Wanaomshambulia Magufuli wote wanasukumwa na chuki binafsi hayo mengine ni blah bkah tu.Mnavyo mtetea!! 🙄 Sasa kama alijua fika ana hayo matatizo, si angejipumzikia tu!! Alikuwa ni mbunge na waziri kwa miaka 20! Kipi kilichomvutia kugombea Urais? Tena kwa awamu mbili!! 😟
Yaani hapa ishu ni kwamba corona ya awamu hii ya pili inawasakama sana watu wenye umri mkubwa na wale wenye magonjwa sugu ya kuambukizwa na pia yale yasiyo ya kuambukizwa.
Kwa bahati mbaya na mzee naye amekutwa na huo mkasa. Tukubali matokeo, na pia tuendelee kuchukua tahadhari. Full stop!!😇
Hayo matatizo ya moyo amekaa nayo tangu akiwa anasoma Master degree miaka takribani thelathini. Na katika miaka hiyo 30 ameifanyia makubwa sana nchi hii: yeye ndiye baba wa miundombinu tangu akiwa waziri na hadi alipokuwa Rais. Pili alikomesha ufisadi uliokuwa umetalaki serikalini .
Hivi uliona wapi mtu anaacha kazi ili asubiri kifo? Mbona wale wanaomkosoa wao hawakai wakasubiri vifo vyao na wanaendelea na kazi zao? Kifo ni siri ya Mwenyezi Mungu kila mmoja kitamfika kwa namna yake lakini hatutakiwi tukae tu kusubiri kifo.
Kimsingi watanzania tumegawanyika makundi mawili tu bila kujali vyama vyetu: wanaotaka kuiba na wanaopinga wizi. Wale wanaopinga wizi wanamunga mkono Magufuli wamo ndani ya CCM na pia nje ya CCM; na wale wanaounga mkono wizi/ufisadi wanampinga JPM na wamo ndani ya CCM na pia vyama vya upinzani.
Watu kama kina Maria wakati wa JK alikuwa anapata sana kazi ya kuwa moderator katika mikutano ya taasisi za serikali na kulipwa pesa lukuki, lakini wakati wa Magufuli alipoteza hizo kazi ndio sababu mojawapo ya kumchukia JPM.
Watu walivyo wajinga eti wanahoji kwa nini aligombea urais! Hivi mtu akiwa anaumwa ndio akae asifanye shughuli? Wao hawaumwi?
Rais Buhari wa Nigeria alilazwa nje ya nchi muda mrefu sana lakini baadae alirejea na bado aligombea urais kwa mara ya pili na hadi sasa yupo. Marais kufia madarakani hutokea na hakuna anayeweza kujua kama yupi atamaliza kipindi chake na yupi hatamaliza. Rais wa Malawi alikufa akiwa madarakani, Rais Mwanawasa wa Zambia naye alifia madarakani; pia huko miaka ya 1979 Rais Neto wa Angola alikufa akiwa anatibiwa huko Urusi. Katiba kwa kulitambua hilo ndio maana imeweka utaratibu mzuri pindi likitokea. Sio marais tu hata wabunge/madiwani pia wanakufa mara tu baada ya kuchaguliwa au wakati wa kampeni. Kifo hakina uhusiano na shughuli anazozifanya mtu.
Kazi alizozifanya JPM zimeacha alama ya kudumu katika nchi hii na zitaendelea kuchangia sana kuchochea ukuaji wa uchumi kwa miaka mingi ijayo.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu ampokee mbinguni, akishafika mbinguni atakuwa mwombezi wa nchi yetu.