Hayati Mkapa: Makosa yangu yalisababisha mafisadi kujenga ngome ndani ya Chama cha Mapinduzi

Hayati Mkapa: Makosa yangu yalisababisha mafisadi kujenga ngome ndani ya Chama cha Mapinduzi

Ni mnafki sana yule mzee imagine kwenye chaguzi za mwaka 2000 na mwaka 2005 mkapa alikuwa kinara wa kuiba kura na wakati wa 2015 aliwaita wapinzani malofa

Ila kwenye kitabu chake akaandika anatamani siku Tanzania ifanye uchaguzi huru na haki unajua mambo mengine ni ya ajabu sana ulivyokuwa madarakani hukuonyesha mfano wa kuheshimu sanduku la kura umeondoka madarakani ndo unatamani mambo ya ajabu sana
Una soft copy yake ya hiki kitabu mkuu?
 
WANASEMA HAYA YALIKUWA MAZURI YAKE PIA.


Huyu Ndiyo Hayati Benjamin Mkapa wa Tanzania!

Denis Mpagaze
___________________

1. Wazazi wake walitamani awe Padre wa Jimbo akawa Rais wa nchi. Sisi tunapanga na Mungu anapangua.

2. Aliingia madarakani nchi ikiwa imedumaa kiuchumi, akatawala kwa falsafa ya “Huwezi kupata maendeleo bila kubadili fikra!”

3. Akasisitiza watu wafikiri. Waliozembea kufikiri aliishia kuwatukana kwamba ni wavivu wa kufikiri.

4. Mkapa alifundishwa na Mwl. Nyerere pale Pugu. Baada ya Pugu Nyerere alienda kutafuta uhuru wa nchi, Mkapa akaenda kutafuta uhuru wa fikra huko Makerere.

5. Walikuja kukutana tena na Nyerere kila mtu amepata alichokwenda kutafuta, wakapiga kazi pamoja kuijenga nchi.

6. Nyerere Rais, Ben Katibu Tawala Dodoma, vyeo vikaanza kumgombania, mara balozi, mara mbunge, mara waziri, mara Rais!

7. Mkapa akiwa Rais aliamini ili Tanzania iendelee ilihitaji taasisi imara na siyo watu imara. Akaanza kujenga taasisi hizo bhana.

8. Palipo na umasikini alijenga TASAF maskini wakaanza kula na kushiba.

9. Palipokosa uhakika wa matibabu alianzisha bima ya afya watu wakawa na uhakika na afya zao.

10. Palipojaa rushwa alianzisha TAKURU kuitokomeza rushwa kwa kiasi chake.

11. Waliokosa ada za vyuo vikuuu, alianzisha Bodi ya Mikopo watoto wa maskini wakatinga vyuo vikuu kwa mbwembwe na ushamba ndani yake.

12. Palipo na upotevu wa mapato, alianzisha TRA, mapato yakaongezeka karibu mara tatu kutoka dola 612,587 hadi dola 1,796,862 kwa mwezi.

13. Ili kuzipa hadhi rasilimali za wanyonge alianzisha MKURABITA kurasimisha ardhi yao ikapata maana.

14. Ili kuvutia uwekezaji alianzisha TIC, wageni wakachangamkia fursa wazawa wakasinzia.

15. Katika kuimarisha usalama wa nchi alianzisha TISS nchi ikawa na usalama wa uhakika.

16. Mkapa alishirikisha taasisi za dini kuchochea elimu nchini.

17. Alitoa majengo ya Sekondari ya Mazengo kwa Waanglikana wakaanzisha St. Joseph University Dodoma.

18. Akatoa majengo ya Sekondari ya Magamba Rushoto wakapewa Walutheri wakaanzisha Sebastian Kolowa Memorial University

19. Alitoa majengo ya Benki Iringa kwa wakatoliki wakafungua Ruaha University.

20. Alitoa majengo ya TANESCO Morogoro wakapewa waisilamu wakaanzisha Chuo Kikuu cha Kiislamu.

21. Elimu ya chuo kikuu Tanzania ikawa kitu cha kawaida, vyuo vikuu vilizagaa kila kona ya nchi.

23. Ili kuwapa ahueni maskini, Mkapa alifuta kodi ya kichwa. Zamani kuna wazee walishinda porini wamejificha hawana kodi wasidakwe na mgambo.

