Hebu tusemezane: Ulianza kazi mwaka gani na mshahara wako wa kwanza ulikuwa kiasi gani?

Hebu tusemezane: Ulianza kazi mwaka gani na mshahara wako wa kwanza ulikuwa kiasi gani?

Ajira yangu ya kwanza (baada ya kumaliza Form Six 1976) ilikuwa na mshahara 760/= (Shilingi), ondoa kodi Sh. 90, take home Sh. 670/- (zilikuwa nyingi saaaaaana).

Enzi hizo noti kubwa ilikuwa ya Shilingi 10.
Enzi hizo 1$ = 7 Shillings, 1£ = 20 Shillings.

Nilimaliza degree mwaka 1981, mshahara ulikuwa Sh. 1,400/-, nakumbuka wenzetu walioapply kwenye mashirika na kufanikiwa walikuwa na mshahara kwenye Sh. 2,000/-.

Waliokuwa wakifanya kazi East African Community ndiyo wakipata mishahara mikubwa.
[emoji119][emoji119][emoji119][emoji119][emoji119]
 
Mwaka 1983 nilianza kazi Serekalini kwa mshahara al_maarufu enzi hizo; "Four Figures" Gross salary ilikuwa Tsh 1050. Baada ya makato ilikuwa inagota laki 9.... Mihela mingi tu wakati huo. 😂
laki tisa au shilingi mia tisa?

Wewe tuko age group moja mimi nilimaliza degree 1981
 
2009 Niliajiriwa posta mshahara ulikuwa ni Elfu 70 (elimu nilikuwa nimemaliza kidato cha nne shemeji yangu akanipigia pande hapo)

2017 nikapata ajira rasmi mashahara nilianza na 1.6 milioni
Plus over time 40K per day
Housing laki 2 na busy
Transport laki na nusu
N.K
Chini ya miaka 10 ukavuka toka elfu 70 mpaka 1.6M

Hii inatakiwa initie moyo au inivunje moyo
 
Nimejikuta nawaza tu....

Binafsi ajira yangu ya kwanza ilikua mwaka 2000, na mshahara wangu ulikua 115,000Tsh.

Nakumbuka nilikua nimemzidi babayangu mshahara na alishangaa sana.
Mh mjumbe naomba nikae kimya...[emoji41]
 
Back
Top Bottom