Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Kwanzia Leo na kuendelea uitwe paschalojo nguruwe lenye njaa
 
Kuwa serious Pascal. Ni kwa namna gani tunaweza kumheshimu Rais ambaye amesaini mkataba unao ziweka sheria zote za nchi yake kuwa chini ya Mkataba wa DP World? Kuna masuala sensitive sana yamekubaliwa kwenye ule mkataba na ndiyo maana werevu wanatoa machozi. Toka nianze kuijua mikataba ya kimataifa sijawahi ona mkataba wa kipumbavu kama huu, kwamba ikitokea mkataba ku-conflict na sheria yoyote ya nchi basi mkataba utakuwa juu ya sheria ama kanuni hizo. Kwa mkataba ulio sainiwa DP World watakuwa na uwezo hata wa kuua na wasiwajibike kwa sheria yoyote
 
Aende kwao Zanzibar akaheshimiwe huko sisi Watanganyika tunaanzaje kumheshimu wakati anauza Mali zetu? Si akauze za kwao


Hiiiiii....!!!Tena asituchezee!!
 
Pasko! Umeanza tena! Unajua mtu akikwambia kwa maneno ya upole kuwa hapa umenikosea na ukakaa kimya kama hakijatokea chochote, mpige tusi au kuwa mkali, lazima atakujibu tu, hivyo hii ilikuwa ni njia ya watu kupata majibu wala siyo matusi.
Technic hii inaitwa agent provocateur, sisi waandishi tunaitumia sana, kanuni na maadili ya habari, yanasisitiza ku balance story, lakini kwenye stories za madudu, wahusika wana kwepa the media, hivyo sometimes you have to provoke them to come out, lakini ndio utukane?
P
 
Nimenukuu maneno haya sehemu na yako kwenye kiingereza...

"respect must be earned. It may be demanded"...., in this case as a president, " ....but it can never be imposed. Fear may be coerced, and obedience may be enforced; but respect flows freely from a heart full of appreciation for admirable qualities and behavior..."

......Mwishi wa kunukuu
===================


Kwa kusikitisha, mitazamo yetu wa kuwa na uwezo wa kuchambua na kudadavua mkataba huu ili kujaribu kuivusha na kufikia malengo fulani kwa Nchi yetu tumepigwa(haujazingatiwa kwa mapana yake) na kudharauliwa au kubezwa yaani tunajisikia tunaachwa bila kupewa maanani. (Hatusikilizwi) wameziba masikio!

Hakika wadau hawajapendezwa(binafsi sijapendezwa)na tabia zilizoonyeshwa.

Inaweza kuwa ukweli ni mchungu na ni mgumu kuukumbatia, na kidonge kichungu kumeza. Lakini mwisho wa siku,uwepo angalau, ufahamu kuwa wananchi hawajapenda kudharauliwa!
Uongozi wa CCM na Serikali Wasijiondoe ufahamu.

Mpaka kieleweke.
 
Paschal, siyo lazima kumpenda Rais. Lakini mtu anaweza kuibomoa heshima yake mwenyewe. Kwenye maisha unaweza ukaheshimiwa kweli lakini ukija ukawadharau wale wanakuheahimu pia wao watakudharau na kukupuuza kabisa.
Jiheshimu utaheshimiwa,thamini wengine watakuthamini,wapende wengine watakupenda pia.
Kiongozi huyu ametukosea Sana Watanzania kwa MOU Ile. Paschal haifai na mtu mwenye akili timamu Tena aliyepewa mamlaka ya kuongoza nchi akakubali kusaini mkataba kama ule ni maajabu.
Zaidi ni alituona sisi hatufai, ni wajinga, ametupuuza na hatupendi Toka moyoni.
Bro,kaka. Ni aibu,ni aibu kubwa. Wengi hatukutegemea kuona hilo likifanyika lakini mwenzetu kafanya Tena tukikumbuka tumetoka kupigwa kwenye madini na gesi.
Yeye ni Binadamu na atapita lakini aitendee haki nchi yake kwani hata udongo wake ndiyo utamzika hata zikwa na udongo toka Uarabuni..
Atupende tutampenda,atuthamini tutamthamini, atujali tutamjali
Tanzania ndiyo nchi yetu ya furaha.🇹🇿
 