24. Mkapa alifuta hadi kodi ya baiskeli na mifugo ili kumpa ahueni maskini, halafu alidhibiti mfumko wa bei hadi maskini wakaanza kunywa chai.

25. Katika utawala wake kilo ya sukari tuliinunua kwa shilingi mia tano kwa muda mrefu! Haikupanda.

26. Mkapa alipenda kusema sisi ni maskini mfukoni lakini matajiri kichwani. Hii kali!

27. Hatuwezi kuweka fedha mifukoni mwenu ila tutandaa mazingira ya kupata pesa alisisitiza.

28. Mkapa hakupenda kuabudiwa. Alikataa kuitwa Mtukufu Rais kama walivyoitwa Mtukufu Al-Hassan Mwinyi na Mtukufu Daniel Arap Moi

30. Alikataa picha yake kutumika kwenye sarafu, alikataa kuitwa daktari pamoja na kutunukiwa PhD kibao za heshima.

31. Hata barabara ya kwenda kwao imekuja kujengwa na Rais Magufuli, yeye aligoma kujenga.

32. Hata huu uwanja wa mpira umekuja kuitwa kwa jina lake baada ya kuondoka duniani. Unaitwa Mkapa Stadium. Halafu yeye ndo aliujenga.

33. Ni uwanja wa kisasa kweli kweli hadi Brazil wakaja kuweka kambi tukawaona akina Ricardo Kaka, Robinho Do Santos na Ruis Fabiano live.

34. Mkapa hakupenda kuonyeshwa kwenye TV mara kwa mara kama Moboutu Seseko wa Zaire ndo maana aliwashauri waonyeshe mambo ya maendeleo na changamoto za vijijini.

35. Hata aliposaidia watu hakuhitaji kuitangazia dunia kama mnavyofanya nyie.

36. Mkapa alikuwa msomaji mzuri wa vitabu ndo maana alijua mengi!

37. Kutosoma vitabu ni kujiongezea janga la umaskini alipenda kusema Mkapa.

38. Mbele ya Mkapa kama husomi na kufanya tafiti alikuona takataka.

39. Hotuba za Mkapa zilikonga nyoyo za wengi kwa sababu ya utamaduni wake wa kusoma sana.

40. Enzi zake nchi ilikaa kimya kumsikiliza mwanaume akihutunia kupitia kwenye TV.

41. Halafu alikuwa na majibu ya kuudhi balaa hasa ukimuuliza swali lilitofautiana na fikra zake.

42. Mkapa atakumbukwa kama Rais aliyekuza uchumi, kujenga taasisi imara na kufanya makosa kwenye ubinafsishaji na uuzaji wa nyumba za serikali.

43. Ila alitubu miezi nane kabla ya kufa kwake sababu kukosea ni ubinadamu kukiri makosa ni uungwana.

44. Mkapa ndo alikuza uhuru wa habari. Hakula chakula cha jioni kabla ya kusikiliza taarifa ya habari.

45. Alisoma sana magazeti hadi barua za wasomaji na wakati mwingine aliwaagiza wasaidizi kuwatafuta waandishi wa barua zilizomgusa.

46. Waandishi wengi wa Tanzania aliwaita wavivu wa kufikiri kutokana na aina ya habari walizoandika na maswali mepesi waliyomuuliza.

47. Mkapa amewahi kutangaza RTD na kuhariri magazeti ya chama pamoja na Daily News, alitumia jina la bandia kuwakosoa viongozi kupitia gazeti.

