Hayati Magufuli kwanini ana pande zote za uongozi? Yaani ana upande mzuri sana na mbaya sana kuliko wenzake waliotangulia

Hayati Magufuli kwanini ana pande zote za uongozi? Yaani ana upande mzuri sana na mbaya sana kuliko wenzake waliotangulia

Yani hiki kikundi kidogo cha wahuni kinacholipwa pesa kuichafua legacy ya mwamba wa dunia JPM hapa JF ndiyo uamini kuwa ana mabaya? Utakuwa hauko makini na una matumizi mabaya sana na ubongo wako.

Flyovers(Ubungo)

Umeme wa bwawa,

Mahospitali,

Reli ya kisasa ya umeme (SGR)

Barabara tena za kisasa (Ubungo hadi Mbezi mwisho),

Kuifikisha TZ uchumi wa kati.

Kutumbua vyeti feki,

Kubana matumizi yasiyo na ulazima(kusafiri nnje ya nchi)

Kuboresha mikataba upya ya madini (Barrick company),

Kulinda rasilimali zisitoroshwe nnje ya nchi (Twiga, ndovu)

Kupunguza na kuzuia madawa ya kulevya,

Kuboresha bandari zote (za maji na kavu),

Kujenga viwanja vya ndege (Terminal 3),

Kununua ndege za kisasa 11,

Kudhibiti mifumuko ya bei,

Kujenga stendi za kisasa za mabasi,

Nimechoka kuandika, lakini mwenye akili na mwenye macho haambiwi "ONA".

JPM "Hata kama hamniamini mimi basi aminini kazi zangu"
Ushamba mtupu! Falsafa ya nchi hii imejikita kwenye maendeleo ya watu, siyo ya vitu. Kwa sababu ya ulimbukeni wake alinyonga maendeleo ya watu na kuelekeza rasilmali zote kwenye ujenzi ili watu wenye upeo mdogo waione na kumtukuza. Ndiyo maana shule zetu zina upungufu wa waalimu kwa asimia 40! Na je, kwa upeo wako hii ndiyo miradi ya maana sana iliyopata kutekelezwa nchi hii tangu izaliwe? Watu walipigania uhuru ili kwanza wawe watu huru katika nchi yao. Makaburu wa Afrika Kusini walijenga miundombinu mingi na mizuri kuliko hiyo lakini bado walikataliwa.
 
View attachment 2191047

Hakuna aliyewahi kupewa huu upendo toka tanzania izaliwe.

Watanzania hata ikitoe mtu kafumaniwa guest utaona wanajazana kuangalia. Nenda mahali barabara inajengwa utakuta watu wamejazana wanaangalia catapillar linavyong'oa miti. Itakuwa hilo tukio lililopewa promo na vyombo vyote vya habari?
 
Jehi Pi Hemu alikuwa kama uncle SCAR
Ninashangaa sana hili. JPM anaonekana kuwa Kiongozi mzuri sana kati ya viongozi walioitumikia Tanzania na wakati huo huo anaonekana ni Kiongozi mbaya sana kati ya wote waliopita - Hasa kwenye jambo la ukatili! Hili kwa kweli linanishangaza sana kwa sababu anatrend kuliko wote kwa pande zote hizo - ubaya na uzuri! Sijui wenzangu mnasemaje?
 
Wizi wake uko kwenye ripoti za CAG. Sasa ww unaleta porojo za mahaba niue wakati ukweli official upo!

Wewe hujui unaloliongea!! CAG aliongelea matumizi yasiyofuata utaratibu. Yaani nje na bajeti. Kama huelewi hili nitafafanua.
 
Watanzania hata ikitoe mtu kafumaniwa guest utaona wanajazana kuangalia. Nenda mahali barabara inajengwa utakuta watu wamejazana wanaangalia catapillar linavyong'oa miti. Itakuwa hilo tukio lililopewa promo na vyombo vyote vya habari?

Tutake radhi bana, mbona mimi nimewahi kuona katapila ling'oa miti nikapita tu bila kushangaa. Na tulikuwa wengi tu.
 
Wewe hujui unaloliongea!! CAG aliongelea matumizi yasiyofuata utaratibu. Yaani nje na bajeti. Kama huelewi hili nitafafanua.

Unifafanulie jambo lisilofuata utaratibu!,? Hapo utakuwa unanifafanulia au unataka kupotosha? Kama huna lako jambo unaachaje kufuata utaratibu?
 
Uzuri wake upo ndani ya mioyo ya watu wa Hali ya chini ambao ni wengi na hawaongei, ubaya wake upo mdomoni mwa wachache waliopigwa pin kisiasa na ndo midomo yao imefunguliwa wanatumia njia zote kuwaaminisha walio wengi kuwa JIWE alikuwa fisadi. Ni hayo Tu nawatakia Heri ya Pasaka
Hatar sana !!
 
Kimsingi sio JPM pekee, binadamu awaye yeyote lazima awe na pande mbili, huwezi kumfurahisha/kumchukiza kila mtu.

Hata Nyerere kuna watu wanamponda na wengine wanampa sifa, Kikwete vivyo hivyo.

Mashine tu haiwezi kuwa perfect for 100%, sembuse binadamu!?
 
Mitaani watu wachache sana wanaofuatilia mambo ya ripoti za CAG na wajomba wa Twita wengi wao wana wana ukukubali utawala wa Magufuli na kumkumbuka kama shujaa wao .
 
Ninashangaa sana hili. JPM anaonekana kuwa Kiongozi mzuri sana kati ya viongozi walioitumikia Tanzania na wakati huo huo anaonekana ni Kiongozi mbaya sana kati ya wote waliopita - Hasa kwenye jambo la ukatili! Hili kwa kweli linanishangaza sana kwa sababu anatrend kuliko wote kwa pande zote hizo - ubaya na uzuri! Sijui wenzangu mnasemaje?
Loved and hated in equal measure
 
Huwa najiuliza sana mtu kama Mandela aliwafanyia nini watu wake mpaka awe na legacy kubwa nchini kwake na kimataifa? Naona katika kazi ulizoziorodhesha sioni alijishughulisha na ipi,lakini anasifiwa kuliko kiongozi yeyote Africa.
Legacy ya Mandela haifiki ht Robo ya Legacy na Nyerere.
Legacy na Mandela sio kwa kua alifanya makubwa ktk ukombozi bali ni kwa yale aliofanyiwa na Makaburu akapata Public Sympathy.
 
Two facedness ni Sifa ya Viongozi Wanafiki, Manipulators na People users
Watu wanajitazama wao tuu kama Mungu wa Kirumi Ajulikanaye kama Janus!

Uongo wa Jiwe nani haujui hadi kumtumia Mungu wetu Bure mbele za Watu

Magufuri aliwause vijana Vibaya kama kina Ally Happy, Makonda, Sabaya na Gambo!

Janus ni Mungu wa Kirumi ambaye ana Sura mbili
IMG_9206.jpg
 
Back
Top Bottom