View attachment 3655693Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema kuwa chama chake kinaendelea kukabiliwa na vita kali ya kisiasa kwasababu kimekataa katakata kushiriki katika "siasa za udalali".
Akizungumza jana, Agosti 22, 2026, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Heche ameeleza kuwa vita inayoelekezwa kwake binafsi na kwa chama chake inatokana na msimamo wao thabiti wa kukataa kuwa mawakala wa unyonyaji.
“Hii serikali haipaswi kuwa madarakani siyo leo. Jana ilipaswa iwe imeondoka madarakani na ndio maana wanapoona watu hatutaki kufanya siasa za udalali tunapigwa vita kweli kweli,” ameongea Heche huku akiwataka wananchi kusimama imara na kukataa kuyumbishwa.
Heche ameeleza kuwa kukataa kwao "udalali" kumezua hofu kubwa kwa watu ambao amewataja kuwa wamekuwa wakimshambulia kwa maneno kila wanapopata fursa akisema, “Ukisikia kila siku waziri akitokea huku, ‘Heche tu, Heche, Heche!’... Kwa nini? Kwasababu tumekataa udalali. Sema kataa udalali!”.
Chanzo: Jambo TV