Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Wizi hauwezi kwisha,

Lakini Nia na uthubutu wake Kupambana na wezi ndio msingi wa thread hii.

RIP Magu.
 
Unajinadi kuwa uliendelea kusambaza dawa za KULEVYA waziwazi kipindi kile?

Au sijakuelewa.
We kima kwani ushawahi ona mateja wameisha mitaani? Zaidi alifanya dawa zipande Bei tu! Kupambana na wauzaji inahitaji akili na siyo kutaja watu wawili watatu kisa ni mahasimu wako kisiasa
 
Naheshimu mawazo Yako,

Nami naheshimu uamuzi wangu wa kukumbuka maeneo ambayo HAYATI Magufuli aliyatendea HAKI.

Abarikiwe huko aliko.
Usipotoshe Sasa kuwa alikuwa mlinzi sahihi wa pesa za umma, wakati hakuwa anakubali ukaguzi wa fedha za umma. Kibaya zaidi hata hizo ripoti ya fedha za umma ilionyesha yeye ni mfujaji, hiyo ilipelekea kumuondoa kimizengwe msimamizi wa fedha za umma.
 
We kima kwani ushawahi ona mateja wameisha mitaani? Zaidi alifanya dawa zipande Bei tu! Kupambana na wauzaji inahitaji akili na siyo kutaja watu wawili watatu kisa ni mahasimu wako kisiasa
Nilichosema mateja wengi walijisalimisha sobber houses sababu ya kuadimika drugs,

Maana ya wengi ni wengi, wote ni wote.

Soma Kwa kufahamu na kuelewa.
 
Wizi hauwezi kwisha,

Lakini Nia na uthubutu wake Kupambana na wezi ndio msingi wa thread hii.

RIP Magu.
Kama wizi hauwezi kuisha, Hawa unaowalaumu Sasa kuhusu wizi wa fedha za umma unapata wapi uhalali huo? Au umepoteana baada ya kuwekewa rekodi sahihi?
 
Wizi wa Magu hauthibitishwi popote zaidi ya KAZI njema alizolifanyia Taifa.
Aliyetaka kuthibitisha yaani CAG Assad alitimuliwa sasa ulitaka ushahidi utoke wapi?

Kuna watu mna reasoning ya ajabu sana, yaani mtu hataki kukaguliwa alafu uko busy unamsifia kuwa ni msafi.
 
Kama wizi hauwezi kuisha, Hawa unaowalaumu Sasa kuhusu wizi wa fedha za umma unapata wapi uhalali huo? Au umepoteana baada ya kuwekewa rekodi sahihi?
Waliopo jawapasi kulalamika Badala ya kuchukua hatua kama alivyofanya Magu.

Got it?
 
Nilichosema mateja wengi walijisalimisha sobber houses sababu ya kuadimika drugs,

Maana ya wengi ni wengi, wote ni wote.

Soma Kwa kufahamu na kuelewa.
Huna uelewa na hii biashara
Ukiminya Sana ndo unafanya supply ipungue na demand iwe kubwa ...kwa Nini usikamate mateja wote ...weka ndani wataje wanapata wapi dawa unganisha dot mnyororo wote unapatikana
Halafu unapata mapapa ...siyo unakuja kututajia Mara Mr blue,mbowe, gwajima TID au wema sepetu
 
Nimesema Kwa Mfano,

Hilo la wizi wa kura, pia Mimi siliafiki kabisa, kupotoa HAKI ya Sanduku la kura ni jambo baya.

Ingawa hayo hayajadiliwi hapa,

Tunakumbuka mema yake, Hasa katika uchapakazi na kusimamia vizuri pesa za umma zisiporwe na waizi.

Mema yake watu wameuawa huku Zanzibar na wengine wamekuwa vilema wa maisha

RIH Magufuli
 
Tunahitaji mifumo imara na siyo Kiongozi. Tunapopiga kelele tupate Katiba Mpya Bora na Imara tunamaanisha uimarishaji wa Mifumo yetu ya Kiutendaji.

