Hayati Magufuli alimpenda sana Nape Nnauye na alikuwa mwalimu bora kwake, ipo siku Nape atamkumbuka sana Magufuli

Huyo CAG si mpaka alivuliwa uCAG kwasababu hiyo? Au kwakuwa ukweli huo unafichwa unadhani ukweli huo haufahamiki?
Hakuvuliwa UCAG, bali hakuteuliwa kipindi cha pili. Yeye aliteuliwa na Kikwete mwaka 2014 na kipindi chake cha kwanza kikatiba kilikuwa kinakwisha 2019. Baada ya hapo rais aliyeko Madarakani alikuwa anaweza kumteua tena kwa miaka mingine mitano au kuteua mwingine kuongoza taasisi hiyo. Yeye hakuteuliwa kipindi cha pili, katiba iko wazi kabisa kuhusu uteuzi wa CAG. Ni kama Katiba inayosema kuwa Rais atafanya kazi kwa miaka mitano, baada ya hapo anaweza kugomea na kuchaguliwa tena kwa miaka mingine mitano, ila haruhusiwi kuendelea kwa zaidi ya miaka kumi.

Miaka kumi siyo automatic.
 

Wakati anavuliwa mpaka viatu bungeni ili kudhalilishwa tuliona. Hicho kipindi anamaliza muda wake alikuwa ameshadhalilishwa sana, na sababu ni kuweka wazi hiyo 1.5t. Huenda mnadhani ni zamani sana, kiasi kwamba tutakuwa tumesahau jinsi alivyokuwa anatendewa na bunge kwa maagizo ya Magufuli.
 
Kutolewa bastola hadharani na kudhalilishwa ndiyo sawa kwako?
 
Hivi yule msiba yuko wapi siku hizi? Au aliondoka na bwana yule?
 
Kwanza hata hiyo clip ya Prof Assad aliyoiweka, kuanzia dk ya 13.31 Prof Assad anathibitisha ripoti yake na yeye mwenyewe hajawahi kusema kuna wizi wa trilioni 1.5, kilichokuwepo ni tatizo la reconciliation.
 
Hata yeye hakuweka ushahidi kukanusha alichoandika cag. Hivyo hela aliipiga. Rais ambaye alikuwa msafi Ni mmoja tu naye ni Nyerere ndo Mana hasemwi. Rais anayeongoza kusemwa vibaya ni jpm pekee
Hivi, CCM ile aliyoicha kikwete kwa jinsi ilivyokuwa imeoza na kunuka kwa rushwa, wizi,ujangili uliokuwa ukifanywa na viongozi na wanachama haohao unategemea wangempenda mtu aliyeingia madarakani na kuanza kufunga mirija na kuwafukuza?
Watanzania tu wasahaulifu sana aisee!
 
If a taarifa ya Kamati ya Bunge ya PAC ambao ndo wanaochambua ripoti za CAG imesema wazi hapakua na upotevu wa 1.5T
 
Hata yeye hakuweka ushahidi kukanusha alichoandika cag. Hivyo hela aliipiga. Rais ambaye alikuwa msafi Ni mmoja tu naye ni Nyerere ndo Mana hasemwi. Rais anayeongoza kusemwa vibaya ni jpm pekee
Yeye anawekaje ushahidi? Kwani ripoti ya CAG inajadiliwa na kujibiwa na Rais. Hii inaonesha dhahiri ulivyo mpumbavu usiejua chochote bendera fuata upepo. Kama JPM ameiba hizo hela atakua amezificha wapi? Ana utajiri aliouacha kutokana na hizo fedha? Amekufa Sasa, si ingekua vizuri hizo pesa zikachukuliwa au Mali zake zitaifishwe kwa maslahi ya taifa. Haya maswali mbona hamuwaulizi majuha wenzenu kina zitto waliozusha uongo huu.
 
Ukipata nafasi ya kutubu dhambi zako kabla ya kifo chako, hiyo ni ishara ya kuwa mtu mwema wachache sana hupata nafasi hii.
 
If a taarifa ya Kamati ya Bunge ya PAC ambao ndo wanaochambua ripoti za CAG imesema wazi hapakua na upotevu wa 1.5T
Ni watanzania wachache tu wanaokubaliana na huo uwongo wa Zitto kuhusu hiyo 1.5t ambao unatokana na chiki zake binafsi dhidi ya Magufuli.
 
Ulikunya creti ya bia au ulitaga creti ya bia?
 
Umesahau kuwa awamu ya Kikwete ndiyo awamu pekee iliyowafunga mpaka mawaziri kwa ufisadi?

Tanzania hatujapata Rais bora na mwenye muono mpana na aliyeibadilisha Tanzania kama Kikwete.

Nyingi ya "tuhuma" kwa Kikwete ni uongo mtupu na propaganda za majitaka tu.

Tunasubiri sasa wale wale waanzishe shutuma kwa Mama. Tunawaona mitandaoni humu wakijitahidi kurusha uongo uleule wa propaganda za kijinga. Wenye kufikiri tunafahamu yanaanzia wapi hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…