48. Alijiita "Mwana wa Matonya! Lakini pia ndo mwanzilishi wa SHIHATA, yaani Idara ya Habari Maelezo ya leo.

49. Katika utawala wake Mkapa alikutana na majanga mazito yakamuimarisha badala ya kumdhofisha ndo maana hakuikimbia Ikulu.

50. Mei 21, 1996, mwaka mmoja tu baada ya kuingia madarakani likatokea balaa la kuzama kwa meli ya MV Bukoba.

51. Mwaka uliofuta yaani 1997 tukapigwa na mafuriko ya el nino yakavuruga nchi.

52. Februari 13, 1998 sekeseke la mauaji ya mwembe chai likatia doa utawala wake.

53. Oktoba 14, 1999 baba wa Taifa akaondoka duniani katika utawala wake.

54. Januari 27, 2001 mauaji ya Pemba yakautia doa tena utawala wake

55. Julai 4, 2001 makamu wa Rais Dkt. Omar Ali Juma akaaga dunia!

56. Lakini pia Mkapa anasema alikuwa na wasiwasi pale Rais wa Zanzibar Salmin Amour alipotaka kubadilisha sheria na kutawala kipindi cha tatu.

57. Mkapa aliamini uwepo wa vyama vingi vya siasa unadhoofisha demokrasia ndo maana hakuvikubali kabisa vya vya siasa.

58. Aliwahi kusema ushauri unatokana na nguvu ya hoja tutaupokea lakini ushauri unatokana hoja ya nguvu tutaikataa.

59. Alisema vyama vinavyosema vinajiandaa kuikomboa Tanzania ni wapumbafu, malofa, Tanzania iliishakombolewa na CCM.

60. Mkapa alikuwa mume wa mke mmoja na watoto wawili Nicodemus na Steve.

61. Mkapa alioa mwaka 1966 akiwa kijana wa miaka 28. Alimuoa Anna Joseph Shauri Maro wakati huo mtumishi wa wizara ya habari, aliyesomea Uingereza.

62. Ndoa yao ilifungwa ukweni Moshi katika kanisa katoliki. Mkapa alibaki kuwa mkatoliki kwa maisha yake yote na Anna ameendelea kuwa mlutheri hata sasa kwa sababu walipendana kwa dhati.

63. Wazo la Mkapa kugombea Urais lilianzia kwa Jenerali Ulimwengu na vijana wenzake waliokuwa bungeni enzi hizo, wazo likaenda kwa Mzee Warioba na kufika kwa Mkapa