Tukiwa na mifumo imara isiyoyumbishwa wala kuchezewa, hakuna wa kucheza na mali za Umma. Nikupe mfano " ukiwa unaendesha gari (manual transmission) ukawa uko no 5 speed 80, huwezi ku engage reverse gear ikakubali" Kwasababu ya mfumo.

Kiongozi wa Umma anapotenda kinyume basi Mfumo utamkataa. Achaneni na Viongozi Madikteta wanaoamini ktk wao, bali tujengeni mifumo imara kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Aliyetaka kuthibitisha yaani CAG Assad alitimuliwa sasa ulitaka ushahidi utoke wapi?

Kuna watu mna reasoning ya ajabu sana, yaani mtu hataki kukaguliwa alafu uko busy unamsifia kuwa ni msafi.
HOJA yangu Iko kwenye mambo aliyoifanya Magu yanayoonekana, na yanayoshikika,

Sijui kama unaelewa, ndiyo maana sijaquote Ripoti ya CAG sababu Si Rahisi kumuelewesha mkulima, mvuvi kupitia Ripoti ya CAG akaelewa.

Kama hujaelewa Hadi hapo, ni ubishi tu ๐Ÿ˜€
 
Mema yake watu wameuawa huku Zanzibar na wengine wamekuwa vilema wa maisha

RIH Magufuli
Hiyo ni nje ya mada.

Hapa amayejadiliwa ni HAYATI Magu Kwa issues nyeti Bora alizowahi fanya Kwa miaka yake mitano pekee.
 
Hivi zile trilioni 4 ziliibwa na mfumo gani?

TAL alihujumiwa na majambazi wa mfumon gani?

Prof Assad afanywa na mfumo gani?

Nk,nk
 
Ameonyesha njia katika vile ambavyo watu waliamini haviwezekani lakini kwa Magufuli viliwezekana !
Hivyo huko mbele ya safari atakuja kutokea mwingine atafanya hayo kwa ustadi na uangalifu wa hali ya juu na hapo ndipo maendeleo yanayohitajika yatapatikana kwa haraka sana !

Hayati Magufuli aliamini katika ule msemo wa wahenga usemao -
Ukicheka na nyani utavuna mabua !
 
Hivi zile trilioni 4 ziliibwa na mfumo gani?

TAL alihujumiwa na majambazi wa mfumon gani?

Prof Assad afanywa na mfumo gani?

Nk,nk
Yote hayo ni nje ya mada.

Yaezakuwa Magu aliziiba Kisha akanunulia ndege bila kulihusisha bunge.

Au alizichota Akaenda kujenga flyover hapo dar,

Yaezakuwa aliziiba bila kufuata Utaratibu wa kibunge Kisha akajenga JNHP.

Wizi wa aina hiyo ni MWEMA, maana imeondoa jam hapo dar, kivuko kinakamilika hapo Busisi, na meli na vivuko vilinunuliwa.

Sasa tuseme zaidi ya kusema,

HAYATI Magu Abarikiwe
 
Na Kweli aliwatisha ngedere Hasa.

Huwezi msaidia maskini bila Kupambana na aliyemfunga maskini katika Umaskini.

Abarikiwe huko aliko.
 
We mtu uko vizuri sana
 
Betting ipo tangu enzi za Nyerere ๐Ÿ˜‚
Hapana kipindi cha Nyerere hakukuwa hata na simu za digitali wala hakukuwa hata na pampu za kuuzia mafuta za digital !
Mambo ya Casinos yalianzia awamu ya hayati Mzee Mwinyi !
Tulikuwa tunajimwambafay pale Las Vegas Casino Upanga !๐Ÿ˜…
Tulikuwa tunaanzia pale nje Jolly Club ๐Ÿ˜…๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