Hayati Magufuli alionesha mara kadhaa kuwa ni mgonjwa wa moyo

Kama ni hivyo mbona alikuwa anasema safari za nje ni anasa na kuwananga waliotangulia?
 
Daktari wake naona umefafanua vizuri sana
 
Itakuwa uchizi kuamini amekufa na Ugonjwa wa moyo tu, ili hali aliwwza kuuahi nao miaka yote, alitakiwa ajilinde sana na corona kutokana na afua yake lakini alipuuzia ndiyo hivyo tena.
Hatusemi sana lakini tujihadhari na corona ipo na inauwa hapa nilipo nomepata msiba wa mama mkwe wangu leo.
 
Hujaandika cha maana... HII sijawahi isikia ikisemwa kwenye public
 
Wakati Lowassa akigombea urais kupitia Chadema kuna watu waliookuwa wana mkejeli kwa maradhi yake Frederick Sumaye alipowajibu alitupa hint kwa kusema
"...kwani Magufuli naye ni mzima?'
Ndipo akaanza kupiga pushups.
 
Rais alikuwa shupavu la sivyo angeshaachana na siasa siku nyingi..
R.I.P
 
Sasa ndiyo napata jibu ni kwanini alikuwa hapendi kupanda ndege mara kwa mara, na kwa upande mwingine naona namna tulivyo muonea na kumhukumu mtu huyu bila kuujua ukweli!!
How I wish angetufahamisha ili baadhi ya maneno ya kumkejeli kuhusu uwezo wake wa kutumia kimombo ungepungua..ilifika wakati nikajiuliza kama hajui kimombo,si angetembelea nchi kama Urusi,ufaransa,ujerumani,japani, Scandinavian countries au ata Koreas... anyways now watawala wajifunze kutumia power of information..inasaidia Sana kupunguza sintofahamu katika jamii.
 
Nakubaliana nawe kwa mengi, lakini hilo la "ametutoka kwa miujiza!" Hapana! Hapana!
Kifo chake ni cha kawaida tu kama binadamu wengine. Ungekuwa miujiza kama angepaa kwenda mbinguni kama nabii Eliya.
 
Amekaa aka 5 tu madarakani impact yake ya maendeleo tumeiona kwa macho.Mungu amlaze pema peponi......
Yy aliyemuumba alikuwa na makusudi yake jina lake lihimidiwe.....
wale wazee wa kuchonga ngenga mnaweza kuendelea haina kwere
Nimejifunza kitu kwa watu ambao hawadumu muda mrefu;
Hufanya mambo makubwa na magumu kwa haraka haraka sana
 
Umbea
 
Gonjwa lolote laweza kumpata yeyote hivyo kukanusha au kuficha haisadii mtu.
Nadhani tumejifunza kitu maana tulianza kuficha muda mrefu, bila kupima, bila takwimu tukaamini ndio njia sahihi.
 
Hii wengi tumejiuliza , pengine ndio maana hakupenda kusafiri
 
Maneno kuntu!
 
Pole sana mkuu!

Rais Magufuli ni aina ya watu wenye energy na determination sana, na aina ya watu hao kitu pekee cha kuwastopisha ni kifo tu.

Ndio maana suala la corona aliliona ni kikwazo katika determination yake akaamua kulipuuza. Kwake ilikuwa bora afie vitani kuliko kujikunyatia ndani kwa sababu ya corona. Kwake suala la maendeleo ya nchi ilikuwa suala la vita. You either win or lose, but retreating is not an option.

Amekufa kishujaa, na kumbukumbu yake itabaki kama Rais bora kabisa wa nchi yetu, baada ya baba wa taifa.
 
Ilikuwaje akagombea nafasi kubwa namna hiyo ambayo imejaa stress, ugonjwa wa moyo na stress havitakiwi kukaa pamoja..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…