Hayati Magufuli aliweza kuwatisha waovu, mifumo iliamka kufanya kazi

Ni propaganda tu ndiyo zilitawala na kutisha vyombo vya habari visiripoti uhalisia. Uwizi wa mali ya umma ulikuwapo kama kawaida. Kama unabisha kaangalie CAG report za 2016-2018, kuna Tsh 2.4 Trillion. CAG Assad alipohoji akamfukuza kazi.

Pili aliwatupa watu wengi rumande kwa hisia bila kufuata utaratibu. Watu hao tuliodhani ni mafisadi walikaa rumande kuanzia 2016/17 hadi mwaka 2021 alipokufa bila Mahakama kusikiliza kesi zao.

Kesi hazikuwa na ushahidi, ila yule Shetani Magufuli akikuchukia tu anakupeleka rumande. Nahisi Magu alikufa ili Tanzania ibaki mahali salama pa kuishi
Wizi hauwezi kwisha,

Lakini Nia na uthubutu wake Kupambana na wezi ndio msingi wa thread hii.

RIP Magu.
 
Unajinadi kuwa uliendelea kusambaza dawa za KULEVYA waziwazi kipindi kile?

Au sijakuelewa.
We kima kwani ushawahi ona mateja wameisha mitaani? Zaidi alifanya dawa zipande Bei tu! Kupambana na wauzaji inahitaji akili na siyo kutaja watu wawili watatu kisa ni mahasimu wako kisiasa
 
Naheshimu mawazo Yako,

Nami naheshimu uamuzi wangu wa kukumbuka maeneo ambayo HAYATI Magufuli aliyatendea HAKI.

Abarikiwe huko aliko.
Usipotoshe Sasa kuwa alikuwa mlinzi sahihi wa pesa za umma, wakati hakuwa anakubali ukaguzi wa fedha za umma. Kibaya zaidi hata hizo ripoti ya fedha za umma ilionyesha yeye ni mfujaji, hiyo ilipelekea kumuondoa kimizengwe msimamizi wa fedha za umma.
 
We kima kwani ushawahi ona mateja wameisha mitaani? Zaidi alifanya dawa zipande Bei tu! Kupambana na wauzaji inahitaji akili na siyo kutaja watu wawili watatu kisa ni mahasimu wako kisiasa
Nilichosema mateja wengi walijisalimisha sobber houses sababu ya kuadimika drugs,

Maana ya wengi ni wengi, wote ni wote.

Soma Kwa kufahamu na kuelewa.
 
Wizi hauwezi kwisha,

Lakini Nia na uthubutu wake Kupambana na wezi ndio msingi wa thread hii.

RIP Magu.
Kama wizi hauwezi kuisha, Hawa unaowalaumu Sasa kuhusu wizi wa fedha za umma unapata wapi uhalali huo? Au umepoteana baada ya kuwekewa rekodi sahihi?
 
Wizi wa Magu hauthibitishwi popote zaidi ya KAZI njema alizolifanyia Taifa.
Aliyetaka kuthibitisha yaani CAG Assad alitimuliwa sasa ulitaka ushahidi utoke wapi?

Kuna watu mna reasoning ya ajabu sana, yaani mtu hataki kukaguliwa alafu uko busy unamsifia kuwa ni msafi.
 
Kama wizi hauwezi kuisha, Hawa unaowalaumu Sasa kuhusu wizi wa fedha za umma unapata wapi uhalali huo? Au umepoteana baada ya kuwekewa rekodi sahihi?
Waliopo jawapasi kulalamika Badala ya kuchukua hatua kama alivyofanya Magu.

Got it?
 
Nilichosema mateja wengi walijisalimisha sobber houses sababu ya kuadimika drugs,

Maana ya wengi ni wengi, wote ni wote.

Soma Kwa kufahamu na kuelewa.
Huna uelewa na hii biashara
Ukiminya Sana ndo unafanya supply ipungue na demand iwe kubwa ...kwa Nini usikamate mateja wote ...weka ndani wataje wanapata wapi dawa unganisha dot mnyororo wote unapatikana
Halafu unapata mapapa ...siyo unakuja kututajia Mara Mr blue,mbowe, gwajima TID au wema sepetu
 
Nimesema Kwa Mfano,

Hilo la wizi wa kura, pia Mimi siliafiki kabisa, kupotoa HAKI ya Sanduku la kura ni jambo baya.

Ingawa hayo hayajadiliwi hapa,

Tunakumbuka mema yake, Hasa katika uchapakazi na kusimamia vizuri pesa za umma zisiporwe na waizi.

Mema yake watu wameuawa huku Zanzibar na wengine wamekuwa vilema wa maisha

RIH Magufuli
 
Tunahitaji mifumo imara na siyo Kiongozi. Tunapopiga kelele tupate Katiba Mpya Bora na Imara tunamaanisha uimarishaji wa Mifumo yetu ya Kiutendaji.

Tukiwa na mifumo imara isiyoyumbishwa wala kuchezewa, hakuna wa kucheza na mali za Umma. Nikupe mfano " ukiwa unaendesha gari (manual transmission) ukawa uko no 5 speed 80, huwezi ku engage reverse gear ikakubali" Kwasababu ya mfumo.

Kiongozi wa Umma anapotenda kinyume basi Mfumo utamkataa. Achaneni na Viongozi Madikteta wanaoamini ktk wao, bali tujengeni mifumo imara kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Aliyetaka kuthibitisha yaani CAG Assad alitimuliwa sasa ulitaka ushahidi utoke wapi?

