- Thread starter
- #61
Ulaya vinchi vingi ni maskini,Kuna Nchi Ulaya ni masikini zaidi yenu?
Bila kuungana vingeshafilisika.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ulaya vinchi vingi ni maskini,Kuna Nchi Ulaya ni masikini zaidi yenu?
Kuanzisha sio tatizo, Bali kumalizia ndio kaziMengi yamewahi kufanyika na yanafanyika,
Kutumia miaka mitano pekee kuanzisha ujenzi SGR, Daraja la Busisi, Flyovers, Ununuzi wa ndege, barabara Nchi nzima,
Jambo Hilo linashtua,
Magu ametupa kujua kuwa nchi yetu Ina pesa nyingi sana zinazopotea Bure.
Mimi siipendi CCM, ila Magu alisababisha tuitazame Nchi yetu Kwa jicho la tofauti.
Baada ya tarehe 17, tutaendelea na spana.
Na waovu wananguvu balaa wanaeeza hata kununua media zote uli kumchafua aliyesimamia hakiSalaam, Shalom.
Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia Hayati Magufuli kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha.
Maeneo yafuatayo, alidhibiti kwelikweli;
1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA
Tumesikia Rais Samia analalamika Badala ya kuamrisha mifumo, asema kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!
Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda kwa kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa hasa.Usingeweza kukwiba pesa ya umma ukabaki salama.
2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.
Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, hilo litoshe kutupa kujua kazi kubwa aliyoifanya hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na Usalama kutenda kazi Kwa viwango vya juu.
3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA
Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri kwa kutapakaa kwa dawa za kulevya, lakini baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za kulevya mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika kazi kubwa underground.
4. UTAKATISHAJI FEDHA
Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za kulevya, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, jambo hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi kwa kuwa Kwa namna moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.
5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI
Vituo vya mafuta kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa kutoa risiti, walitishia kugoma.
Ujasiri wa Magufuli, ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali kutoa EFD bila masharti.
6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI
Ni katika uongozi wa Hayati Magufuli, document za kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.
Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magufuli, alipambana kweli kweli na ufanisi ulionekana.
HITIMISHO
Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya Hayati Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI. Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.
OMBI: Wananchi tunaomba atokee kiongozi atakayefuta BETTING nchini, hivi sasa, vijana wa CCM+ CDM na wasio na vyama wametekwa na jinamizi hili, HAYATI Magu hakuliweza hili. Maisha hayajawahi kuwa Bahati nasibu.
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania[emoji1241].
Amen.
Unajua hela za wamachinga zilikuwa zinaingia kwenye mfuko gani?Ndugu Tindo, hivi wewe unaweza kujua kwanini Serikali imeacha kukusanya 20,000 Kwa matching guys Nchi nzima ambayo ingeingia hazina na kuepusha Nchi kukopa Ili kujenga matundu ya vyoo na madarasa?
Taja nchi Moja ya ulaya iliyo masikini kuliko Tanzania hadi ikashawishika kuungana.Ulaya vinchi vingi ni maskini,
Bila kuungana vingeshafilisika.
Muhimu wananchi tusisahaulishwe aliyoweza kufanya HAYATI Magu Kwa muda mfupi,Na waovu wananguvu balaa wanaeeza hata kununua media zote uli kumchafua aliyesimamia haki
Mkuu acha unafiki Hata nyie CCM hamkumpenda jiweChadema walimuogopa na kumchukia zaid utadhani alikua Mwenyekiti wa Taifa 🐒
mambo ya sijui unafiki ama nini yametoka wap,Mkuu acha unafiki Hata nyie CCM hamkumpenda jiwe
Unalizungumziaje suala la wabunge kupigwa stop kufanya safari za nje?mambo ya sijui unafiki ama nini yametoka wap,
CCM haikumpenda kivip na yeye ndie alikua mwenyekiti na Rais wa nchi tena kwa ngwe2, ambazo moja aliikamilisha viziri sana na ya pili na mambo ya Mungu yakatokea, hapo sina neno....
ati ccm haikumpenda. huenda wewe ndio ulikua ccm na hukumpenda japo si kitu cha ajabu coz huwez pendwa na watu wote.....
uongozi sio jambo la kufurahisha watu, au kukera watu. uomgozi ni kazi mihimu sana ya kuunganusha watu, kuonyesha njia ya kuleta maendeleo kwa watu wote bila kuona haya wala aibu kwa yeyote...Unalizungumziaje suala la wabunge kupigwa stop kufanya safari za nje?
Vipi kuhusu wabunge kudai nyongeza ya mishahara kutupiliwa mbali?
Wewe binafsi kama CCM ulilifurahia?