64. Mkapa akalipeleka kwa wife, theni kwa jamaa zake na mwisho kwa Mzee Nyerere.

65. Nyerere alishangaa lakini akakubali kumuunga mkono ingawa alikuwa na mgombea wake, Salim Mohammed Salim.

66. Wengi walipigwa butwaa siku Mkapa alipochukua fomu. Jamaa hakuwa na umaarufu kwa sababu aliishi sana nje.

67. Lakini pia hakuwa muongeaji sana hadi Augustine Mrema akamwita "Bubu".

68. Kuna magazeti yaliandika kwamba Ken Mkapa wa Yanga alijulikana zaidi Tanzania kuliko Mkapa.

69. Kwenye kampeni za Mkapa, Jenerali Ulimwengu alikuwemo, sema walikuja kuzinguana baadaye!

70. Nimalizie kwa kusema, Mkapa alikuwa mtu wa matani na vichekesho pia.

71. Hata ule upara alisema ulitokana na kubeba vyombo shuleni. Shuleni walijipikia.

72. Anasema alipokuwa chuoni watoto wa kike walimzimia kishenzi kwa sababu ya kujeng hoja zilizosisimua.

73. The Big Ben amelala lakini fikra zake ziko macho. Kwa uhondo zaidi, Soma kitabu chake cha My Life My Purpose
 
Lakini Mkapa hakujilimbikizia mali hovyo, sema tu alikua kazungukwa na wahuni na aliwaamini bila kuwajua vizuri......madhambi ya awamu ya 5 na 6 yanafanya hata Mkapa aonekane malaika
Mkapa alijimilikisha mgodi huko mbeya,alipouza NBC akakopeshwa na aliowauzia 100m,kule nzega mgodi wa lusu alikua akienda kila mwaka na kupewa kiasi cha dhahabu kama zawadi tu,alianza na koleo la dhahabu ikafuatiwa na tofali la kilo 16 la dhahabu,walipopiga kelele ikawa zawadi hazitajwi
Hakujilimbikizia mali kivipi!?
 
Kuna kitu muhimu mno hajakigusia mostly kwa makusudi - KATIBA BORA ambayo ingeruhusu demokrasia, uwazi na uwajibikaji wa kweli ( sio wa kinafiki).

Mojawapo ya matatizo ambayo yamekuwepo since Nyerere ni wachache kuhodhi madaraka, kutenda wapendavyo, kuharibu bila uwajibikaji kisha baadaye "kujisikitisha"! Inasaidia nini?

Bila KATIBA BORA itakayosimika mifumo bora ya kiuongozi haya MASIKITIKO ya viongozi katika ngazi mbalimbali yataendelea kuwepo baada ya kumaliza vipindi vyao.

KATIBA BORA iwepo ili iwapunguzie MASIKITIKO unfortunately ndio hivyo tena hawataki! Ridiculous!
Demokrasia haina msaada wowote kwenye maendeleo
 
Ila Ugisadi ulishamili kipindi cha Kikwete. Kuanzia 2010 wafanyakazi wa serikali walianza kuwa na Utajiri wa kutisha.
Kikwete aliongeza moshahara ya watumishi kwa zaidi ya 80% kwa mara moja,kisha kila mwaka kukawa na nyongeza, familia za watumishi tuliona mabadiliko ya kipati
Ufisadi ulikua kawaida na lazima kipindi cha mkapa, yaani kupiga dili ilikua kama faradhi
 
M
Huu ndio ukweli, tuache kuwarembaremba hawa ndio watu waliotufikisha hapa.Hawa ndio waasisi wa 10%.

Mzee mchonga naye alikuwa hajui umuhimu wa katiba mpya.26 good years hakuona kitu.

Na kama hakuona kitu basi pale juu hakuhitaji mtu extraordinary hata tukiamua kuweka sanamu litatuongoza tu.Waseme ukweli kuwa mfumo ulikuwa unafaida kwao at their time.Hizi nyingine ni soga tu.

Hawa wazee waache kutuenjoy.We are better than this!!!!
Malecela alipigwa 10% ya mapajero na mamvi,10% haikuanza kwa mkapa
 
Sema awamu ya Nne 🙄 ! Maana Kiongozi wake ndiye aliyekuwa waziri wa madini kipindi cha Mkapa 😳🙄 !
Kikwete alikuwa Waziri wa mambo ya nje tangu siku ya kwanza ya utawala wa Mkapa mpaka siku ya mwisho ya utawala wake.
Waziri wa madini na Nishati serikali ya awamu ya tatu alikuwa Edgar Maokola Majogo.
 
