Hebu tuache utani, hivi inawezekanaje CCM na Serikali wakaupotezea msiba wa mtu muhimu sana kwa Taifa kama Profesa Sarungi?

kilichonishangaza mimi ni kwamba huyo maria sarungi yuko hapo kenya yaani kama ni kweli serikali ya tanzagiza inamtafuta na imeshindwa kumpata basi hii tuko broken kama klk tunavyodhania, fikiria mkenya atafutwe na serikali ya kenya halafu akimbilie tanzagiza angekamatwa fasta kama mwizi …
 
Wakati anahudumia hakuwa analipwa? Acheni ushabiki wa kipumbavu. Hakuna mtu ambaye hajahudumia nchi yake kwa nafasi aliyopo. Hata Mama Ntilie anahudumia taifa kwa kuuza chakula kwa walalahoi. Bodaboda nao wanasaidia taifa kwa usafiri. Hayati Sarungi naye kahudumia taifa kupitia taaluma yake huku akilipwa stahiki zake zote. Kila mtanzania ana CV yake ya kuheshimiwa. Acha kutengeneza matabaka.
 
Makamu mwenyekiti CCM Mzee Wasira, Rais Mstaafu Kikwete, Waziri Ridhiwani na viongozi wengine wa chama na serikali walifika msibani, je hao hawatoshi? Tatizo lenu ni upumbavu wa kutaka Rais aende.
 
Makamu mwenyekiti CCM Mzee Wasira, Rais Mstaafu Kikwete, Waziri Ridhiwani na viongozi wengine wa chama na serikali walifika msibani, je hao hawatoshi? Tatizo lenu ni upumbavu wa kutaka Rais aende.
Hujui kitu wewe, Shut Up!
 
Mkuu,

Bila ya kujali malezi na elimu ya Maria, wala sababu zake za kutokuja kumzika baba yake, hili ni jambo la familia ya Sarungi.

Kwa nini watu baki wasio wa familia wanajiona wana haki ya kuiingilia hii familia kwenye mazishi ya mzee wao?
Kuna nafasi ukifika serikalini wewe unakuwa ni mali ya umma. Acha ujuaji. Uliwahi kuona CDF Mstaafu anafariki kisha anazikwa kiraia??
 
Kuna nafasi ukifika serikalini wewe unakuwa ni mali ya umma. Acha ujuaji. Uliwahi kuona CDF Mstaafu anafariki kisha anazikwa kiraia??
Unajuaje kuwa Profesa Sarungi mwenyewe alitaka kuzikwa na hao viongozi wa chama na serikali?
 
ccm na uongozi wake kwa mtu aliekuwa msafi siyo fiasadi hawana ujamaa naye ukiwaona kwenye msiba basi huyo marehemu alikuwa mtu wa Dili mwenzao
 
CCM wana siasa za kishamba sana,wanafanya ufisadi lakini hawataki kukosolewa ukiwakosoa wanatengeneza bifu na visasi.
 
Hatujadili hypotheticals, seeing is believing
Hii si hypothetical.

Umeona wosia wa Sarungi na kasema nini kuhusu viongozi wa chama na serikali kumzika?

Stephen Wasira, Makamu Mwenyekiti wa CCM, kaenda msibani. Mjane wa Profesa Sarungi kampa maneno yake, kamwambia nyie viongozi mlikuwa wapi wakati Profesa anaumwa, hamkuonekana, mnaonekana sasa kashafariki? Wasira katoka nduki.

Sasa familia hiyo kitu gani kinakufanya ufikiri inataka viongozi wa chama na serikali wahusike kwenye msiba wao?
 
Kwani imeshindikana vp Rais kuungana na familia kwenye msiba au kumtuma makamu wake. Wakaona wamtume Riz Moko. Huu kweli ni uungwana!? La hasha!
ni sahihi Rais kutokwenda, marehemu ni mwanasiasa mstaafu, safu ya viongozi walioenda inatosha sana kuonyesha uwepo wa serikali
 
Makamu mwenyekiti CCM Mzee Wasira, Rais Mstaafu Kikwete, Waziri Ridhiwani na viongozi wengine wa chama na serikali walifika msibani, je hao hawatoshi? Tatizo lenu ni upumbavu wa kutaka Rais aende.
uwepo wa serikali msibani ni wakutosha
 
Unajuaje kuwa Profesa Sarungi mwenyewe alitaka kuzikwa na hao viongozi wa chama na serikali?
Sio suala la kutaka, bali ni lazima. Jifunze kutofautisha hayo mambo mawili.

Mzee Mkapa (RIP) angeweza kutaka asizikwe kitaifa?? Na wahusika wangetekeleza takwa hilo??

Unaifahamu miongozo husuiana na misiba ya viongozi wa kitaifa??

Rais wa Malawi Joyce Banda alitakaga kuingia jikoni kupika chakula cha familia yake, ila wasaidizi wakamzuia asilisogelee huko.

Sasa huyo mbona alitaka ila akakatazwa??
 
Watanzania wengi kama wewe hamjui hata uhuru wa mtu binafsi ni nini.

Ndiyo maana mnaburuzwa kila siku.

Mnapelekwa kama nyumbu na CCM na mnaenda tu.
 
Watanzania wengi kama wewe hamjui hata uhuru wa mtu binafsi ni nini.

Ndiyo maana mnaburuzwa kila siku.

Mnapelekwa kama nyumbu na CCM na mnaenda tu.
Kuna level ukifika, wewe ni kioo cha Taifa na kamwe hauwezi kuishi kama zamani/unavyojisikia. Kubali au kataa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…