Sasa utamaliza vipi ikiwa unakopa, pesa zikitolewa hazina kwenda Mahali husika, wahuni wanazikwapua na zinachepushwa kwenye account binafsi?Kuanzisha sio tatizo, Bali kumalizia ndio kazi
Mimi siwajibiki kwenye udhaifu wake, nimejikita kwako kwenye hizo sifa unazomwagia Magufuli. Ulivyokolea kwenye propaganda zake, unadhani hata na sisi tulikolea kwenye zile propaganda kama ww. Ni hivi, alikuwa ni rais aliyeamua kujikita kwenye miundo mbinu, huku akiacha sehemu nyingine kama ajira, utawala Bora nk.Sasa utamaliza vipi ikiwa unakopa, pesa zikitolewa hazina kwenda Mahali husika, wahuni wanazikwapua na zinachepushwa kwenye account binafsi?
Huo ujenzi au KAZI itaisha?
Kwanini kiongozi alalamike Badala ya kuchukua hatua?
Yale masomo ambayo Magu alifaulu vizuri, tungependa viongozi wengine watumie uzoefu huo kufaulu pia.Mimi siwajibiki kwenye udhaifu wake, nimejikita kwako kwenye hizo sifa unazomwagia Magufuli. Ulivyokolea kwenye propaganda zake, unadhani hata na sisi tulikolea kwenye zile propaganda kama ww. Ni hivi, alikuwa ni rais aliyeamua kujikita kwenye miundo mbinu, huku akiacha sehemu nyingine kama ajira, utawala Bora nk.
Magufuli namfanananisha na mwanafunzi anayepata A+ kwenye Somo moja, huku akipata F masomo mengine yote. Hakuna namna unaweza kusema mwanafunzi huyo ni Bora.
Una uhakika gani Magufuli alikomesha wizi,Wakati hakutaka uwazi kwenye serekali yake? Alikuwa anatangaza jambo limekwisha na alizuia watu kutangaza mambo hayo ili ionekane serekali yake imemaliza matatizo hayo. Mfano halisi ni migogoro ya ardhi, hakutaka itangazwe Ili ionekane kamaliza matatizo hayo. Ni kweli migogoro ya ardhi iliisha nchi hii?Yale masomo ambayo Magu alifaulu vizuri, tungependa viongozi wengine watumie uzoefu huo kufaulu pia.
Kwa Yale Magu aliyofail, wahakikishe wao wanayafaulu.
Uongozi ni kupeana vijiti.
Tusingetegemea viongozi waliopo washindwe kusimamia pesa za umma zisiibwe ilhali wanajua nini Magu alifanya kukomesha Hali hiyo.
Weka propaganda pembeni, weka Ripoti za CAG pembeni,Una uhakika gani Magufuli alikomesha wizi,Wakati hakutaka uwazi kwenye serekali yake? Alikuwa anatangaza jambo limekwisha na alizuia watu kutangaza mambo hayo ili ionekane serekali yake imemaliza matatizo hayo. Mfano halisi ni migogoro ya ardhi, hakutaka itangazwe Ili ionekane kamaliza matatizo hayo. Ni kweli migogoro ya ardhi iliisha nchi hii?
Pitia ripoti za CAG kipindi chake kama kweli alimaliza wizi wa fedha za umma. Rejea kufukuzwa kwa CAG professor Assad kisa kuweka ukweli wa fedha za umma, na yeye Magufuli akiwa mmoja wapo wa wafujaji wa pesa hizo. Hakuna anayekukataza kuwa na mahaba na Magufuli, lakini usitake wote tuone alikuwa mzuri hivyo kutokana na propaganda zake, wakati ukweli tunaujua.
Let Truthfulness & Righteousness and Justice, lead the way.Umenena vyema [emoji120]
Ndio maana nimekuambia alifanya vizuri pekee kwenye miundombinu, hata hivyo hata akiwa waziri huko kwenye miundombinu ndio alikofanya vizuri. Urais ni zaidi ya miundombinu pekee. Kwa maneno marahisi hakuwa rais mzuri na hakustahili kuwa rais, maana alikuwa ni mtendaji zaidi kuliko kiongozi.Weka propaganda pembeni, weka Ripoti za CAG pembeni,
Tuangalie vitu , miradi na KAZI zinazoonekana alizofanya Magu Kwa 5 yrs ndizo zitumike kuhalalisha mafanikio au mapungufu ya Magu.
