Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni makala elimishi ikielimisha kuhusu heshima ni kitu cha bure, hivyo kuwaelimisha wana jf na mitandao ya kijamii, kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote, lakini ni lazima aheshimiwe na wote kwasababu mtu akiishakuwa rais wa nchi, hapo hapo ana assume dual personality, yaani wanakuwa ni watu wawili in one!, hivyo rais wa nchi ni lazima aheshimiwe kwa heshima ya lazima ya kimamlaka, akosolewe kwa lugha ya staha, asitukanwe wala asitusiwe!.

Hoja hii ni kufuatia mjadala mingi kwenye mitandao ya jamii kwenye issue ya Bandari yetu na DPW, kuna watu wamevuka mipaka na kumkosea heshima Rais Samia na kumkosoa kwa lugha kali, kumtweza, kumkashifu na wengine kuvuka mipaka kwa kumtukana hadi matusi ya nguoni!, this is not right!.

Angalizo la Uzalendo Uchawa Vs Uzalendo Halisi!.

Kufuatia kuibuka kwa dhana ya uchawa, kuna watu wanajiita kabisa chawa wa Mama, hivyo mtu kama mimi nikijitokeza kutaka Rais Samia aheshimiwe wote, watu wenye akili fupi hawachelewi kuniona chawa!. Mimi sio chawa na hili sio bandiko la uchawa! ni bandiko la kukumbushana heshima ya kiasili ya Kiafrika ya heshima kitu cha bure, mkubwa kumheshimu mdogo, na mdogo kumheshimu mkubwa, heshima kwa wote.

Declaration ya Kutosaka Uteuzi.
Kumezuka mtindo wa sisi waandishi wa habari na watu wa media, tukiusifu utawala kwa mazuri au tukisifu viongozi, tunaonekana kuwa tunasaka uteuzi, naomba niwahakikishie tena Paskali hasaki uteuzi wowote na hili Paskali aliisha mueleza mteuzi mwenyewe face to face Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!

The Duality of President. heshima ya lazima ya kimamlaka!, Akosolewe kwa Staha na Asitukanwe!.
Duality ni kanuni ya mtu mmoja ku na personalities mbili kwa wakati mmoja.
Rais wa nchi ni dual personality ana personalities mbili ambazo ni duality but they exist in one!. Yaani ni mtu mmoja mwenye two personalities ambazo zina exist in one and at the same time.

Kanuni hii ya double personalities au dual personality imezungumzwa vizuri na Mwana Saikolojia mahiri wa Marekani, Dr. Segmund Freud katika kukichambua kitabu cha Dr. Jekyll and Mr. Hyde, kilichoandikwa na Dr. Robert Luis Stevenson aliyeandika pia kitabu cha Kisiwa chenye Hazina, Treasure Island, ambapo mtu mmoja mwenye double personality mchana yuko vingine na usiku yuko vingine kama watu wawili tofauti.

Hii duality ipo sana katika jamii zetu mfano mzuri ni wanga, wachawi na washirikina, ukiwaona mchana ni watu wa kawaida, lakini usiku ni watu wengine kabisa!.

Persnality ya kwanza ya Rais wa nchi ni mtu binadamu, a human being kama binadamu mwingine yoyote wa kawaida anayeitwa Samia Suluhu Hassan, Huyu ni human being, she has feelings, compassion na ana mahitaji mengine yote ya kibinaadamu ikiwemo heshima, love and dignity and can make mistakes just like any other human beings. Hivyo huyu Samia ambaye she is only a human, unaweza kumpenda au usimpende, unaweza usimkubali, unaweza kumbeza, unaweza kumtukana na kumdhalilisha au kusema chochote kumhusu mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan na hakuna tatizo!. Mfano mzuri wa hili ni huyu mtu niliyemzungumzia hapa Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu? bandiko kama hili liliwezekana kupandishwa kwasababu she is just a human na enzi hizo alikuwa na single personality, sasa with dual personality bandiko kama hili haliwezi kupanda.

Personality ya pili ya Rais Samia, ni rais wa nchi, hivyo huyu binadamu anaitwa Samia Suluhu Hassan, baada ya kuwa ni rais wa nchi, assume kitu kinachoitwa presidential personality, huyu sasa sio mtu binadamu, ni mtu taasisi yenye mamlaka ya juu kabisa ndani ya JMT, hivyo rais wa nchi kwa personality yake ya urais, ni lazima aheshimiwe, utii kwa mamlaka, huwezi kumtukana, huwezi kumdhalilisha, itakuwa ni kuitukana taasisi ya urais.

