Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Nitamshauri mama, akuone huruma unazeeka na depression, akupe TU u RC ,jaman
 
Nitamshauri mama, akuone huruma unazeeka na depression, akupe TU u RC ,jaman
Mayalla ananishangaza sana, amehangaikia uwakili miaka yote mpaka akaupata uzeeni, sasa baada ya kuupata badala autumie positively kwa manufaa yake, ameamua kujiegemeza kwenye uchawa kwa kupotosha makusudi kupitia taaluma aliyoipatia uzeeni.
 
"Rais Samia kama taasisi ya urais siyo binadamu hawezi kufanya makosa ndiyo maana hawezi kushitakiwa"

"Rais Samia siyo malaika ni binadamu anaweza kukosea"

Tukianza na Samia kama taasisi
Ni kweli hapaswi kufanya makosa kwa kuwa ana kila nyenzo kuhakikisha kwamba anafanya mambo kwa usahihi wake

Lakini haya makosa yanatoka wapi sasa?

sisi kama wananchi hiyo inatuumiza sana
Kuona kwamba tumekupatia kila kitu ili kufanya mambo kwa usahihi lakini bado unafanya makosa jibu ni kwamba hiyo nafasi haikufai kwa sababu hatuna tena cha kukupa

Hiyo imepelekea sisi kukosoa kwa uchungu mkubwa kwa kuonyesha hisia zetu za maumivu tunayopitia kutokana na makosa yanayofanywa na hii taasisi

Rais kama binadamu
Hakuna mtanzania mwenye tatizo nae
Ukiweka tabia hasi za mtu ambazo anaweza kuwa nazo hapa Samia kama binadamu lazima anazo na haziko kwenye mijadala
 
Paskali umekula hongo ya Walodi acha kurukaruka na mi paragraph wewe .Ku declare interest eti hutaki teuzi niuongo mtupu ..nilikuheshimu sana kabla wajumbe kukata mkia pale Kawe ....Wewe shida mileage yako ipo juu sana, umechakaa hutalamba asali kamwe.
 
Utamweshimuje anayekudharau Bwana Paskali Manjaa?!
We huoni kama ni dharau kubwa sana kwa Watanzania kuwalazimisha mkataba ambao wanaona ni wa kuuza uhuru na usalama wa nchi yetu?!
Hebu saa zingine tuachage ushabiki, tutangulize uzalendo.
 
Heshima haiji tu, heshima inatafutwa, hakuna mtu anayeweza kumuheshimu mtu muhuni muhuni asiye na maadili au mwizi. Ukitenda matendo ya heshima utaheshimika ukitenda ya hovyo utadharauliwa. Mimi binafsi huyo uliyemtaja kamwe siwezi kumuheshimu maana hajafanya yanayostahili kuheshimiwa.
 
Anko P!
Respect is earned. Kukalia kile kiti ca patakatifu Magogoni ni synonymous na kuvalia cha Baba yetu RIP Nyerere! Kiatu cha MWALIMU! Nyerere, narudia tena. Ndo kiwango, benchmark. Mengine siandiki kwani kila mwenye kukereketwa basi achanganye na zake. Hadi kufikia kupendekezwa kuitwa MWENYEHERI alafu ati wewe unaandika nini bana kwa hawa wengine in singularis? Nchi ya Nyerere hii.
 
Tanzania hatuna Rais toka alipotutoka Mh. Rais wetu ambaye tulimchagua kwa kishindo cha 81%. Kwa sasa tuko na mwangalizi wa nafasi ya Urais. Ndo maana hata "handling" yake kwa wananchi ni kama ya mama wa kambo kwa mtoto wake wa kambo!
Fuatilia mwenendo wa Rais Hayati JPM kwa wananchi waliompigia kura, na mwenendo wa huyu mama yetu wa kambo utagundua ninachokiongelea.
We mtu gani akina mama wa watu wanakuja wanakulilia uwasaidie matatizo yao, halafu unawaambia wasaidizi wako kwa dharau eti "mwondosheni huyo anatupigia kelele"!

Halafu eti Paskali anawalazimisha hao akina mama wamuheshimu mtu ambaye alitweza utu wao!

Hapana, hii haikubaliki.

Heshima hutangulia heshima.

Ukitudharau, tutakudharau tu.

Hata kama tunajua kwa kufanya hivyo tuna-risk maisha yetu, lakini lazima tutakudharau tu.

Kwa kumalizia, huo mkataba wa DPW, hatutaki kuendelea kuhelimishwa kwa sababu hata ambao hatukwenda shule tunajua kilichomo ndani yake kwa sababu tumesomewa na kufafanuliwa vizuri na watu zaidi ya mmoja. Hivyo kuendelea na hiyo elimu yenu kwetu ni mwendelezo wa dharau kwetu sisi wananchi, ambao kwa sasa ni yatima hadi 2025 tutakapomchagua tena Mh. Rais wa ndoto zetu Inshallah.
 
raisi mwizi tuogope kumwita mwizi. Raisi anatia saini kwenye mikataba ya kijinga tuogope kusema mikataba ya kijinga yenye rushwa ya wazi wazi.
Taifa la watu waoga waoga.

Sijawahi kumsikia raisi samia akihimiza watu kufanya kazi kwa bidii. Kwa sababu anapenda vya dezo.
 
Mkuu umeandika vzr sana.
Kifupi kiongozi anayekwambia eti "nimeziba masikio, nasonga mbele", utamweshimuje?
Uzuri ni kuwa watu wanajua endapo unawapenda kwa dhati au huwapendi.
So, ni vigumu sana kwa mtu ambaye unamwonesha waziwazi kutompenda, eti hakuheshimu! We nani?!!
 
Rais alisha wahi kuwambia watanzania ni milango kwahiyo kelele zao hazito mnyima usingizi. Rais anapokuwa na maneno ya kifedhuri unatweza utu wao, kisha bwana Paschal unataka wananchi wameimbie pambio za hosana mbinguni si ndiyo? mkumbushe rais kama pwani ajazaliwa pekee yake ujivuni, ufedhuri, dharau, kwa watanzania tunamwelewa kwahiyo mkae kwa kutulia.
 
Hebu tuoneshe kwenye ile IGA ni wapi pameandikwa waarabu wataendesha baadhi ya magati, halafu mimi nikuoneshe wapi pameandikwa wataendesha bandari zetu zote Tanganyika milele..
Kwanza nikupe pole, Watanzania Watanzania wanahitaji kuelimishwa IGA ni nini na ya nini na HGA ni nini?. IGA ni makubaliano tuu yaani MoU
Mayalla hii kazi unayoifanya, kupigia debe rasilimali.za taifa kutolewa bure kwa wageni, hata kama unajipendekeza kwa mtawala ili upate chochote, mimi nakuona kabisa unajitafutia laana ya uzeeni, laana utakayokwenda kufa nayo usipotubu mapema.
Duh...!.
P
 
Naunga mkono hoja.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…