Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 8,105
- 20,307
Hayati Benjamin Mkapa Katika kitabu chake "My Life, My Purpose" (2019) Ameeleza maeneo aliyofeli kama kiongozi
1. Kufeli Kukubwa Kuliko kote: Ubinafsishaji (Privatization) Anasema "Nilifanya Haraka Sana"
"Tuliamini soko huria litatatua kila kitu. Tuliuza viwanda 400 kwa bei ya hasara. Tuliwaamini wawekezaji wa nje kuliko Watanzania wenyewe"
Anataja:
2. Kufeli kuzuia Rushwa ameandika "Nilichelewa Kuipinga"
"Nilidhani nikijenga uchumi, rushwa itapungua yenyewe. Nilikosea. Rushwa ndio iliyokula uchumi wangu"
Anataja kesi 3 zinazomuumiza:
3. Kufeli Siasa "Niliwabeza Mwinyi na Nyerere"
Katika ukurasa 203 anasema:
"Nyerere aliniambia 1995 - 'Usifanye haraka kuua chama. Chama ndio nyumba'. Mimi nilitaka kuwa Rais wa kitaalam, sio wa chama. Nikaacha CCM iende yenyewe. Matokeo yake mafisadi wakajenga ngome ndani ya chama"

- Kiwanda cha Viatu Bora, General Tyre, Nyanza Glass* - viliuzwa na kufungwa, wafanyakazi 80,000 walipoteza kazi
- Mabenki: NBC na CRDB ziliuzwa kwa bei ya chini sana. Anasema "Tuliuza bila kujua thamani yake"
- Akakiri Tulipaswa kubinafsisha taratibu na kuwa na masharti ya kuajiri Watanzania na kuhamisha teknolojia. Hatukufanya hivyo"
2. Kufeli kuzuia Rushwa ameandika "Nilichelewa Kuipinga"
"Nilidhani nikijenga uchumi, rushwa itapungua yenyewe. Nilikosea. Rushwa ndio iliyokula uchumi wangu"
Anataja kesi 3 zinazomuumiza:
- Kashfa ya Radar (2001): Kununua rada ya kijeshi ya Uingereza kwa $40M wakati bei yake halisi $12M. BAE Systems ilikiri Mahakama ya London 2010 ilitoa rushwa. Mkapa anasema "Wizara ya Ulinzi ilinidanganya kuhusu bei"
- Kashfa ya Buzwagi na Geita Gold Mine:Mikataba ya madini 1998-1999 aliipa kampuni za kigeni bila royalties za kutosha. Anasema "Tulikuwa tunaogopa wawekezaji watakimbia, tukawapa kila kitu"
- Kashfa ya Twin Towers na IPTL: Anasema "Niliwaamini mawaziri wangu sana, baadaye nikagundua walikuwa na maslahi ndani"