Hayati Mkapa: Makosa yangu yalisababisha mafisadi kujenga ngome ndani ya Chama cha Mapinduzi

Naelewa unacholenga kwa hayo maneno (alijitahidi sana); lakini bila ya kujuwa kujitahidi huko ndiko kumewafunza hawa waovu njia zote wanazotumia sasa hivi kutukandamiza.
Sioni jitihada za maana hapo.
Inasikitisha sana
 
Inasikitisha sana
Elewa sasa kwamba tunalo tatizo kubwa zaidi kuliko wengi wetu tunavyotambua. Huyu Samia ni kifaa/chombo tu kinachotumika sasa hivi na watu wenye nguvu zaidi duniani.

Naamini sasa kwamba wengi wetu bado hatumjui adui yetu mkubwa hasa kama taifa ni nani.

Tutapata taabu sana.

Niliposoma mada yako mwanzo kabisa hapo juu kuhusu ya Mkapa, na kueleza kwa maoni yako aliyoyakiri Mkapa, nikajuwa umejihoji vya kutosha kuhusu u-CCM wako. Tatizo tu nililobaki nalo kwako ni kwa kudhani Magufuli alijitahidi kubadili hali hiyo mbovu aliyotuweka Mkapa.
Nami ningekuwa naimba sifa za Magufuli kama wewe kwa baadhi ya hayo yaliyokuvutia wewe, lakini nilishindwa tokea mwanzo kwa namna alivyoyasimamia na hata mengine nje kabisa mabovu sana nje ya hayo ambayo tungependa sote kumsifia..

Hakuna sababu ya kuendelea kulialia na yaliyopita, inabidi tu sasa tuungane pamoja kubadili hali hii mbovu inayolikabili taifa letu sasa hivi kwa kuunga mkono njia zitakazosaidia kuleta mabadiliko, hata kama ni kutoka kwa watu ambao tunatofauti kubwa na wao, ili mradi hawaungani na waovu hawa.
 
Umeishia kulalamika tu
 
Umeishia kulalamika tu
Sina uwezo wa kwenda kuwafufua Magufuli na Mkapa, sasa ulitaka nifanye nini kuliko kukueleza ukweli ambao wewe unasema ni "kulalamika".

Unapokuwa shabiki wa kiongozi na kujiondoa kabisa akili za kudadisi na kujuwa mabaya aliyoyafanya hakukufanyi kuwa mfuasi mzuri wa kiongozi huyo.
Tunakubali mazuri aliyojaribu kuyafanya Maguguli kwa taifa hili, pamoja na kwamba njia zake zilikuwa za hovyo; lakini hapo hapo hatuwezi kamwe kunyamazia uovu mwingi na tabia zake mbovu kabisa alizoonyesha kuwa nazo ambazo hazikubaliki
 
Back
Top Bottom