Hayati Magufuli alionesha mara kadhaa kuwa ni mgonjwa wa moyo

Hayati Magufuli alionesha mara kadhaa kuwa ni mgonjwa wa moyo

Kama ni hivyo mbona alikuwa anasema safari za nje ni anasa na kuwananga waliotangulia?
 
Magufuli alikuwa na tatizo la moyo muda sana lakini corona ndiyo imesababisha tatizo kuwa kubwa mpaka kumwondoa hili halina mjadala. Corona sio ugojwa na mdudu ambaye analeta matatizo. Magufuli alikuwa na tatizo kubwa na mapigo ya moyo akawekewa kifaa pacemaker cha kusaidia mapigo hayo yakizidi tatizo Corona ilienda na kutibua michipa ya moyo na kufanya pacemaker isifanye kazi na kumpelekea kifo. Hivyo amekufa kwa tatizo la moyo lakini vilevile Corona ndiyo iliongeza hili tatizo. Ni kama cancer tu vitu vingine ndivyo vinakumaliza.

Seif naye kafa kwa kama magufuli lakini sababu ya kupata mpasuko wa damu ni corona
Daktari wake naona umefafanua vizuri sana
 
Itakuwa uchizi kuamini amekufa na Ugonjwa wa moyo tu, ili hali aliwwza kuuahi nao miaka yote, alitakiwa ajilinde sana na corona kutokana na afua yake lakini alipuuzia ndiyo hivyo tena.
Hatusemi sana lakini tujihadhari na corona ipo na inauwa hapa nilipo nomepata msiba wa mama mkwe wangu leo.
 
Pamoja na majonzi ya kuondokewa na mh. Rais lakini ni vema tukakumbuka maisha aliyoishi.

Magufuli kwa kutambua kwamba ana maradhi yasiyotibika alienda kupata kikombe Cha miujiza kwa Babu wa Liliondo . Baadae iligundulika kwamba kikombe kile ulikuwa usanii tu hivyo JPM aliendelea kuwa mgonjwa.

Pili kwa kutambua kwamba ana matatizo ya moyo- Magufuli Mara kadhaa amekuwa akijiepusha kushiriki katika masuala ya simanzi Kama misiba kwa sababu za kiafya.

Hi misiba ya karibuni hasa wa Balozi Kijazi bila Shaka ilimuathiri sana Magufuli.

Naamini si CORONA Wala Mabeberu

Alale salama.
Hujaandika cha maana... HII sijawahi isikia ikisemwa kwenye public
 
Je, yawezekana pia hayo matatizo yake ya moyo ndo yaliyomfanya asiwe anasafiri sana hususan nchi za nje?

Manake wakati mwingine ujinga unaweza ukamfanya mtu amhukumu kimakosa mtu mwingine.

Sisi tulikuwa tukitania ni kwa sababu alikuwa haongei vizuri Kiingereza na ndo maana alikuwa hasafiri sana kwenda nchi za nje.

Nimelifikiria sana hili suala na naona lina make sense.

Dah! I wish I knew he had some serious heart problems.
Wakati Lowassa akigombea urais kupitia Chadema kuna watu waliookuwa wana mkejeli kwa maradhi yake Frederick Sumaye alipowajibu alitupa hint kwa kusema
"...kwani Magufuli naye ni mzima?'
Ndipo akaanza kupiga pushups.
 
Je, yawezekana pia hayo matatizo yake ya moyo ndo yaliyomfanya asiwe anasafiri sana hususan nchi za nje?

Manake wakati mwingine ujinga unaweza ukamfanya mtu amhukumu kimakosa mtu mwingine.

Sisi tulikuwa tukitania ni kwa sababu alikuwa haongei vizuri Kiingereza na ndo maana alikuwa hasafiri sana kwenda nchi za nje.

Nimelifikiria sana hili suala na naona lina make sense.

Dah! I wish I knew he had some serious heart problems.
Rais alikuwa shupavu la sivyo angeshaachana na siasa siku nyingi..
R.I.P
 
Sasa ndiyo napata jibu ni kwanini alikuwa hapendi kupanda ndege mara kwa mara, na kwa upande mwingine naona namna tulivyo muonea na kumhukumu mtu huyu bila kuujua ukweli!!
How I wish angetufahamisha ili baadhi ya maneno ya kumkejeli kuhusu uwezo wake wa kutumia kimombo ungepungua..ilifika wakati nikajiuliza kama hajui kimombo,si angetembelea nchi kama Urusi,ufaransa,ujerumani,japani, Scandinavian countries au ata Koreas... anyways now watawala wajifunze kutumia power of information..inasaidia Sana kupunguza sintofahamu katika jamii.
 
Keshamaliza zamu yake, bado yako na yangu, tengeneza maisha yako kabla hujatembelewa na umauti, haitasaidia kumsema vibaya zamu zetu ziko palepale iwe Kwa magonjwa ama ajali ama vyovyote vile

Mwacheni apumzike Jembe

Aliingia kwenye kinyang'anyilo cha Uraisi Kwa miujiza, kafanya kazi zake nyingi na kubwa Kwa miujiza na ametutoka Kwa miujiza kwani hakuna aliyefahamu kuwa ataondoka
Nakubaliana nawe kwa mengi, lakini hilo la "ametutoka kwa miujiza!" Hapana! Hapana!
Kifo chake ni cha kawaida tu kama binadamu wengine. Ungekuwa miujiza kama angepaa kwenda mbinguni kama nabii Eliya.
 