Rais Samia kama taasisi ya urais, huhitaji kumpenda lakini ni lazima kumheshimu. Rais Samia kama taasisi ya urais, she is not human, hawezi kufanya makosa ndio maana hawezi kushitakiwa!.

Wito kama huu niliwahi kuutoa enzi za utawala wa JK, Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim! na wakati wa Magufuli pia nilishauri Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli
Hivyo sasa tuko na Samia, tunaweza tusimpende lakini lazima tumuheshimu na ukitokea ukosoaji, tumkosoe kwa lugha ya staha na sio kumtukana na kumdhalilisha.

Niliwahi kushauri humu kuwa Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda unaweza usimpende lakini ni lazima kumheshimu.

Hitimisho
Rais Samia ni rais wetu, tumpende, tumheshimu, tumsuport, na hata ikitokea, kuna sehemu anakosea tumkosoe kwa heshima na staha.
Kwa sisi wengine ambao tunamkubali Samia kama Mama, mzazi wako, hata akukosee vipi, kamwe huwezi kumtukana!. Samia ni Mama wa Taifa, tumheshimu, namalizia kwa msisitizo huu

Heshima Kitu cha Bure, Rais Samia, ni lazima aheshimiwe na wote, akosolewe kwa staha na asitukanwe!.​

Paskali
Naunga Mkono hoja.
 
Kimamlaka,

Huyo mtu wa pili,

Hana JINSIA, Hana dini, Hana kabila.

Anatakiwa asimamie KATIBA na SHERIA za Nchi.

Kumbuka kiapo; Mimi......., Naapa kwamba, nitailinda na kuitetea Jamuhuri ya Muungano wa......,

Ee Mwenyezi Mungu nisaidie.

Mkataba wa DP world, unakuja na vipengele ambavyo viko juu ya Katiba ya nchi.

Mabadiliko ya haraka yanahitajika Ili Nchi iendelee kuwa salama.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen
 
Mama alikusudia kuwaletea watanganyika maendeleo flani (kwa alivyoona yeye) kwa kuwapa DPW bandari za Tanganyika tu. Leo Watanganyika WAMEKATAA KABISA jambo hilo. Je, yeye (mama) ANAHESHIMU MAWAZO YA WATANGANYIKA? Hili jambo ni gumu sana kuliko yeye anavyofikiria au kushauriwa. Aachane na mpango wake wa DPW aone kama hatarudisha furaha kwa watanganyika na ukiwafurahisha watu hawawezi kukuvunjia HESHIMA.
 
Kwa sasa nadhani mnaelewa kwanini dini ya kiislamu imekataa mwanamke kuwa kiongozi kwenye jamii ambayo wanaume tena weny ya kuongoza wapo. Allah aliona mbali, angebaki katika misingi ya dini yake wala asingetukanwa. Ilitosha awe makamo au waziiri tu
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za kwa maslahi ya taifa, makala ya leo ni makala elimishi ikielimisha kuhusu heshima ni kitu cha bure, hivyo kuwaelimisha wana jf na mitandao ya kijamii, kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote, lakini ni lazima aheshimiwe na wote kwasababu mtu akiishakuwa rais wa nchi, hapo hapo ana assume dual personality, yaani wanakuwa ni watu wawili in one!, hivyo rais wa nchi ni lazima aheshimiwe kwa heshima ya lazima ya kimamlaka, akosolewe kwa lugha ya staha, asitukanwe wala asitusiwe!.

Hoja hii ni kufuatia mjadala mingi kwenye mitandao ya jamii kwenye issue ya Bandari yetu na DPW, kuna watu wamevuka mipaka na kumkosea heshima Rais Samia na kumkosoa kwa lugha kali, kumtweza, kumkashifu na wengine kuvuka mipaka kwa kumtukana hadi matusi ya nguoni!, this is not right!.

Angalizo la Uzalendo Uchawa Vs Uzalendo Halisi!.

