitia haya na mengine ndipo Magufuli kapiga marufuku mikutano ya kisiasa kwasababu badala ya watu wajikite kwenye hoja badala yake wanafanya personal attack na akaona kwa Tanzania wanaamini ili kuwe demokrasia ni pale tu kutakuwepo na uhuru wa kutukana na kudhalilishana ndio maana akaenda mbali zaidi.
Nikija kwenye huu uongozi wa Mama Samia ameona kuwa na uhuru wa kuongea na kuimairisha demokrasia ndio maana akaruhusu mikutano ya kisiasa, akawaachia wanasiasa wa upinzani walikuwa jela lengo ni kuifanya Tanzania wawe wamoja.Japo Mimi binafsi sio muumini wa hii awamu ila kwenye hili ni lakupongeza pamoja na kufanya hivi watu wanatumia uhuru huo vibaya ndio maana Magufuli aliona hili mapema.
Kwanini mnatukana huyu Mama kuna haja gani? Kwanini hatuwezi kuwasilisha hoja zetu bila matusi na udhalilishaji na kizuri ameshawaeleza kama kuna vitu hulizishwi navyo awamu yake ongea watavifanyia kazi, kama no kukosoa kosoa muhimu usivunje sheria na kuwe na mipaka kwa hivi mnavyomtukana nae akaamua kuchukua maamuzi ya awamu ya Magufuli kuhusu demokrasia mtasema amewaonea?