Tetesi: Hayawi Hayawi, Diamond kumposa Zuchu Ijumaa!

Mbona unachosema ni tofauti na tulichokuwa tunajadili Mkuu?
 
Can somebody check on Diamond? Is he alright? Team kataa ndoa tuna wasiwasi inawezekana mwenzetu kashikiwa bunduki
Zuchu amemnunia, ndio anabembelezwa kwa ndoa.
 
Mama wa za ndani,ngojea tusubiri.
 
Hapa unamaanisha nini Mkuu?
 
Asante mdomo wa farasi
 
Sijui kwanini, kama Diamond angekuwa kijana wangu, ningehakikisha anamuoa Tanasha.
Kiukweli wengi tunampenda Tanasha baada ya Wema, ila ndio hivyo tena.
 
...na hiyo ndoa yao itavunjika kabla ya Ramadhan ya 2026. Kama kawaida ya ndoa za wasanii.
 
Umelewa?
 
Sijui kwanini Diamond hajawahi kuwa proud na Zuchu Kama ilivyokuwa kwa mahusiano yake mengine.

Hajawahi hata kukiri hadharani kutoka naye kimapenzi! Huwa najiuliza sana…

Hilo bado sijafahamu kama kutakuwa na prenup au lah!
Ndio maana naiona aidha ni drama ama ni biashara japo hadi sasa ukiangalia kwa ukaribu. Couple ya Diamond na Zuchu haijawa power couple kama kipindi yupo na Zari ama Wema ambazo zote zilimpa ile controversie au thamani kwa sababu alionekana kama anadate na wanawake ambao wapo on top of fame and beauty.

Kwa hiyo hii couple naona inamfaidisha Zuchu kuliko Diamond
 
Suala la ndoa nilikuwa siamini hadi niliposhtuliwa na mtu wangu nyeti, nilidhani ni drama tu.

Mwanzoni nilidhani pengine Diamond anaona aibu kwa ukubwa wake kuonekana anatoka kimapenzi na mfanyakazi wake, ila sasa kaamua kuoa kabisa sielewi.

Sijui kwanini aliamua kuyaweka mahusiano yao chini ilhali kwa Zuchu haiko hivyo.
 
Saa hizi watakuwa wanalia kama wamefiwa 🤣🤣 maana huyu alikuwa mwana chama mtiifu wa kataa ndoano
Kwakweli Zuchu ametuinua sana, itabidi wanawake tuitishe kikao tujadili kombe la kumpa mwenzetu na zawadi siku ya ndoa yao.
 
Hii ni habari njema sana... itawasaidia CHADEMA kushinda majimbo mawili ya uchaguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…