Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!

Na Mwandishi wetu.

Mwenyekiti Jumuiya na Taasisi za Kiislaam nchini Tanzania, Shekhe Mussa Kundecha amefunguka na kukemea wazi wazi kitendo cha chapisho la Picha za Kudhihaki Vazi la kislaam na Waislam wote.

View attachment 3017478
Naendelea kusisitiza viongozi waheshimiwe
P
 
Hata mimi huwa naumia sana kuona Mheshimiwa Rais akitukanwa matusi na vitoto vidogo kama li Mdude Nyagali
Naunga mkono hoja, sisi kaka zao tumo humu na from time to time tunajitahidi sana kuvifunza adabu hivi vitoto visivyo na adabu kwa mabandiko kama haya
P
 
Wanaukumbi.

Vijana wa Tanzania, taifa linalotilia mkazo maadili mazuri mnawezaje kumtukana Rais SuluhuSamia matusi mazito?

Kuna uhusiano gani kati ya kudai haki au kukosoa Utendaji wa Serikali na matusi? Kwani mama au baba zenu wakikosea huwa pia mnawatukana? Badilikeni, matusi sio uungwana.

Kundi la watu wanaojiita wanaharakati ("Team Space") wanatuumia

Nguvu kubwa kugawa watanzania "Divide and Rule" ili Watanzania wasiwe na sauti moja. Matokeo yake mnakuwa kama lugha gongana "mlima babeli"

Harakati hizi ni kwa manufaa ya wachache, haziwezi leta mabadiliko, kamwe!

Haki haipiganiwi kwa matusi au kutweza utu wa wengine. Ni muhimu kukumbusha vijana kwamba hakuna harakati za demokrasia na haki zilizowahi kushinda bila watu kupendana, kuwa wamoja na kuwa na sauti moja. Team Space inatengeneza "DIVIDE AND RULE" harakati za maslahi kupiga hela

PIA SOMA
- Heshima kitu cha bure! Kwanini Rais Samia, japo sio lazima apendwe na wote lakini ni lazima aheshimiwe na wote? Akosolewe kwa staha na asitukanwe!
 
'Wasituambie hawajui (kuhusu utekaji na mauaji). IGP asituambie hajui, Mkurugenzi (Mkuu) wa usalama wa taifa asituanbie hajui, CDF ndiyo mkubwa wao wote, wasituambie wote hawajui... Lazima wajue, la sivyo hawana sababu ya kuwa pale" Mzee Joseph Butiku
 
Unazumgumziaje viongozi wanaongia madarakani kwa kupora chaguzi, kisha wanataka waheshimiwe baada ya kutukana uchaguzi? Kuingia madarakani kwa kupora chaguzi za nchi ni zaidi ya hayo matusi unayosema. Au kupora chaguzi za nchi ni sehemu ya maadili yenu kama taifa?

Siungi mkono mtu au kiongozi yoyote kutukanwa. Lakini kiongozi aliyeko madarakani kwa kupora uchaguzi ana heshima gani ambayo anataka apewe? Unataka heshima, ingia madarakani kwa njia ya heshima, vinginevyo endelea kuweka vikundi vya watekaji ukilazimisha heshima ya uoaga ambayo hutaipata.
 
Wanaukumbi.

Vijana wa Tanzania, taifa linalotilia mkazo maadili mazuri mnawezaje kumtukana Rais SuluhuSamia matusi mazito...
Hoja nzuri ni ile inayotolewa kwa lugha nzuri na staha. Huwezi kumjadili Mhe. Rais na CI kirahisi na lugha isiyo na staha! Uhuru wa maoni ni jambo chanya la maendeleo siyo jinai.πŸ™πŸ™πŸ™
 
As much as I want to agree with you ila ungeanza kwanza kuwakumbusha hao kufanya wajibu wao. Comparison ya Mzazi na Rais doesn't hold water.

Mzazi sikumchagua. Rais anachaguliwa.

Mzazi hanilipishi kodi. Rais na serikali yake wanakula kodi zetu bila kutimiza wajibu wao.

Hapo sijagusia utekaji unaoendelea. Either ni serikali au watu wasiojulikana bado serikali ina wajibu wa kulinda raia na mali zao kama inavyokula kodi zao.

Katika hali kama hiyo huwezi mchagulia mtu silaha.

Afu sifa zote mnampa rais ila lawama mna deflect. You seem to have selective competence.
 
Kutumia makalio kufikiri hya ndo madhara yake ….. rudi nyuma tafakari zike ripoti za CAG ubadhilifu ulio fanywa na serikali inayo ongozwa na huyo chura kiziwi inatosha kusema hafai tena
 
Maadili ni tatizo la jamii. Mkanyage kwa bahati mbaya kijana kwenye daladala sikiliza maneno yanayotoka mdomoni. Dada wa watu abishane tu na konda au kijana mwingine kituoni: sikiliza aina ya maneno yasiyo ya staha yatakayotoka mdomoni hapo. Kwa hiyo, kutumia maneno au kutenda mambo yanaoumiza wengine ndiyo imekuwa silaha yetu siku hizi. Na kwa bahati mbaya mijadala hatuiwezi kwa sababu ni wavivu wa kujenga hoja, isipokuwa tunalazimisha hoja na mtu akitofautiana nasi tunaanza kumtukana au kukimbilia kuanika kashfa alizonazo, hata kama ni za kupika. Shame upon us!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…