Kufuatia kuibuka kwa dhana ya uchawa, kuna watu wanajiita kabisa chawa wa Mama, hivyo mtu kama mimi nikijitokeza kutaka Rais Samia aheshimiwe wote, watu wenye akili fupi hawachelewi kuniona chawa!. Mimi sio chawa na hili sio bandiko la uchawa! ni bandiko la kukumbushana heshima ya kiasili ya Kiafrika ya heshima kitu cha bure, mkubwa kumheshimu mdogo, na mdogo kumheshimu mkubwa, heshima kwa wote.

Declaration ya Kutosaka Uteuzi.
Kumezuka mtindo wa sisi waandishi wa habari na watu wa media, tukiusifu utawala kwa mazuri au tukisifu viongozi, tunaonekana kuwa tunasaka uteuzi, naomba niwahakikishie tena Paskali hasaki uteuzi wowote na hili Paskali aliisha mueleza mteuzi mwenyewe face to face Pongezi Zangu ni Bonafide-Genuine! Sisaki Teuzi, Sitaki Teuzi, Niko Naye Mbeya, Nitamweza!

The Duality of President. heshima ya lazima ya kimamlaka!, Akosolewe kwa Staha na Asitukanwe!.
Duality ni kanuni ya mtu mmoja ku na personalities mbili kwa wakati mmoja.
Rais wa nchi ni dual personality ana personalities mbili ambazo ni duality but they exist in one!. Yaani ni mtu mmoja mwenye two personalities ambazo zina exist in one and at the same time.

Kanuni hii ya double personalities au dual personality imezungumzwa vizuri na Mwana Saikolojia mahiri wa Marekani, Dr. Segmund Freud katika kukichambua kitabu cha Dr. Jekyll and Mr. Hyde, kilichoandikwa na Dr. Robert Luis Stevenson aliyeandika pia kitabu cha Kisiwa chenye Hazina, Treasure Island, ambapo mtu mmoja mwenye double personality mchana yuko vingine na usiku yuko vingine kama watu wawili tofauti.

Hii duality ipo sana katika jamii zetu mfano mzuri ni wanga, wachawi na washirikina, ukiwaona mchana ni watu wa kawaida, lakini usiku ni watu wengine kabisa!.

Persnality ya kwanza ya Rais wa nchi ni mtu binadamu, a human being kama binadamu mwingine yoyote wa kawaida anayeitwa Samia Suluhu Hassan, Huyu ni human being, she has feelings, compassion na ana mahitaji mengine yote ya kibinaadamu ikiwemo heshima, love and dignity and can make mistakes just like any other human beings. Hivyo huyu Samia ambaye she is only a human, unaweza kumpenda au usimpende, unaweza usimkubali, unaweza kumbeza, unaweza kumtukana na kumdhalilisha au kusema chochote kumhusu mtu anayeitwa Samia Suluhu Hassan na hakuna tatizo!. Mfano mzuri wa hili ni huyu mtu niliyemzungumzia hapa Ikitokea kuna Kiongozi ana Macho mazuri, na umeyapenda, je, kuna ubaya kumsifia macho yake? Ni ukosefu wa heshima na adabu? bandiko kama hili liliwezekana kupandishwa kwasababu she is just a human na enzi hizo alikuwa na single personality, sasa with dual personality bandiko kama hili haliwezi kupanda.

Personality ya pili ya Rais Samia, ni rais wa nchi, hivyo huyu binadamu anaitwa Samia Suluhu Hassan, baada ya kuwa ni rais wa nchi, assume kitu kinachoitwa presidential personality, huyu sasa sio mtu binadamu, ni mtu taasisi yenye mamlaka ya juu kabisa ndani ya JMT, hivyo rais wa nchi kwa personality yake ya urais, ni lazima aheshimiwe, utii kwa mamlaka, huwezi kumtukana, huwezi kumdhalilisha, itakuwa ni kuitukana taasisi ya urais.

Rais Samia kama taasisi ya urais, huhitaji kumpenda lakini ni lazima kumheshimu. Rais Samia kama taasisi ya urais, she is not human, hawezi kufanya makosa ndio maana hawezi kushitakiwa!.

Wito kama huu niliwahi kuutoa enzi za utawala wa JK, Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim! na wakati wa Magufuli pia nilishauri Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli
Hivyo sasa tuko na Samia, tunaweza tusimpende lakini lazima tumuheshimu na ukitokea ukosoaji, tumkosoe kwa lugha ya staha na sio kumtukana na kumdhalilisha.