Pascal Mayalla hoja yako ni nzuri na ni ya msingi sana tena sana. Bahati mbaya sana maji yalishamwagika
No hayajamwagika ni paa letu tuu linavuja na ukuta wa nyumba yetu umepata ufa, mvua zikinyesha tutaangazia panapovuja na kupaziba, na huu ufa tutauziba bila ya kusubiria kujenga ukuta.
kudhihaki/kukebehi/kudharau/kubeza/kukaaa kimya pale kauli tata za kutweza utu wa Dkt Magufuli na yeye mwenyewe pia kutoa kauli tata kipindi cha maombolezo.
Sikumbuki Viongozi kumtweza JPM, kila kinachosemwa kumhusu ni ukweli mtupu!. Mfano kumuita Mwanamke "we malay... " ni kumtweza na kumtukana, lakini kama Mwanamke huyo kweli ni malay. na anaendesha maisha yake kwa shughuli hiyo, kumuita malay. sio kumtukana au kumtweza bali ni kumwambia ukweli!.
Tena tuliandika hata wewe ni shahidi, tena tulimuomba mara kibao hata Maxence Melo waangalie utaratibu wa kufunga na kuzui posti zote zinazotweza utu wa aliyetumikia taifa kwa uzalendo ila hatukusikilizwa.
Hii ndio jf advantage, maximum freedom of expression. Afadhali Max alikataa maana huo pia ni udikiteta
 
Kwa hiyo kaka, akina tibaijuka,warioba,shivji,Adam Malima, Lisu,mbowe,Butiku,mawakili mbalimbali,Diaspora na wengine wengi, wameongea/wanaongea kwa kupotosha???? Ni kichaa tu anayeweza kusaini masharti yale
 
Kwa hiyo kaka, akina tibaijuka,warioba,shivji,Adam Malima, Lisu,mbowe,Butiku,mawakili mbalimbali,Diaspora na wengine wengi, wameongea/wanaongea kwa kupotosha????
Hakuna mtu yoyote anajejua kila kitu, hivyo pia inawezekana they are all wrong. Mimi ni miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kukosoa makubaliano hayo Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! ile mambo yanarekebishika.
Ni kichaa tu anayeweza kusaini masharti yale
Huku pia ni kumtukana kwa matusi ya reja reja!, unamuita kichaa!. Heshima ni kitu cha bure!. Mama yako aliyekuzaa, akifanya jambo usilopendezwa nalo, unaweza kumuita kichaa?.
P
 
Hebu tuoneshe kwenye ile IGA ni wapi pameandikwa waarabu wataendesha baadhi ya magati, halafu mimi nikuoneshe wapi pameandikwa wataendesha bandari zetu zote Tanganyika milele..

Mayalla hii kazi unayoifanya, kupigia debe rasilimali.za taifa kutolewa bure kwa wageni, hata kama unajipendekeza kwa mtawala ili upate chochote, mimi nakuona kabisa unajitafutia laana ya uzeeni, laana utakayokwenda kufa nayo usipotubu mapema.
 

Kwa manitki hiyo hapo juu, ni sawa kabisa SSH aitwe na kuzodolewa kama alivyofanywa na hao wanaomtukana au lah!

Yaani kuwa kinachosemwa kipo! kweli haiingii akilini kudai wanaosema kuna kasoro lukuki huko halafu ionekane wote wakawa wanakosea
Kwa hiyo kaka, akina tibaijuka,warioba,shivji,Adam Malima, Lisu,mbowe,Butiku,mawakili mbalimbali,Diaspora na wengine wengi, wameongea/wanaongea kwa kupotosha????
...Suala zima limekuwa mishandled from the beginning...mnafunika funika vifuu vya moshi. It is sad to imagine wanatoa kifuu kimoja kimoja chenye moto na kinachofuka moshi kutoka kwenye rundo la vifuu vinavyowaka moto. The buck stops with her...as a President she needs to pay attention and do something period.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…