Kuna watu mna reasoning ya ajabu sana, yaani mtu hataki kukaguliwa alafu uko busy unamsifia kuwa ni msafi.
HOJA yangu Iko kwenye mambo aliyoifanya Magu yanayoonekana, na yanayoshikika,

Sijui kama unaelewa, ndiyo maana sijaquote Ripoti ya CAG sababu Si Rahisi kumuelewesha mkulima, mvuvi kupitia Ripoti ya CAG akaelewa.

Kama hujaelewa Hadi hapo, ni ubishi tu 😀
 
Mema yake watu wameuawa huku Zanzibar na wengine wamekuwa vilema wa maisha

RIH Magufuli
Hiyo ni nje ya mada.

Hapa amayejadiliwa ni HAYATI Magu Kwa issues nyeti Bora alizowahi fanya Kwa miaka yake mitano pekee.
 
Salaam, Shalom.

Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia Hayati Magufuli kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha.

Maeneo yafuatayo, alidhibiti kwelikweli;

1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA

Tumesikia Rais Samia analalamika Badala ya kuamrisha mifumo, asema kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!

Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda kwa kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa hasa.Usingeweza kukwiba pesa ya umma ukabaki salama.

2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.

Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, hilo litoshe kutupa kujua kazi kubwa aliyoifanya hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na Usalama kutenda kazi Kwa viwango vya juu.

3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA

Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri kwa kutapakaa kwa dawa za kulevya, lakini baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za kulevya mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika kazi kubwa underground.

4. UTAKATISHAJI FEDHA

Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za kulevya, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, jambo hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi kwa kuwa Kwa namna moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.

5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI

Vituo vya mafuta kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa kutoa risiti, walitishia kugoma.

Ujasiri wa Magufuli, ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali kutoa EFD bila masharti.

6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI

Ni katika uongozi wa Hayati Magufuli, document za kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.

Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magufuli, alipambana kweli kweli na ufanisi ulionekana.

HITIMISHO

Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya Hayati Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI. Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.

OMBI: Wananchi tunaomba atokee kiongozi atakayefuta BETTING nchini, hivi sasa, vijana wa CCM+ CDM na wasio na vyama wametekwa na jinamizi hili, HAYATI Magu hakuliweza hili. Maisha hayajawahi kuwa Bahati nasibu.

Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania[emoji1241].

Amen.
Hivi zile trilioni 4 ziliibwa na mfumo gani?

TAL alihujumiwa na majambazi wa mfumon gani?

Prof Assad afanywa na mfumo gani?

Nk,nk
 
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania🇹🇿.

Amen.
Ameonyesha njia katika vile ambavyo watu waliamini haviwezekani lakini kwa Magufuli viliwezekana !
Hivyo huko mbele ya safari atakuja kutokea mwingine atafanya hayo kwa ustadi na uangalifu wa hali ya juu na hapo ndipo maendeleo yanayohitajika yatapatikana kwa haraka sana !

Hayati Magufuli aliamini katika ule msemo wa wahenga usemao -
Ukicheka na nyani utavuna mabua !
 
Hivi zile trilioni 4 ziliibwa na mfumo gani?

TAL alihujumiwa na majambazi wa mfumon gani?

Prof Assad afanywa na mfumo gani?

Nk,nk
Yote hayo ni nje ya mada.

Yaezakuwa Magu aliziiba Kisha akanunulia ndege bila kulihusisha bunge.

Au alizichota Akaenda kujenga flyover hapo dar,

Yaezakuwa aliziiba bila kufuata Utaratibu wa kibunge Kisha akajenga JNHP.

Wizi wa aina hiyo ni MWEMA, maana imeondoa jam hapo dar, kivuko kinakamilika hapo Busisi, na meli na vivuko vilinunuliwa.

Sasa tuseme zaidi ya kusema,

HAYATI Magu Abarikiwe
 
Ameonyesha njia katika vile ambavyo watu waliamini haviwezekani lakini kwa Magufuli viliwezekana !
Hivyo huko mbele ya safari atakuja kutokea mwingine atafanya hayo kwa ustadi na uangalifu wa hali ya juu na hapo ndipo maendeleo yanayohitajika yatapatikana kwa haraka sana !

Hayati Magufuli aliamini katika ule msemo wa wahenga usemao -
Ukicheka na nyani utavuna mabua !
Na Kweli aliwatisha ngedere Hasa.

Huwezi msaidia maskini bila Kupambana na aliyemfunga maskini katika Umaskini.

Abarikiwe huko aliko.
 
Wezi wengi wamo ndani ya chama chenu, WAPINZANI Wachache walitumika tu.

Ujenzi wa BWAWA la JNHP ulipingwa Kwa nguvu na watu ndani ya Serikali ukichagizwa na viongozi wa upinzani kukwamisha Magu.

Maslah ya nchi yanatakiwa yatangulizwe mbele,

Uchama hautatufikisha kokote.
We mtu uko vizuri sana
 
Betting ipo tangu enzi za Nyerere 😂
Hapana kipindi cha Nyerere hakukuwa hata na simu za digitali wala hakukuwa hata na pampu za kuuzia mafuta za digital !
Mambo ya Casinos yalianzia awamu ya hayati Mzee Mwinyi !
Tulikuwa tunajimwambafay pale Las Vegas Casino Upanga !😅
Tulikuwa tunaanzia pale nje Jolly Club 😅🙏🙏
 
Back
Top Bottom