Niliwahi kushauri humu kuwa Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda unaweza usimpende lakini ni lazima kumheshimu.

Hitimisho
Rais Samia ni rais wetu, tumpende, tumheshimu, tumsuport, na hata ikitokea, kuna sehemu anakosea tumkosoe kwa heshima na staha.
Kwa sisi wengine ambao tunamkubali Samia kama Mama, mzazi wako, hata akukosee vipi, kamwe huwezi kumtukana!. Samia ni Mama wa Taifa, tumheshimu, namalizia kwa msisitizo huu

Heshima Kitu cha Bure, Rais Samia, ni lazima aheshimiwe na wote, akosolewe kwa staha na asitukanwe!.​

Paskali
Kuruhusu aina ile ya makubaliano kuwafikia watanzania kuyapeleka hidi bungeni, na kuwaambie eti watu waendelee kuujadili ni tusi kubwa na dharau kuliko dharau nyingine yoyote ile utakayoweza kuilalamikia.

Yeyote aliyeruhusu lile kwa kweli hana staha na amekosa kabisa adabu. Anastahili kuwajibika.
 
kabla ya yote niruhusu niseme juu yako Pascal, wewe ni mnafiki na una woga pia..una kaujinga fulani ambamo ndani yake kuna upumbavu mwingi unaodumaza uwezo wako wa kufikiri sawa na umri wako.

Mara nyingi nimekuwa nasema hapa nchi hii ina umri zaidi ya miaka 60 ni umri wa mtu mzima anaelekea kuwa Mzee, kwenye jamii yetu tuanzie kwenye familia zetu hutarajii mtu wa umri huu awe kama kijana au mtoto kwa maneno na matendo yake..suala la kuheshimiana si la siku moja au ni kwa ajili ya tukio fulani, kuheshimiana inapaswa kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku!!

Kwa hali ilivyo neno kuheshimiana halipo hapa Tanzania na walio leta hali hii ya kutoheshimiana ni Viongozi!

Matendo na maneno yao mengi hayajengi tuwe nchi tunayoheshimiana, mfano wale wote ambao si wana ccm wanaonekana ni raia daraja la chini mbele ya viongozi wa ccm na wana ccm, rejea kiongozi anawaambia watu ataleta maendeleo kwenye eneo lao pale tu watakapomchagua mwana ccm, wasipomchagua hawastahili maendeleo wakati kodi wanayolipa haitofautishi kati ya mwana ccm na asiye mwana ccm, matendo ya kuvuruga uchaguzi, vitisho kutisha watu kuwa watapotezwa, kiongozi kukiri na kuhamasisha watu waitane chawa na kuwa yeye ana chawa wake..kifupi chawa ni mdudu anaishi kwenye maeneo ya mwili wa binadamu ambayo mengine si staha kuyatamka hadharani, siri siri nyingi kwenye mambo ambayo watu wanapaswa kujua, mfano kiongozi anapokuwa mgonjwa, anaulizwa kiongozi mmoja anasema Rais ni mzima anaendelea na kazi, halafu badae jioni taarifa ya kifo inatolewa..tabia ya kukaa kimya pale watu wanapolalamikia au kuuliza jambo fulani rejea mambo ya tozo kwenye miamala ya simu nk yote haya hayaleti kuheshimiana..hivyo, kabla hujaleta huu wito kwa raia ungeanza kwanza kwa viongozi uwaambie waache tabia ya kutokuheshimu watu, na wasidhani, kiongozi ni kuwa na akili kupita wote wasio viongozi, ukiona umefanikiwa then ungeleta rai yako kwa raia kwamba ni vyema raia kuwaheshimu viongozi wote na si mtu mmoja!

Mwisho ni wewe Pascal tena, jifunze kuleta hoja zinazoonyesha unaheshimu wanaosoma unayoandika!
 
Acheni Watanganyika 🙏 vyao.. urithi huu ulitunzwa vizuri kisha anakuja mtu hata hatumjui kwenye Marathi anauza mali ya yatima... mjalana ... Watanzania now wanahisi wamepata False President
Huu ni ubaguzi, haukubaliki
P
 
Back
Top Bottom