Sir Andy Chande na BWM walikua "brothers" kwenye ile taasisi ya siri.He had an ego, and didnt want to hear any second opinion. He was an elitist.
Nakumbuka Nyerere alisema mtabinafsisha mpaka magereza.
Unategemea nini kama mwenyekiti wa ubinafishaji alikuwa Sir Andy Chande?
Majanga matupu
Huu ndio ukweli, tuache kuwarembaremba hawa ndio watu waliotufikisha hapa.Hawa ndio waasisi wa 10%.Mkapa ni architect wa mambo mengi sana ya hovyo na alifanya akijua baadae atakuja kuomba msamaha na hii tabia tunayo watanzania wengi
Huu ndio ukweli, tuache kuwarembaremba hawa ndio watu waliotufikisha hapa.Hawa ndio waasisi wa 10%.
Mzee mchonga naye alikuwa hajui umuhimu wa katiba mpya.26 good years hakuona kitu.
Kama hakuona kitu basi pale juu hakuhutaji mtu extraordinary hata tukiamua kuweka sanamu litatuongoza tu.Waseme ukweli kuwa mfumo ulikuwa unafaida kwao at their time.Hizi nyingine ni soga tu.
Hawa wazee waache kutuenjoy.We are better than this!!!!
Uko sahihi 100%Mkapa ni architect wa mambo mengi sana ya hovyo na alifanya akijua baadae atakuja kuomba msamaha na hii tabia tunayo watanzania wengi
Ni mnafki sana yule mzee imagine kwenye chaguzi za mwaka 2000 na mwaka 2005 mkapa alikuwa kinara wa kuiba kura na wakati wa 2015 aliwaita wapinzani malofaUko sahihi 100%
Yote ambayo Mkapa aliyaita makosa yake, akiwa madarakani aliyanya kwa mkusudi.
Mkapa aliposema alitikiswa na kashfa ya radar,na kwamba eti alidanganywa na wizara ya ulinzi, wengi tulijua anadanganya kwa sababu waziri wa UK wa masuala ya Afrika Bi Lyinda Chalker alifanya safari zaidi ya mara 3 kuieleza serikali ya Tanzania kwamba inapigwa katika ununuzi huo kwa vile bei iliyoyotajwa imeongezwa kwa shinikizo toka kwa watendaji wapigaji wa serikali ya Tanzania,..lakini Mkpa akaweka pamba masikioni.
Mkapa alijua wakiuza viwanda kwa bei ya kutupa itawapa fursa wao wakubwa serikalini kupata commission ya pembeni toka kwa wanunuzi,na wao watendaji pia kugawana baadhi ya viwanda kama yeye Mkapa alivyojigawia Kiwira coal mine kwa bei ya bure...,ambao ilikuja kurudishwa serikalini baadaye.
Mkapa ndiye mwanzilishi wa kuchota fedha katika acc ya Escrow(kupitia kashfa ya Kagoda) ili kuisaidia ccm katika uchaguzi...kitendo ambacho kilirudiwa tena na Kikwete....
The list is endless
Tusaidie softcopy MkuuHayati Benjamin Mkapa Katika kitabu chake "My Life, My Purpose" (2019) Ameeleza maeneo aliyofeli kama kiongozi
1. Kufeli Kukubwa Kuliko kote: Ubinafsishaji (Privatization) Anasema "Nilifanya Haraka Sana"
"Tuliamini soko huria litatatua kila kitu. Tuliuza viwanda 400 kwa bei ya hasara. Tuliwaamini wawekezaji wa nje kuliko Watanzania wenyewe"
Anataja:
- Kiwanda cha Viatu Bora, General Tyre, Nyanza Glass* - viliuzwa na kufungwa, wafanyakazi 80,000 walipoteza kazi
- Mabenki: NBC na CRDB ziliuzwa kwa bei ya chini sana. Anasema "Tuliuza bila kujua thamani yake"
- Akakiri Tulipaswa kubinafsisha taratibu na kuwa na masharti ya kuajiri Watanzania na kuhamisha teknolojia. Hatukufanya hivyo"
Hii ndio sababu mpaka leo watu wanamlaumu kwa umasikini wa viwanda.
2. Kufeli kuzuia Rushwa ameandika "Nilichelewa Kuipiga"
"Nilidhani nikijenga uchumi, rushwa itapungua yenyewe. Nilikosea. Rushwa ndio iliyokula uchumi wangu"
Anataja kesi 3 zinazomuumiza:
- Kashfa ya Radar (2001):*Kununua rada ya kijeshi ya Uingereza kwa $40M wakati bei yake halisi $12M. BAE Systems ilikiri Mahakama ya London 2010 ilitoa rushwa. Mkapa anasema "Wizara ya Ulinzi ilinidanganya kuhusu bei"
- Kashfa ya Buzwagi na Geita Gold Mine:Mikataba ya madini 1998-1999 aliipa kampuni za kigeni bila royalties za kutosha. Anasema "Tulikuwa tunaogopa wawekezaji watakimbia, tukawapa kila kitu"
- Kashfa ya Twin Towers na IPTL:*Anasema "Niliwaamini mawaziri wangu sana, baadaye nikagundua walikuwa na maslahi ndani"
Anasema alianzisha TAKUKURU na Mahakama ya Rushwa 2001, lakini ilikuwa "too little, too late"
3. Kufeli Siasa "Nilimbeza Mwinyi na Nyerere"*
Katika ukurasa 203 anasema:
"Nyerere aliniambia 1995 -'Usifanye haraka kumuua chama. Chama ndio nyumba'. Mimi nilitaka kuwa Rais wa kitaalam, sio wa chama. Nikaacha CCM iende yenyewe. Matokeo yake mafisadi wakajenga ngome ndani ya chama"
Ndugu yangu wahuni ni wahuni tu....hawakwepeki hata uwe makini vipi.....ndo mana unakua na mke ndani unamwamini kwa asilimia zote lakini boda wanamla na huwezi kuja kujua..."Alikuwa kazungukwa na wahuni"; unadhani nini kilipelekea hilo? Alikosa umakini? Uwezo wa kiuongozi? Au?