Maeneo ambayo hakufanya vizuri hayajadikiwi katika thread hii, hayo mapungufu ya Magu,anayajua vizuri Erythrocyte
Hapo nakubaliana nawe.Ndio maana nimekuambia alifanya vizuri pekee kwenye miundombinu, hata hivyo hata akiwa waziri huko kwenye miundombinu ndio alikofanya vizuri. Urais ni zaidi ya miundombinu pekee. Kwa maneno marahisi hakuwa rais mzuri na hakustahili kuwa rais, maana alikuwa ni mtendaji zaidi kuliko kiongozi.
Kwa taarifa yako hata kaburu Pieter Botha aliijenga Africa kusini sana kimiundombinu kuliko Magufuli hapa kwetu, lakini ni wapi unaona akisifiwa kuwa ni kiongozi mzuri? Mandela hakujenga miundombinu yoyote mikubwa zaidi ya Pieter Botha, lakini anasifiwa kuwa ni kiongozi Bora. Inaonekana propaganda za utawala wa Magufuli zilikuchota sana, Hadi unadhani Kila mtu alichotwa kama ww.
Salaam, Shalom.
Ili pawe na Amani, huna budi kuwatisha waovu, KAZI hii ya kuhakikisha waovu hawachezei Sharubu za Serikali, Mungu alimsaidia Hayati Magufuli kuifanya kazi hiyo kwa ufasaha.
Maeneo yafuatayo, alidhibiti kwelikweli;
1. MTANDAO WA WIZI WA PESA ZA UMMA
Tumesikia Rais Samia analalamika Badala ya kuamrisha mifumo, asema kuwa umerudi mtandao wa kuiba pesa za umma, yaani pesa inatoka hazina kuja halmashauri, wanatokea watu, wanachepusha pesa hizo zinaingia katika account zao, na pesa hizo ni za mikopo tuliyokopa!
Miradi aliyeanzisha Magu, ilienda kwa kasi sababu ya ufuatiliaji wa karibu na wezi walidhibitiwa hasa.Usingeweza kukwiba pesa ya umma ukabaki salama.
2. UJAMBAZI WA KUTUMIA SILAHA.
Katika kipindi chake, majambazi walienda likizo, hilo litoshe kutupa kujua kazi kubwa aliyoifanya hasa katika kuifanya mifumo ya ulinzi na Usalama kutenda kazi Kwa viwango vya juu.
3. KUDHIBITI MTANDAO WA DAWA ZA KULEVYA
Kabla ya Magufuli kuingia madarakani, Nchi yetu ilikithiri kwa kutapakaa kwa dawa za kulevya, lakini baada ya miaka kadhaa, mateja wengi walijisalimisha katika sobber houses, sababu kuu ikiwa ni kuadimika Kwa dawa za kulevya mtaani. Hilo litoshe kutuonyesha jinsi ambavyo palifanyika kazi kubwa underground.
4. UTAKATISHAJI FEDHA
Pesa haramu, chafu zilizotokana na biashara ovu ya kuiba pesa za umma, uuzaji dawa za kulevya, biashara chafu za ukwepaji kodi, zilidhibitiwa kwa kiasi kikubwa, jambo hilo lilileta mtikisiko kwenye Uchumi kwa kuwa Kwa namna moja au ingine, pesa hizo zilisaidia kutengeneza ajira sekta binafsi.
5. MFUMO WA EFD ULIFANYA KAZI
Vituo vya mafuta kwa Mfano, vyenye kuingiza pesa nyingi, hazikuwa zikitoa EFD, na walipobanwa kutoa risiti, walitishia kugoma.
Ujasiri wa Magufuli, ulisaidia wafanyabiashara hao kurudi mezani na kukubali kutoa EFD bila masharti.
6. UFANISI KATIKA MIFUMO YA UTOAJI MIZIGO BANDARINI
Ni katika uongozi wa Hayati Magufuli, document za kutoa Mzigo bandarini zilipungua, mwanzoni palikuwa na utitiri wa karatasi na mizunguko iliyochelewesha ufaulishaji mizigo bandarini.
Scana ya ukaguzi wa vitu vinavyopita bandarini ULIFANYA KAZI utawala wa Magufuli, alipambana kweli kweli na ufanisi ulionekana.
HITIMISHO
Pamoja na mapungufu wa kibinadamu na makosa kadhaa aliyoifanya Hayati Magufuli, itoshe kusema, Mungu alimwezesha kukaa katika KITI cha maamuzi sawasawa na kuhakikisha mifumo inafanya KAZI. Magufuli hakulalamika, alichukua hatua.
OMBI: Wananchi tunaomba atokee kiongozi atakayefuta BETTING nchini, hivi sasa, vijana wa CCM+ CDM na wasio na vyama wametekwa na jinamizi hili, HAYATI Magu hakuliweza hili. Maisha hayajawahi kuwa Bahati nasibu.
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya Rais Magufuli.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo Tanzania🇹🇿.
Amen.