Sidhani kama kuna jipya ambalo hatulifafamu kwa kitakacho kuwamo kwenye hicho kitabu zaidi ya taarifa ambayo mwandishi alikuwa anaokoteza kutoka kwenye hotuba za upande mmoja wa Magufuli.
Huyo profesa atakuwa ni mhanga wa UWONGO ambao Magufuli aliutengeneza kwa miaka 5. Kwa mfano Magufuli alikuwa anasema anajenga miundombinu kwa fedha za ndani. Wakati kiukweli alikuwa anakopa kutoka mabenki ya biashara ya nje kama Credit Suisse, Stanchart na AfDB.
Huyo mtunzi hawezi kujua namna Magufuli alivyoiba uchaguzi wa S/mitaa wa 2019 na uchaguzi mkuu wa 2020 kisha kuweka wabunge mamluki ambao alitaka waje watumike kubadili katiba mwaka 2025 ili kumfanya aendelee kutawala.
Hicho kitabu kitabakia ni mkusanyiko wa karatasi tu za kumpamba hayari dikteta.