Alipopokonywa uwaziri, Nape alikaa akajitathmini, na baadaye akaamua kwenda kuomba radhi kwa Magufuli. Magufuli mwenyewe alisema hadharani kwamba alikuwa akipokea maombi mengi tu kwamba Nape anataka kuja kumuomba radhi. Siku ya siku kibali kikatoka; tukamuona Nape akitembea kipande kirefu tu ndani ya Ikulu kwenda kumuona Rais. Akamwambia mimi ni kijana tu, nilipotoka na sasa nimeona makosa yangu. Naomba unisamehe. Rais akasema kukosea ni ubinadamu. Maadam umeona uliyokosea na unaomba msamaha, mimi ninakusamehe.
Leo hii, Nape anarusha ndogondogo kwamba Magufuli alikuwa mbaya sana. Sasa huo msamaha ulioomba ulikuwa wa nini? Hypocrisy tu? Hata huko kumsifia Samia unakofanya hivi sasa, tutajuaje kama utaendelea hivyo hivyo hata baada ya Samia kutokuwa madarakani? Baada ya kuona uliyomfanyia Magufuli, siwezi kuwa na imani na wewe.