Hayati Magufuli alionesha mara kadhaa kuwa ni mgonjwa wa moyo

Wanaomshambulia Magufuli wote wanasukumwa na chuki binafsi hayo mengine ni blah bkah tu.
Hayo matatizo ya moyo amekaa nayo tangu akiwa anasoma Master degree miaka takribani thelathini. Na katika miaka hiyo 30 ameifanyia makubwa sana nchi hii: yeye ndiye baba wa miundombinu tangu akiwa waziri na hadi alipokuwa Rais. Pili alikomesha ufisadi uliokuwa umetalaki serikalini .
Hivi uliona wapi mtu anaacha kazi ili asubiri kifo? Mbona wale wanaomkosoa wao hawakai wakasubiri vifo vyao na wanaendelea na kazi zao? Kifo ni siri ya Mwenyezi Mungu kila mmoja kitamfika kwa namna yake lakini hatutakiwi tukae tu kusubiri kifo.
Kimsingi watanzania tumegawanyika makundi mawili tu bila kujali vyama vyetu: wanaotaka kuiba na wanaopinga wizi. Wale wanaopinga wizi wanamunga mkono Magufuli wamo ndani ya CCM na pia nje ya CCM; na wale wanaounga mkono wizi/ufisadi wanampinga JPM na wamo ndani ya CCM na pia vyama vya upinzani.

Watu kama kina Maria wakati wa JK alikuwa anapata sana kazi ya kuwa moderator katika mikutano ya taasisi za serikali na kulipwa pesa lukuki, lakini wakati wa Magufuli alipoteza hizo kazi ndio sababu mojawapo ya kumchukia JPM.

Watu walivyo wajinga eti wanahoji kwa nini aligombea urais! Hivi mtu akiwa anaumwa ndio akae asifanye shughuli? Wao hawaumwi?

Rais Buhari wa Nigeria alilazwa nje ya nchi muda mrefu sana lakini baadae alirejea na bado aligombea urais kwa mara ya pili na hadi sasa yupo. Marais kufia madarakani hutokea na hakuna anayeweza kujua kama yupi atamaliza kipindi chake na yupi hatamaliza. Rais wa Malawi alikufa akiwa madarakani, Rais Mwanawasa wa Zambia naye alifia madarakani; pia huko miaka ya 1979 Rais Neto wa Angola alikufa akiwa anatibiwa huko Urusi. Katiba kwa kulitambua hilo ndio maana imeweka utaratibu mzuri pindi likitokea. Sio marais tu hata wabunge/madiwani pia wanakufa mara tu baada ya kuchaguliwa au wakati wa kampeni. Kifo hakina uhusiano na shughuli anazozifanya mtu.

Kazi alizozifanya JPM zimeacha alama ya kudumu katika nchi hii na zitaendelea kuchangia sana kuchochea ukuaji wa uchumi kwa miaka mingi ijayo.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu ampokee mbinguni, akishafika mbinguni atakuwa mwombezi wa nchi yetu.
 
Suala La Moyo liliongelewa Sana na Aliyekuwa wazuri Mkuu awamu ya tatu Bwana Frederic Sumaye.
Sumaye alisisitiza kuwa Magufuli asipewe Nchi na kusababisha Rais apige Pushap kuonyesha yupo Fiti.


Tunamshukuru Mungu kwa Maisha Ya Rais Magufuli.
Apumzike kwa Amani.
 
Sasa ndiyo napata jibu ni kwanini alikuwa hapendi kupanda ndege mara kwa mara, na kwa upande mwingine naona namna tulivyo muonea na kumhukumu mtu huyu bila kuujua ukweli!!
Na wanaoitwa wazushi mara kadhaa wamekuwa wakisema, kazimika lakini baada ya muda tunamwona tena. Pia Tabia ya ukatili ilikuwa inamfariji labda alijua hatadumu hivyo alikuwa anafurahi watu wakiumia.
 
Huyu ndo alikuwa mwanaume sasa...sio hao masharobaro wa mjini
 
Gwaji girl atarudi kwenye line aliyemuogopa kandei
 
... halafu hakupenda sana kusafiri nje ya nchi hususan long safaris; kwanza uchovu kwenye midege; pili maswali ya maudhi ambayo angeulizwa yangemuumiza sana! Mliokuwa mnahoji kwanini Magufuli alikuwa hasafiri jibu ndio hilo hayo mengine uzushi!


Kwa hiyo ndo ikabidi kubania na wengine wasisafiri kwa Uhuru ?
 
Itakuwa ndiyo sababu ya yeye kukataa kuvaa barakoa, pumzi ilikuwa ndogo. Naona watu wake wanaiga kukataa kuvaa barakoa. Ngoja tuone.


Huenda ni namna mojwapo ya kumuenzi bwana yule! [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Lwakatale??????????..

We unaumwa au .
 
najiuliza kilichokuwa kinampa ujasiri magufuli wa kuidharau corona ili hali anajijua na tatizo la moyo ni nini sipati jibu
Hakuna mwenye jibu, binafsi nilikuwaga namshangaa hata ujasiri wa kupiga pushup alikuwa anautoa wapi. Apumzike kwa amani, mwendo ameumaliza!
 
Tusimjadili sana wakati ameanzisha somo la historia, na lengo ni yeye aongelewe kwenye hilo somo? Yesu na Muhamad wote ni marehemu kwa sasa na kila siku tunawajadili, nini Magufuli?
Ndiyo Ukweli Wenyewe
Nasema Uongo Ndugu Zangu
😎😎
 
Mimi simshangai bali namkubali kwa kitu kimoja. Akijuia kabisa ana shida ya moyo lakini bado alipata guts za kugombea nafasi ya juu kabisa katika utawala wa nchi yetu ...

Afu kuna pimbi nyingine zina complications ndogo tu kama BP na kisukari zinaogopa hata kuongoza vikao vya familia...

Nilikuwa namdis sana Magu, ila leo nimemvuia kofia rasmi...
 
Na hapo ndipo yale maneno yake akitoa hotuba akisema "mtanikumbuka sana"

yanapopenya ktk mishipa yetu ya damu mpk rohoni,maana ukweli tumeujua sasa

kumbe Rais wetu alikua anajitahidi sana hata kwa kwenda baadhi ya sehemu kadhaa

pamoja na afya yake,nawaza yawezekana hata kuna wakati walimshauri "mzee leo pumzika"

ila yeye akasema hapana Nitajitahidi nitaenda,ila huku nnje kwakutokujua kwetu tulikua tukilalama.

Hakika Tunamkumbuka sasa na tutamkumbuka especialy ME nitamkumbuka mno lkn pia nimejifunza vingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…