Hao wahuni leo bado wapo? Kwanini?
Kigezo hapo kilichotumika ni tafakari tu, ni mali zipi alizofuja? Ambazo zinaonekana tangu alipoondoka madarakani hadi leo? Mana kwa nchi yetu siri hakuna mtu akiacha mali watu wanajua tu hizi mali ni za fulani....sasa mimi katika kuzurura kwangu sijawahi kukuta sehemu wanasema hii ni mali ya Mkapa....Sijui umetumia kigezo kipi kudhani Mkapa hakujilimbikizia mali, ikiwa ufisadi ulianzia awamu yake na wewe unakiri hivyo.
Mimi naona tofauti ya Mkapa na hawa mafisadi wa siku hizi ni kelele zao tu, wakati Mkapa alikuwa akila kimya kimya, hawa wa siku hizi wanakula na kipofu kwa kumshika mkono!.
Thinking yako nyepesi sana, unamsubiri kiongozi ataje mali zake ili tuanze kumuuliza amezitoa wapi ikiwa kipato chake hakimruhusu kuzimiliki!Kigezo hapo kilichotumika ni tafakari tu, ni mali zipi alizofuja? Ambazo zinaonekana tangu alipoondoka madarakani hadi leo? Mana kwa nchi yetu siri hakuna mtu akiacha mali watu wanajua tu hizi mali ni za fulani....sasa mimi katika kuzurura kwangu sijawahi kukuta sehemu wanasema hii ni mali ya Mkapa....
Kijana pambana unowe ubongo wako kwa maarifa zaidi.Kigezo hapo kilichotumika ni tafakari tu, ni mali zipi alizofuja? Ambazo zinaonekana tangu alipoondoka madarakani hadi leo? Mana kwa nchi yetu siri hakuna mtu akiacha mali watu wanajua tu hizi mali ni za fulani....sasa mimi katika kuzurura kwangu sijawahi kukuta sehemu wanasema hii ni mali ya Mkapa....
Mimi sisemei mali wanazozitaja kwenye form zao uchwara hizo, naongelea habari za Mtaa....mfano wewe unayeamini alikua mfuja mali, nitajie mali hata 3 tu kubwa zinazomilikiwa na familia yake ambazo unahisi zilitokana na ufujaji.....tuache porojo tuongee uhalisia..Thinking yako nyepesi sana, unamsubiri kiongozi ataje mali zake ili tuanze kumuuliza amezitoa wapi ikiwa kipato chake hakimruhusu kuzimiliki!
Hizo fomu wanazojaza za maadili huwa wanadanganya mali walizonazo.
Ukishajua 10% inahusika kwenye mikataba, hiyo ni rushwa, usisubiri kuletewa majibu ukiwa nyumbani.
Jiongeze.
Unaishi mapori ya wapi ?Lakini Mkapa hakujilimbikizia mali hovyo, sema tu alikua kazungukwa na wahuni na aliwaamini bila kuwajua vizuri......madhambi ya awamu ya 5 na 6 yanafanya hata Mkapa aonekane malaika
Huo mgodi ndio ule wa Kiwira!Unaishi mapori ya wapi ?
Mgodi wa makaa ya mawe
Magorofa ya msajili ya Ilala
Na vingine vingi tu
Tatizo ni moja."Nyerere aliniambia 1995 -'Usifanye haraka kumuua chama. Chama ndio nyumba'. Mimi nilitaka kuwa Rais wa kitaalam, sio wa chama. Nikaacha CCM iende yenyewe. Matokeo yake mafisadi wakajenga ngome ndani ya chama"
Hata hivyo ni vigumu sana kumwamini Mkapa.Hebu aseme ukweli, kuwa alitishwa na ngome hiyo, ndipo akaamua afanye yanayomuhusu. Ubinafsi.
Ndio ndio.Hata hivyo ni vigumu sana kumwamini Mkapa.
Kama haya yote aliyoeleza kweli alikuwa ameyagundua, asingemwachia uongozi huyo aliyepishana naye; kwa sababu huyo ndiyo ilikuwa tayari inajulikana ni kiongozi wa ngome hiyo.
Kiufupi, Mkapa mwenyewe anajidhalilisha kabisa kukosa uongozi imara.
Hakuweka maslahi ya nchi mbele.