Kikwete alikuwa Waziri wa mambo ya nje tangu siku ya kwanza ya utawala wa Mkapa mpaka siku ya mwisho ya utawala wake.
Waziri wa madini na Nishati serikali ya awamu ya tatu alikuwa Edgar Maokola Majogo.
Anata kumrundikia kikwete dhambi za madini, waziri hana lolote kwenye maamuzi ya magnitude hiyo
 
Hayati Benjamin Mkapa Katika kitabu chake "My Life, My Purpose" (2019) Ameeleza maeneo aliyofeli kama kiongozi

1. Kufeli Kukubwa Kuliko kote: Ubinafsishaji (Privatization) Anasema "Nilifanya Haraka Sana"

"Tuliamini soko huria litatatua kila kitu. Tuliuza viwanda 400 kwa bei ya hasara. Tuliwaamini wawekezaji wa nje kuliko Watanzania wenyewe"

Anataja:

  • Kiwanda cha Viatu Bora, General Tyre, Nyanza Glass* - viliuzwa na kufungwa, wafanyakazi 80,000 walipoteza kazi
  • Mabenki: NBC na CRDB ziliuzwa kwa bei ya chini sana. Anasema "Tuliuza bila kujua thamani yake"
  • Akakiri Tulipaswa kubinafsisha taratibu na kuwa na masharti ya kuajiri Watanzania na kuhamisha teknolojia. Hatukufanya hivyo"

Hii ndio sababu mpaka leo watu wanamlaumu kwa umasikini wa viwanda.

2. Kufeli kuzuia Rushwa ameandika "Nilichelewa Kuipiga"

"Nilidhani nikijenga uchumi, rushwa itapungua yenyewe. Nilikosea. Rushwa ndio iliyokula uchumi wangu"

Anataja kesi 3 zinazomuumiza:

  • Kashfa ya Radar (2001):*Kununua rada ya kijeshi ya Uingereza kwa $40M wakati bei yake halisi $12M. BAE Systems ilikiri Mahakama ya London 2010 ilitoa rushwa. Mkapa anasema "Wizara ya Ulinzi ilinidanganya kuhusu bei"
  • Kashfa ya Buzwagi na Geita Gold Mine:Mikataba ya madini 1998-1999 aliipa kampuni za kigeni bila royalties za kutosha. Anasema "Tulikuwa tunaogopa wawekezaji watakimbia, tukawapa kila kitu"
  • Kashfa ya Twin Towers na IPTL:*Anasema "Niliwaamini mawaziri wangu sana, baadaye nikagundua walikuwa na maslahi ndani"

Anasema alianzisha TAKUKURU na Mahakama ya Rushwa 2001, lakini ilikuwa "too little, too late"

3. Kufeli Siasa "Nilimbeza Mwinyi na Nyerere"*

Katika ukurasa 203 anasema:

"Nyerere aliniambia 1995 -'Usifanye haraka kumuua chama. Chama ndio nyumba'. Mimi nilitaka kuwa Rais wa kitaalam, sio wa chama. Nikaacha CCM iende yenyewe. Matokeo yake mafisadi wakajenga ngome ndani ya chama"
Nilipo kuwa Mdogo Niliwaza

Kuna mikataba mingine ili tuivunje lazima itumike nguvu ya kijeshi Moja ya iyo mikataba ndio hii mikataba ya kunyonywa Kwa miaka 99🤔
 
Sijui umetumia kigezo kipi kudhani Mkapa hakujilimbikizia mali, ikiwa ufisadi ulianzia awamu yake na wewe unakiri hivyo.

Mimi naona tofauti ya Mkapa na hawa mafisadi wa siku hizi ni kelele zao tu, wakati Mkapa alikuwa akila kimya kimya, hawa wa siku hizi wanakula na kipofu kwa kumshika mkono!.
Mkuu una hoja.
Mwaka mmoja baada ya utawala wa Mkapa kuanza kazi 1996, Mawaziri wake Profesa Simon Mbilinyi (Fedha)
Dr Juma Ngasongwa (Viwanda na Biashara)

Kilontsi Mpologomi (Naibu Waziri)
Waliingia kwenye kashfa nzito ya kula rushwa ya sh milion 900 ili kutoa misamaha ya kodi kwa wafanyabiashara wa Viwanda vya mafuta ya kula na Viwanda vya kusindika minofu ya samaki.

