Hayati Magufuli alikuwa 'system disruptor', kwa bahati mbaya hakuimaliza kazi, kwa sasa hakuna tumaini tena

Hayati Magufuli alikuwa 'system disruptor', kwa bahati mbaya hakuimaliza kazi, kwa sasa hakuna tumaini tena

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2020
Posts
4,437
Reaction score
13,836
Ili Tanzania mpya izaliwe, ilikuwa ni lazima ile ya zamani ife. Hapa nazungumzia 'system' ya zamani. Yale makundi ya watu yaliyohodhi madaraka na mamlaka ya nchi, ambayo yanabadilishana tu kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

JPM, labda kwa bahati mbaya au kwa mipango madhubuti ya wazalendo alikwenda ikulu kwa kazi hiyo. Ilikuwa ni vita kwelikweli.

Kwenye madaraka haitakiwi kuacha 'vacuum', unapo ua system ya zamani ni lazima ujenge 'sytem' mpya. System ya JPM ilikuwa bado changa, haina mizizi wala mtaji wa watu kwenye chama na serikali. Na sasa imefagiliwa mbali.

'System' ya zamani imeshinda vita na imerudi madarakani, Tanzania ya zamani inasonga mbele. Kwasasa hakuna matumaini tena ya kuziondoa zile familia za kifalme kwenye madaraka ya nchi.

RIP JPM, you tried.
 
System hii ya akina Bashiru, Makonda, Sabaya, Ally Hapy, Polepole, Mpango, Mnyeti
Nadhani kwenye system yake alipanga kuwajaza wasomi wa vyuo vikuu na watu wengine aliowainua toka jalalani.

Somehow the gaps had to be filled with the available human resources.

Akina Happy, Sabaya na Bashite ni kwa ajili ya kufanya 'dirty work' ambayo ni lazima iwepo wakati wa kuvunja mfumo wa zamani. Hauwezi kuwatuma wa jalalani kufanya kazi hizo
 
Waona mbali hua wanatazama 'big picture', JPM alikuwa na mapungufu mengi, lakini inawezekana waliona yanavumilika ili tu kazi ikamilike.
Alipaswa a-deal na "kurupt sistim" moja kwa moja bila athari kwa watazamaji/wananchi wengine.

Badala yake vumbi la upupu na pilipili liliegemea zaidi kwa wananchi wa kawaida ambao hawakuwa ndani ya hiyo sistim!
 
Ili Tanzania mpya izaliwe, ilikuwa ni lazima ile ya zamani ife. Hapa nazungumzia 'system' ya zamani. Yale makundi ya watu yaliyohodhi madaraka na mamlaka ya nchi, ambayo yanabadilishana tu kutoka kizazi kimoja hadi kingine...
System ya Magufuli ya upendeleo, utekaji nyara, ubambikaji kesi na kodi, wizi wa wazi kama tril 1.5, ukabila hadi kuhisi kuna Sukuma Gang.

System hiyo haiwezi kuwa endelevu popote duniani.
 
Hivi ni kweli tunamuomba MUNGU atusaidie nchi yetu itoke kwenye tope lililokwamisha maendeleo?

Ikiwa ni kweli wewe nikiongozi basi Muombe MUNGU akuepushe na Kiburi,upendeleo na ubinafsi.

Jitenganishe wewe na taasisi mfano MGONI wako akija kuomba huduma sizizohusiana na kesi yako ya ugoni muhudumie kama taasisi.Usirithi maadui wa rafiki yako.

Kwenye uchaguzi kuwe na fair ground.
 
Nadhani kwenye system yake alipanga kuwajaza wasomi wa vyuo vikuu, na watu wengine aliowainua toka jalalani.

Somehow the gaps have to be filled with the available human resources.

Akina Happy, Sabaya na Bashite ni kwa ajili ya kufanya 'dirty work' ambayo ni lazima iwepo wakati wa kuvunja mfumo wa zamani. Hauwezi kuwatuma wa jalalani kufanya kazi hizo
Hizi ni takataka haziwa na binu hata kidogo zaidi ya mabavu
 
Back
Top Bottom