Heche: Napigwa vita kwa sababu nimekataa siasa za udalali

Heche akiamka ni Samia,baada ya chai Samia,baada ya chakula Samia,jioni Samia,usiku Samia daah .Yaani politics of issues ilikufa kitambo
Jizi na lipenda rushwa nalo linatoa comments bila aibu
 
Kuna shida maana maridhiano sio kua wewe unataka hiki na kile na lazma kikubaliwe...ukifikia huko hamna maana ya maridhiano.Ingawa najua na ninayo imani kua watu wanafanya hivyo ili wasipotee kwenye political media
Hivi tukikubaliana kuwa jambo flani itafanyika kwa utaratibu huu alafu wewe unakuwa wa kwanza kutuma watu kukivuruga then unarudi tena baada ya vurugu kuwa tukubaliane tena?

Wakati mwingine watu wanashindwa kuwataja watu majina na kuweka video humu jukwaani kwasababu ya sheria za jamiiforum. Kusema ukweli CCM hawahitaji kuridhiana na mtu au kikundi yeyote kwasababu nia yao siyo nzuri.

Fikia Kiongozi anaapisha wasimamizi wa uchaguzi kwenye Ukumbi anatamka wazi kabisa kuwa mkatekeleze kile ambacho utaambiwa na hakuna watakacho tufanya...then baada ya madhara ya hicho wanarudi kuwa tukaridhiane. And next time wanakirudia.

Unyani ni mbaya aisee.
 
Nilijua tunaweza kujadiriana tukiwa neutral ila sasa tukianza kutupa makosa au lawama kwa upande flani kamwe atuwezi kufikia mwisho.
 
Mbona huko UK walionesha ushahidi mkuu, sasa ukisema flani amekula pesa bila kuonesha ushahidi hiyo nayo inakuwa tuhuma?
Kinachotokea kwa huyo wa Tanzania ndo kama kilichomkuta yule wa UK? Zilikuwa tuhuma kama ambavyo huyo anayejipa umuhimu kwenye nchi anavyotuhumiwa. Wanasiasa wetu wakubali kuwajibika, tuhuma wanazowapa wenzao bila ushahidi zikiwageukia na wao wawe tayari kuzijibu.
 
Mkuu kwanini usijifunze kwanza kuandika kwa ufasaha kisha uje huku jukwaani? Uzuri sasa hivi elimu ni bure, unakwama wapi?
Yaani ninapata shida sana kusoma michango yake.
Tatizo la "elimu za hapa na pale" bado ni kubwa sana.

MEMKWA imekufa kwani!!?
 
Maana yangu ni Siasa za kukubaliana,kuheshimiana,kusikilizana,kushirikiana,kushauriana,kujengana nk ndiyo maana halisi ya Siasa za maridhiano. Karibu
Unawezaje kukaa na kuzungumza na mtu aliyeficha upanga (utekaji, kesi feki za ugaidi, mauaji) mgongoni!!??
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema kuwa chama chake kinaendelea kukabiliwa na vita kali ya kisiasa kwasababu kimekataa katakata kushiriki katika "siasa za udalali".

Akizungumza jana, Agosti 22, 2026, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Heche ameeleza kuwa vita inayoelekezwa kwake binafsi na kwa chama chake inatokana na msimamo wao thabiti wa kukataa kuwa mawakala wa unyonyaji.

“Hii serikali haipaswi kuwa madarakani siyo leo. Jana ilipaswa iwe imeondoka madarakani na ndio maana wanapoona watu hatutaki kufanya siasa za udalali tunapigwa vita kweli kweli,” ameongea Heche huku akiwataka wananchi kusimama imara na kukataa kuyumbishwa.

Heche ameeleza kuwa kukataa kwao "udalali" kumezua hofu kubwa kwa watu ambao amewataja kuwa wamekuwa wakimshambulia kwa maneno kila wanapopata fursa akisema, “Ukisikia kila siku waziri akitokea huku, ‘Heche tu, Heche, Heche!’... Kwa nini? Kwasababu tumekataa udalali. Sema kataa udalali!”.

Chanzo: Jambo TV
Hiyo ndiyo kazi yake aache malalamiko na kutafuta huruma ya wananchi. Kama yeye anawasema watu why nao wasimseme.

Ajishikilie.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amesema kuwa chama chake kinaendelea kukabiliwa na vita kali ya kisiasa kwasababu kimekataa katakata kushiriki katika "siasa za udalali".

Akizungumza jana, Agosti 22, 2026, katika Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, Heche ameeleza kuwa vita inayoelekezwa kwake binafsi na kwa chama chake inatokana na msimamo wao thabiti wa kukataa kuwa mawakala wa unyonyaji.

“Hii serikali haipaswi kuwa madarakani siyo leo. Jana ilipaswa iwe imeondoka madarakani na ndio maana wanapoona watu hatutaki kufanya siasa za udalali tunapigwa vita kweli kweli,” ameongea Heche huku akiwataka wananchi kusimama imara na kukataa kuyumbishwa.

Heche ameeleza kuwa kukataa kwao "udalali" kumezua hofu kubwa kwa watu ambao amewataja kuwa wamekuwa wakimshambulia kwa maneno kila wanapopata fursa akisema, “Ukisikia kila siku waziri akitokea huku, ‘Heche tu, Heche, Heche!’... Kwa nini? Kwasababu tumekataa udalali. Sema kataa udalali!”.

Chanzo: Jambo TV
Sahihi ✔️
 
Back
Top Bottom