Amekaa aka 5 tu madarakani impact yake ya maendeleo tumeiona kwa macho.Mungu amlaze pema peponi......
Yy aliyemuumba alikuwa na makusudi yake jina lake lihimidiwe.....
wale wazee wa kuchonga ngenga mnaweza kuendelea haina kwere
Nimejifunza kitu kwa watu ambao hawadumu muda mrefu;
Hufanya mambo makubwa na magumu kwa haraka haraka sana
 
Pamoja na majonzi ya kuondokewa na mh. Rais lakini ni vema tukakumbuka maisha aliyoishi.

Magufuli kwa kutambua kwamba ana maradhi yasiyotibika alienda kupata kikombe Cha miujiza kwa Babu wa Liliondo . Baadae iligundulika kwamba kikombe kile ulikuwa usanii tu hivyo JPM aliendelea kuwa mgonjwa.

Pili kwa kutambua kwamba ana matatizo ya moyo- Magufuli Mara kadhaa amekuwa akijiepusha kushiriki katika masuala ya simanzi Kama misiba kwa sababu za kiafya.

Hi misiba ya karibuni hasa wa Balozi Kijazi bila Shaka ilimuathiri sana Magufuli.

Naamini si CORONA Wala Mabeberu

Alale salama.
Umbea
 
Watanzania tumeshazoea kudanganywa. Tulidanganywa kabla ya uhuru, baada ya uhuru na hadi sasa tunadanganywa. Na kila tukidanganywa tunakunya na excuses za ku justify tulivyodanganywa. Wewe ulioleta hii topic hapa hata kama ingelitangazwa kuwa marehemu amefariki kwa maradhi ya kuharisha basi ungelikubali tu bila ya kuuliza masuali simple tu kuthibitisha ulichaombiwa. Kuna suali simple tu "kwa nini wananchi walifichwa na kudanganywa juu ya hali ya raisi wao kwa wiki nne, iwe alikuwa anasumbuliwa na maradhi yeyote yale, kwa nini viongozi walikana kuwa anaumwa? Kama nilivyosema sio kosa lako, ni jambo la mazoea. Unaishi nchi isiyokuwa na uhuru wa kuuliza, hakuna uhuru wa waandishi wa habari na hakuna uhuru wa mtu kujieleza hadharani.
Gonjwa lolote laweza kumpata yeyote hivyo kukanusha au kuficha haisadii mtu.
Nadhani tumejifunza kitu maana tulianza kuficha muda mrefu, bila kupima, bila takwimu tukaamini ndio njia sahihi.
 
Je, yawezekana pia hayo matatizo yake ya moyo ndo yaliyomfanya asiwe anasafiri sana hususan nchi za nje?

Manake wakati mwingine ujinga unaweza ukamfanya mtu amhukumu kimakosa mtu mwingine.

Sisi tulikuwa tukitania ni kwa sababu alikuwa haongei vizuri Kiingereza na ndo maana alikuwa hasafiri sana kwenda nchi za nje.

Nimelifikiria sana hili suala na naona lina make sense.

Dah! I wish I knew he had some serious heart problems.
Hii wengi tumejiuliza , pengine ndio maana hakupenda kusafiri
 
Keshamaliza zamu yake, bado yako na yangu, tengeneza maisha yako kabla hujatembelewa na umauti, haitasaidia kumsema vibaya zamu zetu ziko palepale iwe Kwa magonjwa ama ajali ama vyovyote vile

Mwacheni apumzike Jembe

Aliingia kwenye kinyang'anyilo cha Uraisi Kwa miujiza, kafanya kazi zake nyingi na kubwa Kwa miujiza na ametutoka Kwa miujiza kwani hakuna aliyefahamu kuwa ataondoka
Maneno kuntu!
 
Itakuwa uchizi kuamini amekufa na Ugonjwa wa moyo tu, ili hali aliwwza kuuahi nao miaka yote, alitakiwa ajilinde sana na corona kutokana na afua yake lakini alipuuzia ndiyo hivyo tena.
Hatusemi sana lakini tujihadhari na corona ipo na inauwa hapa nilipo nomepata msiba wa mama mkwe wangu leo.
Pole sana mkuu!

Rais Magufuli ni aina ya watu wenye energy na determination sana, na aina ya watu hao kitu pekee cha kuwastopisha ni kifo tu.

Ndio maana suala la corona aliliona ni kikwazo katika determination yake akaamua kulipuuza. Kwake ilikuwa bora afie vitani kuliko kujikunyatia ndani kwa sababu ya corona. Kwake suala la maendeleo ya nchi ilikuwa suala la vita. You either win or lose, but retreating is not an option.

Amekufa kishujaa, na kumbukumbu yake itabaki kama Rais bora kabisa wa nchi yetu, baada ya baba wa taifa.
 
Ilikuwaje akagombea nafasi kubwa namna hiyo ambayo imejaa stress, ugonjwa wa moyo na stress havitakiwi kukaa pamoja..
 
Back
Top Bottom