Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Wanabodi,

Heshima Kitu cha Bure, Rais Samia, ni lazima aheshimiwe na wote, akosolewe kwa staha na asitukanwe!.​

Paskali
Ninakuunga mkono kwenye hili.
Rais ni alama yetu ya ustawi na amana zote zinazostahili kuheshimika.

Mimi pamoja na kauli zangu kali dhidi ya hawa viongozi wetu na tabia zao zisizoendana na dhamana walizonazo lakini sijawahi kuacha kuwaombea kwa sababu tukiwadhalilisha ni sawa na sisi kujidhalilisha.

Tuwakosoe bila kuvunja utu wao. tuwashauri, tuwakemee, tuwapongeze na kama yapo ya kuwaunga mkono tusioneshe unafiki kwenye hilo.

Amani iwe kwenu
 
Mkuu Ngalikihinja, asante tena, once a teacher, always a teacher, hapa umenifundisha tena somo la heshima mbili,
a true bonafide genuine respect which is earned and derivative respect due to position of power.

Kwa vile rais wa nchi kwa upande mmoja ni mtu binadamu, na kwa upande wa pili ni mtu taasisi, the dividing line kati ya rais binadamu na rais taasisi is very thin, kwa vile rais taasisi ni lazima aheshimiwe, utake usitake, then to be on a safe side ni Rais aheshimiwe!.
P
 
Ikiwa rais haheshimu rasilimali za taifa yafaa nini kumheshimu? Ilipaswa rais ajiheshimu kwanza kwa kutouza rasilimali za taifa kwa waarabu wenzake ndipo heshima yake ingepaa automatically. Heshima ya kulazimisha sio heshima bali ni utwana mamboleo. Jiheshimu uheshimiwe, ukinizingua tutazinguana!
 
Mbona yeye alitutukana STUPID? Kwanini asitukanwe in response kwa matusi yake?
 
Unahisi uko huru sana au sio?
 
Sasa hivi mnakimbilia kwenye hoja ya kijinga sana eti mama anatukanwa. Hoja ya ukabila na ukanda imebuma mnaleta huu ujinga wenu. Alichofanya Rais ni kitendo cha kijinga kuuza nchi. sasa kama ujinga ni tusi basi mnakazi mwaka huu.
 
Kaka Paskali,
Tatizo linaanzia pale watu wanaposhindwa ku- reciprocate heshima. Na hili ni tatizo kubwa sana kwa baadhi ya viongozi wetu. Wapo wanaodhani kuwa heshima waipatayo kutokana na vyeo/cheo walichonacho, inazidi kila heshima nyingine yoyote ile imtu anayotakiwa kupewa.

BTW, It is never true kuwa anayeshimika zaidi ya wote nchini ni rais. Wapo watu kwa waliyoyafanya kijamii wana heshima kubwa kuliko rais kama mwanadamu na si kama rais. Yes, rais lazima aheshimiwe, nakubaliana na wewe kwa 100%, lakini what if yeye ndo chanzo cha kutoheshimiana? Kwamba yeye ndo haheshimu watu? Kitakachofuata ni heshima ya woga kwa rais wetu. Kwamba nahofia kuwekwa ndani masaa aliyoruhusiwa kikatiba..!!

Na by the way, alichokitamka Rostam kuhusu mahakama na baadaye akaomba radhi, ndiyo uhalisia. Kutakosekana tu ushahidi wa wazi, lakini baadhi ya mahakama zetu zipo hivyo na baadhi ya viongozi hutumia nafasi zao kupiga simu moja tu na hukumu ikatoka kwa mujibu wa matakwa ya mpiga simu. KWA SABABU HII, HESHIMA YA WOGA LAZIMA IWEPO NO WAY OUT. Vinginevyo yatakukuta ya kukukuta.
 
Anatakiwa aanze yeye KUHESHIMU maBosi wake wanaomlipa Mshahara wake.... sababu anauza Nchi hata akiambiwa na waajiri wake aache hataki anaamini ktk wajomba
 
Mara tukaanza kusikia kauli za matusi kwenye mikutano ya CHADEMA. Mfano ni ile kauli ya Mdude alisikika akiongea Jukwaani Barracuda Tabata kuwa "Mwambieni huyo Mama yenu, nitamnyoa kwa wembe uleule niliotumia kumnyoa mtangulizi wake"
Duh ...!. Sikubahatika kuusikia hii, ukiweza kutupatia links, tutashukuru, ila kama ni kweli, hizi sio lugha za kistaarabu na kiungwana, niliwahi kushauri Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!
Alitamka maneno mbele ya Mbowe na viongozi wengine wa CDM na hawakumchukulia hatua mpaka leo.
Ni muhimu viongozi wakawakanya wafuasi wao wanapovuka mipaka kwa kutoa lugha na kauli ambazo sio za kistaarabu na kiungwana. Mbowe ni msataafu na muungwana sana, aliwahi kuwasihi wafuasi wake kuacha lugha za kuudhi, ila viongozi wengine wa Chadema bado na mfano mzuri ni huyu Msikie Tundu Lissu Hapa, Anauliza Kama Wenzake Wana Akili Kweli! Maridhiano Ayaita Ujinga. Je, Lissu Bado ni Asset or Sasa ni A Liability?
Kwa mtazamo wangu Serikali imeona pengine bado hatuna busara katika kutumia uhuru wa maoni. Tunaleta matusi badala ya kutoa maoni.
Naunga mkono hoja, tena hakuna kesi yoyote ya uhaini itakayofunguliwa ni kesi tuu ya uchochezi, yaani sedition and not treason!.
P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…