Pre GE2025 Heche: Posho siku moja tu Bungeni tulikuwa tunalipwa laki nne, halafu Mwalimu kwa mwezi unamlipa laki 4!

Pre GE2025 Heche: Posho siku moja tu Bungeni tulikuwa tunalipwa laki nne, halafu Mwalimu kwa mwezi unamlipa laki 4!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mshahara wa mbunge marekani ni takribani 164% ya mshahara wa mwalimu. Mwambie heche apige hesabu. Unategemea kwa nchi kama Tanzania imlipe mwalimu milioni 100 kwa mwaka kama mbunge?

Sababu zinazofanya wahunge walipwe zaidi ya walimu ni majukumu yao, mfumi wa siasa na uchumi wa nchi.
Wabunge mara nyingi hukabiliana na shinikizo kubwa la kisiasa, uchunguzi wa umma, na wakati mwingine vitisho vya usalama.

Pia wanapaswa kusafiri mara kwa mara kati ya majimbo yao na dodoma.

Walimu hufanya kazi kwa muda mrefu, lakini hatari ya kisiasa na usalama kwa ujumla ni ndogo ikilinganishwa na wanasiasa.
Heche ni mropokaji anayetaka kufanya kwamba kila kitu hakina maana. Ni kweli anakamata wajinga ila uhalisia hauko hivo.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hiki kijamaa kinaumia sana kunyimwa kisikanyage bungeni
Hapo unakuta bibi yako hana hata bima ya afya, mwanao Heri shule anaenda kwa mguu masaaa mawili, unga na mchele unanunua bei ghali, sukari ya kupimiwa, maji shida n.k ila bado unamuona Heche anaumia? Safari ni ndefu sana
 
Sikiliza video mkuu, Hoja yake sio kuwa posho za wabunge ni kubwa zipunguzwe, hoja yake ni kuwa inawezekana wote kulipwa vizuri, wabunge, walimu wote inawezekana kulipwa vizuri iwapo hao wanaolipwa vizuri bungeni wakiamua kupigania maslahi ya wengine.
Unapoleta hoja ya watu kulipwa vizuri at least ulete na suluhisho la mapato yatakayowezesha wote walipwe vizuri.Sidhani kwamba inaamuliwa tu kwamba watu wote wasilipwe vizuri bali kuna kuwa hakuna uwezekano wa kufanya hivyo.
Kulinganisha kundi dogo sana la wabunge na kundi kubwa la waalimu ni misleading ingawa sikubaliani na wabunge kulipwa posho huku wana mishahara kwa standard ya Tanzania ni mikubwa.
Kunapokuwa na tatizo basi lete solution kwa kuelezea vyanzo vya mapato vitavyowezesha wote walipwe vizuri.
 
Ni mpumbav pekee tu atapingana na hili analolisema Heche.Tuna ndg zetu ambao ni walimu ni shida tupu.Hata kwenye hizi halmashauri zetu mfagia ofisi tu yuko juu ya mwalimu anaweza kumkolomea anavyotaka, afisa elimu ndio usiseme anaweza kumzaba makofi mwalimu 😂😂😂
 
Unaongea kama vile walikuwa majority. Niambia kupokea kwao stahili zao kuli affect vipi adhma yao ya kusimamia serikali na kuwatetea wananchi wenzake? Ni bora kuendelea kupokea stahili zao kuliko kukimbia mapambano kwa kisingizio kuwa hakubaliani na stahili zake. Hypocrites ndio watasema kuwa amepoteza credibility.

Amandla...
Hukimbii mapambano bali unakuwa mstari wa mbele kupigania unachokiamini kwa vitendo. Unapokea huku unakosoa ni crocodile tears.
 
Mliambiwa hawa ni wanaharakasti hamuelewi..

Kwenye office , Head of Sales analipwa Mil 18, na dereva analipwa laki 3 , hapo kuna unyonyaji mmoja ampunguzie mwingine?

Nilifikiri kwa mtu mwenye hadhi yake angeongelea Muundo wa Bunge na namna gani wanaweza punguza vikao na safari zisizo na tija yeye analinganisha mishahara?

Duniani kote watu wanalipwa kutokana na Value na Impact anayoweza sababisha kwenye jamii..

Kalangabhao
Mbunge wa CCM ana value gani, impact ipi kwenye jamii!!??
 
Jiulize mtu analipwa 570,000 bunge la budget x siku 90 = 51,300,000 nje na mishahara mitatu 18M x 3 = 54,000,000 jumla 105,300,000 ndani ya miezi 3, hapo ni nje na rushwa + ziara za kamati. Hawa ni wanyonyaji wakubwa
Aisee
 
Heche ni populist tu wakat alikua anazipokea hzo hela kwa bashasha yote. Wabunge hawazidi Mia tatu ufananishe na walimu ambao ndo sekta inayoongoza kwa kuajriwa kweny ajira rasmi nchi nzima.
 
Hapo unakuta bibi yako hana hata bima ya afya, mwanao Heri shule anaenda kwa mguu masaaa mawili, unga na mchele unanunua bei ghali, sukari ya kupimiwa, maji shida n.k ila bado unamuona Heche anaumia? Safari ni ndefu sana
Sio rahisi shem
 
Back
Top Bottom