Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Naunga Mkono hoja.
 
Kimamlaka,

Huyo mtu wa pili,

Hana JINSIA, Hana dini, Hana kabila.

Anatakiwa asimamie KATIBA na SHERIA za Nchi.

Kumbuka kiapo; Mimi......., Naapa kwamba, nitailinda na kuitetea Jamuhuri ya Muungano wa......,

Ee Mwenyezi Mungu nisaidie.

Mkataba wa DP world, unakuja na vipengele ambavyo viko juu ya Katiba ya nchi.

Mabadiliko ya haraka yanahitajika Ili Nchi iendelee kuwa salama.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen
 
Mama alikusudia kuwaletea watanganyika maendeleo flani (kwa alivyoona yeye) kwa kuwapa DPW bandari za Tanganyika tu. Leo Watanganyika WAMEKATAA KABISA jambo hilo. Je, yeye (mama) ANAHESHIMU MAWAZO YA WATANGANYIKA? Hili jambo ni gumu sana kuliko yeye anavyofikiria au kushauriwa. Aachane na mpango wake wa DPW aone kama hatarudisha furaha kwa watanganyika na ukiwafurahisha watu hawawezi kukuvunjia HESHIMA.
 
Kwa sasa nadhani mnaelewa kwanini dini ya kiislamu imekataa mwanamke kuwa kiongozi kwenye jamii ambayo wanaume tena weny ya kuongoza wapo. Allah aliona mbali, angebaki katika misingi ya dini yake wala asingetukanwa. Ilitosha awe makamo au waziiri tu
 
Kuruhusu aina ile ya makubaliano kuwafikia watanzania kuyapeleka hidi bungeni, na kuwaambie eti watu waendelee kuujadili ni tusi kubwa na dharau kuliko dharau nyingine yoyote ile utakayoweza kuilalamikia.

Yeyote aliyeruhusu lile kwa kweli hana staha na amekosa kabisa adabu. Anastahili kuwajibika.
 
kabla ya yote niruhusu niseme juu yako Pascal, wewe ni mnafiki na una woga pia..una kaujinga fulani ambamo ndani yake kuna upumbavu mwingi unaodumaza uwezo wako wa kufikiri sawa na umri wako.

Mara nyingi nimekuwa nasema hapa nchi hii ina umri zaidi ya miaka 60 ni umri wa mtu mzima anaelekea kuwa Mzee, kwenye jamii yetu tuanzie kwenye familia zetu hutarajii mtu wa umri huu awe kama kijana au mtoto kwa maneno na matendo yake..suala la kuheshimiana si la siku moja au ni kwa ajili ya tukio fulani, kuheshimiana inapaswa kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku!!

Kwa hali ilivyo neno kuheshimiana halipo hapa Tanzania na walio leta hali hii ya kutoheshimiana ni Viongozi!

Matendo na maneno yao mengi hayajengi tuwe nchi tunayoheshimiana, mfano wale wote ambao si wana ccm wanaonekana ni raia daraja la chini mbele ya viongozi wa ccm na wana ccm, rejea kiongozi anawaambia watu ataleta maendeleo kwenye eneo lao pale tu watakapomchagua mwana ccm, wasipomchagua hawastahili maendeleo wakati kodi wanayolipa haitofautishi kati ya mwana ccm na asiye mwana ccm, matendo ya kuvuruga uchaguzi, vitisho kutisha watu kuwa watapotezwa, kiongozi kukiri na kuhamasisha watu waitane chawa na kuwa yeye ana chawa wake..kifupi chawa ni mdudu anaishi kwenye maeneo ya mwili wa binadamu ambayo mengine si staha kuyatamka hadharani, siri siri nyingi kwenye mambo ambayo watu wanapaswa kujua, mfano kiongozi anapokuwa mgonjwa, anaulizwa kiongozi mmoja anasema Rais ni mzima anaendelea na kazi, halafu badae jioni taarifa ya kifo inatolewa..tabia ya kukaa kimya pale watu wanapolalamikia au kuuliza jambo fulani rejea mambo ya tozo kwenye miamala ya simu nk yote haya hayaleti kuheshimiana..hivyo, kabla hujaleta huu wito kwa raia ungeanza kwanza kwa viongozi uwaambie waache tabia ya kutokuheshimu watu, na wasidhani, kiongozi ni kuwa na akili kupita wote wasio viongozi, ukiona umefanikiwa then ungeleta rai yako kwa raia kwamba ni vyema raia kuwaheshimu viongozi wote na si mtu mmoja!

Mwisho ni wewe Pascal tena, jifunze kuleta hoja zinazoonyesha unaheshimu wanaosoma unayoandika!
 
Acheni Watanganyika 🙏 vyao.. urithi huu ulitunzwa vizuri kisha anakuja mtu hata hatumjui kwenye Marathi anauza mali ya yatima... mjalana ... Watanzania now wanahisi wamepata False President
Huu ni ubaguzi, haukubaliki
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…