Kwenye mgao wa rushwa hiyo imeonekana mwenyekiti wa CCM (hakutajwa jina) ametengewa mgao wake sh milioni 500.

Kamati ya bunge chini ya aliyekuwa mbunge wa Ilala marehemu Iddi Simba imethibitisha kashfa hii. Mawaziri kadhaa wametimuliwa kupitia kashfa hiyo iliyopelekwa bungeni na mbunge Kwela marehemu Chrisant Majiyatanga Mzindakaya.
 
Miaka ile ya ubinafsishaji kulikuwa na tuhuma kuwa Mkapa alikuwa anamtumia aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Uma, marehemu George Mbowe, kufanya mapatano hatimaye kuuza kiwanda kwa bei poa.

Kwa mfano Kiwanda cha viatu Bora kiliuzwa kwa sh milion 700 kinyume kabisa na raslimali zake nyingi ilizokuwa nazo.

Iliituumiza zaidi kiwanda cha Sukari Kilombero kiliuzwa kwa mwekezaji kutoka Afrika Kusini kikiwa na shehena ya sukari iliyojaa kwenye mabohari yake.

Wakati ule Kulikuwa na madai kutoka baadhi ya vyombo vya habari kuwa Balozi furani wa Tanzania katika nchi furani barani Afrika, alihusika kutafuta wawekezaji ili wauze Viwanda na mashirika yenye biashara kubwa.

Hivyo waliletwa wawekezaji kutoka Afrika Kusini kununua TBL, Kilombero Sugar, NBC, Twiga Cement na kampuni ya kuchimba madini ya TANZANITE iliyojulikana kwa jina Tanzania one.
Na Balozi wetu huyo akapewa hisa kwenye kampuni hizo.

Baadaye ilisemwa Balozi anamuwakilsha Mkapa kwenye asasi hizo za kiuchumi.
Madai hayo hayakukanushwa, ingawa yaliongeza chuki kutoka serikali ya Mkapa na aliyekuwa Mwenyekiti na mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Habari Corporation , ndugu Jenerali Ulimwengu.

Ikumbukwe gazeti la RAI lilihusika vilivyo kuchambua madudu kwenye ubinafsishaji chini Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Uma (PSRC).
Hilo ni miongoni mwa mambo yaliyopelekea kuvuliwa uraia wa Ulimwengu.
 
Demokrasia haina msaada wowote kwenye maendeleo
Mkuu Demokrasia ina msaada.
Demokrasia imetupa uhuru kidogo wa kukosoa utendaji wa viongozi wetu angalau kwa kujificha namna hii.
Wakati wa ukilitimba wa chama kimoja hakukuwa na uhuru hata huu mdogo ambao wananchi wengeweza kuutumia kukosoa mapungufu ndani ya serikali yao.
Wingi wa vyombo vya habari umeletwa na mabadiliko ya kisiasa.
 
Kijana pambana unowe ubongo wako kwa maarifa zaidi.

Dunia ya leo unataka kila mtu afungue duka,kiwanda au ajenge apartments.

Wenzako wanawatumia mabroker kama CHIVAYO kwenda kutunza pesa nje kwenye TRUSTS NA OFFSHORE ACCOUNTS!!!

UNAJUA MAMBO YA OFFSHORE ACCOUNTS AU NAPOTEZA MUDA HAPA??
Dubenga, uswizi, UK, singapore, panama, british virgin islands, hong kong, sheli sheli huko.....sio poa kabisaaa, rig G anasema bwana bigi kasepa na mzigo mnene wa kasongoo apoo😥
 
Dubenga, uswizi, UK, singapore, panama, british virgin islands, hong kong, sheli sheli huko.....sio poa kabisaaa, rig G anasema bwana bigi kasepa na mzigo mnene wa kasongoo apoo😥
Hawa masokwe wanaoongoza hizi nchi za Sub-Sahara ni washenzi wakubwa yaani subhuman specie kabisa
 
Back
Top Bottom