Hayati Magufuli alikuwa 'system disruptor', kwa bahati mbaya hakuimaliza kazi, kwa sasa hakuna tumaini tena

Hayati Magufuli alikuwa 'system disruptor', kwa bahati mbaya hakuimaliza kazi, kwa sasa hakuna tumaini tena

Nadhani kwenye system yake alipanga kuwajaza wasomi wa vyuo vikuu, na watu wengine aliowainua toka jalalani.

Somehow the gaps have to be filled with the available human resources.

Akina Happy, Sabaya na Bashite ni kwa ajili ya kufanya 'dirty work' ambayo ni lazima iwepo wakati wa kuvunja mfumo wa zamani. Hauwezi kuwatuma wa jalalani kufanya kazi hizo
Mfano wa kazi chafu ambazo hao walitakiwa kufanya ni zipi?
 
Yaani sijui itakuwaje, kwa sasa zile familia za kifalme zitajipanga na kuhakikisha makosa ya 2015 hayatokei tena. Wanakwenda kushika hatamu ndani ya chama na serikali.

Mbona Magufuri kampeleka mwinyi Zanzibar?.

Tena alijaza ndugu zake Kama doto James hazina na heri James uvccm.

Mpaka kabula nyumba ndogo alipata ubunge viti Maalum.
 
Ili Tanzania mpya izaliwe, ilikuwa ni lazima ile ya zamani ife. Hapa nazungumzia 'system' ya zamani. Yale makundi ya watu yaliyohodhi madaraka na mamlaka ya nchi, ambayo yanabadilishana tu kutoka kizazi kimoja hadi kingine...
Baba aliwahi kuniambia kuwa nijichunge sana hapa Tanzania, alisema hii serikali ya CCM ndiyo adui wa haki na kamwe hatutakuja kuendelea tukiwa chini yao.

Waangalie kina Mwinyi, Mkapa, na JK......wamekaa madarakani miaka 30 hakuna cha maana walichokifanya zaidi ya kujilimbikizia mali na kutesa watu. Huyu Mama naye, kila kitu kwake mpaka kithibitishwe na msanii wa Msoga ndipo akifanyie kazi, sijuwi anatupeleka wapi.
 
Ili Tanzania mpya izaliwe, ilikuwa ni lazima ile ya zamani ife. Hapa nazungumzia 'system' ya zamani. Yale makundi ya watu yaliyohodhi madaraka na mamlaka ya nchi, ambayo yanabadilishana tu kutoka kizazi kimoja hadi kingine...
INAFIKIRISHA SANA !!! Pamoja na mapungufu yaliyokuwepo lakini njia imeonyeshwa kwamba kumbe inawezekana ! Hata katika yale tuliyokuwa tukidhani hayawezekani ! Kinachotakiwa ni uzalendo na ujasiri !! ( even Rome was not built in one day )
 
Njia pekee ili system iliyopo sasa ife, sharti upinzani uingie ikulu. Mbali na upinzani kuongoza ni kujidanganya tu.
Vyama vingi havikuanzishwa Tanzania ili siku moja vyama pinzani vishike madaraka.

Na mzizi wa tatizo uko hapo, vyama vingi halikua dai la wananchi, bali CCM iliamua kurejesha mfumo huo ili kuendana na vuguvugu la mabadiliko ya kisiasa la mwishoni mwa miaka ya 80. Ilikua ni badili au ukubali kubadilishwa, CCM wakaamua ku take control ya mabadiliko

Hivyo basi CCM wanajua namna ya kuishi navyo mwaka hadi mwaka. Wanaosema CCM itatawala milele sio wajinga, wanaujua ukweli mchungu.
 
Mbona Magufuri kampeleka mwinyi Zanzibar?. Tena alijaza ndugu zake Kama doto James hazina na heri James uvccm. Mpaka kabula nyumba ndogo alipata ubunge viti Maalum.
Mwinyi alikua anakwenda kupishana na urais wa JMT mwaka 2025.

Kwasasa kila kitu kiko perfectly aligned, wote wanamaliza 2030. Labda mwenyekiti aone aibu.
 
System ya Magufuli ya upendeleo, utekaji nyara, ubambikaji kesi na kodi, wizi wa wazi kama tril 1.5, ukabila hadi kuhisi kuna Sukuma Gang.

System hiyo haiwezi kuwa endelevu popote duniani.
Ukiona mtu ana msimamo kama wa kwako,ujue ni lile kundi la makupe,lkn raia ambae maisha yake yalikuwa yamenyooka,hawezi kumlalamikia jpm,
 
Ili Tanzania mpya izaliwe, ilikuwa ni lazima ile ya zamani ife. Hapa nazungumzia 'system' ya zamani. Yale makundi ya watu yaliyohodhi madaraka na mamlaka ya nchi, ambayo yanabadilishana tu kutoka kizazi kimoja hadi kingin...
Kama kutakua na nia ya kweli kujenga mfumo mpya kiutawala na mustakabali mzm wa maendeleo ya Taifa alipaswa kujenga taasisi imara kupitia katiba mpya!! Na sio kupitia individual.
 
Acha tule tena kwa urefu wa kamba zetu.
Kipindi cha jpm alitufunga shingo sana alimanusura atonyonge kwa kukaza
 
Back
Top Bottom