Hebu wanawake wa hapa JF ondoeni huu Mkanganyiko!

Hebu wanawake wa hapa JF ondoeni huu Mkanganyiko!

Nimecheka balaa tukalale mtu wangu kesho tugombanie daladala harufu ya ban inaanza kunukia hapa [emoji23][emoji23][emoji23]
Kweli aisee wanatupotezea muda tu, sema sababu kesho ni jmosi bila hivyo ningewatema mapema tu
 
Tafuta pesa mkuu ujenge utoke kwenye Upangaji,Mimi nilijenga kwangu nikiwa nina miaka 27,leo nina miaka 34,unaona namna ninavyofurahia maisha!

Na siyo kujenga tu,bali ujenge nyumba kali ya viwango!.

Huu ni ushauri nakupatia mkuu!
Mm sijengi na hakuna kitu utafanya. Dunia njia, najengaje njiani?
 
Mimi na salamu ni vitu viwili tofauti,salamu zimefanya waafrika wengi wamekuwa masikini!

Hebu nyie mademu wa hapa Jf naomba mniondolee huu utata(Mkanganyiko) ambao unaendelea kunitia wasiwasi humu Jf.

Kumekuwa na utaratibu siku hizi humu Jf hata wanaume kutumia Id za kike,sijajua lengo la wao kufanya hivyo ni kitu gani!

Kwakuwa uongo na utapeli hapa Jf umekuwa wa kutosha,naomba kesho niwatoe wafuatao "OUT" ili kujiridhisha kweli kama ni KE na wala siyo ME.

MALENGO

Malengo ya Kutoka Out ni Kufahamiana,Kubadirishana Mawazo na Ku-Enjoy kwa pamoja kama wanafamilia wa JF.

Kwakua watumiaji wengi wanaotiliwa mashaka ni wanaotumia Id zenye majina ya KE,naomba wafuatao ikiwapendeza kesho tutoke wote kama Familia ili niamini kweli ni KE.

1. Jemima Mrembo
2. cocastic
3. MZURI SANA
4. Lamomy
5. Demi
6. To yeye
7. Leejay49
8. Carleen
9. recho Jr
10. Hornet

Kama nilivyosema,lengo ni kufahamiana,kubadirishana mawazo na Ku-have funny!

ENEO

Eneo ambalo kwangu nahisi litakuwa Karibu na nililolizoea ni pale Mlimani City Samaki- Samaki,Ila nyie mnaweza pia mkapendekeza eneo ambalo mtakuwa mnaona mko- Comfortable kuenjoy.

Nimependekeza hao wanawake kwa siku ya Kesho kwasababu gharama za kuwamudu ninazo,watakula watakacho na kunywa watakacho!.

Nia na Lengo ni kuondoa huu utata wa kudhani nyie ni madume,naombeni mnidhitishie kwa vitendo hiyo Kesho.

Wengi wenu nafahamu mnao usafiri wenu binafsi lakini itakuwa vema kila mmoja akatumia Uber au Bolt ili tuweze kuwa Comfortable zaidi(Ili wasiokuwa na usafiri wasijisikie vibaya).

Fedha ya Usafiri nitalipia mimi,wala msijali!

Naomba kufahamu ratiba zenu nyote niliowatag ili nijue nafanyaje,nitakapojua ratiba zenu nitapanga muda sahihi wa sisi kukutana pale!.

Lengo si kutongozana wala mambo ya Ajabu,Lengo ni kufahamiana tu!.

Nawasilisha!
Kwa huyo mzuri sana umepigwa, kwanza jajiunga sijui jana, hiyo ni ID mpya mtu kafungua. Mimi humu JF nina ID moja tu, nashangaa mtu anakuwa na ID nyingi za nini.
 
Kwa huyo mzuri sana umepigwa, kwanza jajiunga sijui jana, hiyo ni ID mpya mtu kafungua. Mimi humu JF nina ID moja tu, nashangaa mtu anakuwa na ID nyingi za nini.
Hizi joined 2023 wengi vilaza
 
Hiyo akili ya kushauri umeipata lini?

Mm hata pesa ya kula tu sina, leo unaniletea story nijenge. Nijenge ili iweje?
Na ndiyo maana hapo mwanzo nilikwambia Tafuta pesa,acha kushinda hapa Mitandaoni na kutukana watu!,Huu muda ni heri ungelala ili asubuhi udamke kibaruani!

Wenzio kazi zetu zishatufanya usiku kulala muda umeenda!,Shauri yako!
 
Kwa huyo mzuri sana umepigwa, kwanza jajiunga sijui jana, hiyo ni ID mpya mtu kafungua. Mimi humu JF nina ID moja tu, nashangaa mtu anakuwa na ID nyingi za nini.
Mkuu we acha tu!
 
Na ndiyo maana hapo mwanzo nilikwambia Tafuta pesa,acha kushinda hapa Mitandaoni na kutukana watu!,Huu muda ni heri ungelala ili asubuhi udamke kibaruani!

Wenzio kazi zetu zishatufanya usiku kulala muda umeenda!,Shauri yako!
Mm sina issue yoyote mkuu, hapa nilipo hata pa kulala tabu. Bora muda uende tu kukuche
 
Back
Top Bottom