HESLB Mikopo kuunganishwa na NIDA, TIN, Passport na kadi za benki

Siku ukiajiriwa serikalin tu wako na wewe.
 
Ama kweli wewe ni Son of the beach, case closed.
Kwanini Mkuu? Au kwavile umegundua sina mpango wa kuwalipa HESLB? Na si mimi tu nisiyetaka kurejesha deni,tupo wengi mno.

Kwanza huyo Magufuli yeye alirejesha lini fedha aliosomeshewa na awamu ya JK Nyerere (au Mwinyi)? Kuna viongozi kibao serikalini ambao walisomeshwa bure na Mzee Nyerere ila hao hao ndo wanakuja kutukazia nati sisi wasaka tonge.

Yaani HESLB imenisomesha kwa less than 20,000,000/= kisha wanakuja kunidai 60,000,000/= , halafu nikubali kiboya boya tu?
 
ha ha ha, asante ametupa mbinu mpya namna watakwepa kulipa deni la HESLB, itabidi kosa la kutolipa Deni liingizwe kwenye uhujumu uchumi ila liwe na dhamana.
Kama mkiona ulazima wa kutufunga tufungeni tu.Kama Rugemalila na Singh Seth wamekomaa mimi nitashindwa nini kukomaa?

Ikibidi panueni magereza kwa ajili yetu wadaiwa wa Bodi ya Mkopo. NA BADO HATUTALIPA.
 
Sasa Passport inahusiana vipi na mkopo? Alaf mbona wanaolipa ni wachache hivyo kulinganisha na waajiriwa.
Mimi nakwambia sijapata kuona watu wa ajabu kama bodi ya mikopo...wapo watu wengi wamenufaika na pesa za bodi ya mikopo lakini hawalipi kwa sababu bodi hawana taarifa sahihi kuwakamata...hivyo bodi wanachofanya ni kuwabambikia madeni ya uongo wale wachache waliojitokeza kulipa kwa hiari
 
hata marekani na uchumi wote ule hakuna anaesoma bure chuo kikuu, sema hii bodi ilikua inatoa mikopo kiholela sana enzi hizo bila kujua itarudi vp, wanakumbuka shuka asubuhi
 
Dah mwamba umenifurahisha sana[emoji3]
 
Yes, nakubaliana na wewe...haina haja ya kuwalipa kwa hiari mpaka pale watakapoacha tabia za ubabaishaji na udhalimu..... imagine mtu alisoma chuo kuanzia 2004 mpaka 2008 kwa mfano...kipindi hicho sheria ya 6% VRF na hii 15% ya marejesho zilikuwa hazijatungwa...leo bodi ya mkopo wanaitumia sheria iliyotungwa mwaka 2016 kumuumiza mtu aliyemaliza chuo mwaka 2008...hii kisheria haiwezekani....ni kiburi kilichochanganyika na ubabe na ujinga.
 
Tena meko alipe na retention fee
 
mpaka ifike 2025, jasho la meno lazma liwatoke watu flani, waliodhani ni ufahari kula hela ya bodi na ya mzazi kwa wakati mmoja.
Wewe uko nje ya mada....kinacholalamikiwa na wengi ni namna bodi ya mikopo inavyokata mishahara ya watu bila utaratibu....
Nakupa mfano: wapo watu nawajua walipelekwa nje ya nchi Urusi, China, India, Algeria, Ukraine etc na serikali mwaka 2005....na wengi waliambiwa ile ilikuwa ni scholarship.....waliporudi tanzania bodi ya mikopo ikawaambia wanadaiwa millions of money....wengi wao wanadaiwa zaidi ya milion 40 mpaka 70 trust me.....bodi ya mikopo bila kutumia busara ya kuzaliwa bado watu hawa wanabanwa walipe 6% of the outstanding amount...hebu nambie kwa mshahara wa serikali mtu huyu ataweza kumaliza deni?
Na kwa nini sheria ya 6% VRF na makato ya 15% of basic salary kila mwezi iliyotungwa mwaka 2016 inatumika kuwakandamiza na kuwadidimiza kwenyw umasikini watanzania hawa?
Tafakuri sasa ujue kwa nini watu hawako tayari kulipa kwa hiari
 
mkuu frustration zitakuua take it easy life is not that serious
 

Ni kwamba Ulipe au Usilipe, hilo deni halitakaa liishe. Tena kama umeajiriwa ndo mpaka ustaafu bado deni lipo ni mwendo wa kulima mafao tu.
 
hata marekani na uchumi wote ule hakuna anaesoma bure chuo kikuu, sema hii bodi ilikua inatoa mikopo kiholela sana enzi hizo bila kujua itarudi vp, wanakumbuka shuka asubuhi
Sio kila kitu mpaka uitaje marekani hata
Marekani waje wajifunze kwetu Mm naimani tunao uwezo wa kusomesha bure chuo Kikuu.......

Kuna nchi wameweka kuwalipa raia wake wasio na Kazi na wazee......


Kwenye hili la kusomesha bure chuo Kikuu inawezekanaa narudia Tena inawezekanaa......
 
well, that would be something new, inawezekana lakini sasa ni mpaka iwezekane!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…