Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 15,835
- 23,776
- Thread starter
-
- #301
BODI haiangalii kadi za chama, wote wanaisoma nambaHakuna jiwe litakalosalia,sioni ccm siku hizi wakiimba kale kawimbo pendwa,sijui kanaitwaje vile but umalizia.......namba
Jibu kwa hoja, wapi hapo yamesemwa na bodi, mi naona mawazo yake tu hapospeculations, okay endelea kukikalisha hapo , utaelewa tu
Chapa lapa, naona unaishi Marekani na huna habari za TanzaniaJibu kwa hoja, wapi hapo yamesemwa na bodi, mi naona mawazo yake tu hapo
siyo matani, hela ya BODI LAZMA ilipwe, tunataka kujenga hospitali kubwa ya Kitalii kanda maalum ChatoKamua mpaka tone la mwisho
endelea na maswali ya ki-MATAGA siku Majembe auction Mart wakija hapo kuuza hicho kibanda cha urithi ndiyo utaelewa ninachotahadharisha hapa, haya mwenyewe naskia anaelekea INDIA akitokea NAIROBI, tuendelee na mfungo wa siku 21 na wenzetu TAGSasa Passport inahusiana vipi na mkopo? Alaf mbona wanaolipa ni wachache hivyo kulinganisha na waajiriwa.
Wanachukua nini wakati SONGESHA NAO WANADAINoma sana, wanaweza wakachukua vocha ya kujiunga kifurushi.
Kwa pesa wanayonidai saizi nikipiga deiwaka sitaki habari za kutumiana M-Pesa wala Tigo Pesa.
USHUHUDA TOKA KWA YALIYOWAKUTA
Wengi waliosoma nje ya nchi kwa kulipiwa na bodi ya mikopo (HESLB) wanadaiwa fedha nyingi kulinganisha na waliosoma nchini. Nimeona jamaa ana mshahara 900K but anadaiwa 47M. Kwa mwezi atakatwa 143K, kwa mwaka 1.7M. Under "ceteris paribus" mwamba atahitji miaka 28 kumaliza deni lake. Lakini ukiongeza "rention fee" atahitaji miaka 35 kumaliza deni.
Assume ana mika 30 kwa sasa. Jumlisha 35 ya kulipa deni atakua na miaka 65. Umri wa kustaafu ni miaka 60. Maana yake atastaafu bila kumaliza kulipa deni. Ikitokea hivyo Bodi itaenda kukomba kiinua mgongo chake kumalizia deni (kama sheria inavyosema). Sasa jiulize je huku ni kumsaidia mtanzania au kumkomoa?
Kunapaswa kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu mikopo ya elimu ya juu. Wazazi wanaoweza kusomesha watoto wao kwa kuwalipia ni vizuri wafanye hivyo, badala ya kuwaingiza kwenye mikopo hii inayoumiza. Pili, wazazi wasio na uwezo serikali iwape watoto wao ruzuku (bursary) si mikopo (loan).
Awamu ya kwanza na ya pili serikali iliwapa ruzuku wanafunzi wote wa elimu ya juu. Awamu zilizofuata zikaondoa ruzuku na kuleta mikopo. Nyerere na Mwinyi waliweza nini ambacho kimewashinda waliofuata?
Wakati wa Nyerere na Mwinyi wanafunzi wa vyuo vikuu walikula bure, kusoma bure, na kulala bure. Na bado walipewa pesa ya kujikimu. Kuna kipindi nchi ilipita kwenye hali ngumu kiuchumi Nyerere akapunguza bajeti ya mayai kwenye breakfast ya wanafunzi wa UDSM. Wakafanya mgomo. Akawaita Ikulu na kuwatia bakora.
Wakati ule mwanafunzi hana pressure ya ada, kula wala kulala. Anapewa pesa ya stationeries, field na research. Asubuhi anapewa breakfast yenye mapochopocho kibao (maziwa, mkate, mandazi, pancacke, chees, jam, mayai, juice, sambusa, sosage etc). Halafu wanapunguziwa mayai wanaamua kugoma. Nyerere akawatia bakora. Akawaambia msijifanye nyie ni muhimu kuliko watanzania wengine.
Sasa wale waliosomeshwa kwa ruzuku na kupata fursa zote hizo, ndio wameleta kitanzi kinaitwa mikopo ya elimu ya juu. Kitanzi hiki kimewatesa sana watoto wengi wa maskini. Hivi Nyerere nae angeweka mikopo hawa viongozi wa leo wangesoma? Nashauri MIKOPO ifutwe wanafunzi wapewe RUZUKU kama zamani. Rasilimali tulizonazo kama taifa zinatosha.!
1.Kuna kozi nyingi sana hapa ndani hakuna kabisa, yani kwa namna yeyote lazma ukasome nje ya nchi.Ndani hakukuwa na vyuo au ni kutafuta kujimwambafy?? Moto utawawakia na bado watakunywa sana banana
WASISAHAU KUUNGANISHA NA MPESA SASA!!!Abdul Razaq Badru Mkurugenzi wa Bodi amefafanua kwamba mnufaika ataanza kulipa baada ya miezi 24 [miaka 2 ] kama hana ajira.
Baada ya hapo Deni linakuwa kwa 10% kila mwaka.
Watu ambao hawajaajiriwa kwenye sekta rasmi wanapaswa kurejesha 100,000/= au ASILIMIA KUMI 10% ya pato analolipia kodi kwa mwezi.
Kwa sasa BODI ina wanufaika 14,021 wanaorejesha mikopo yao.
Baada ya marekebisho ya Bodi ya mwaka 2016, ni wazi sasa Bodi itaunganisha mishahara, TIN, Passport na kadi za benki ili wanufaika wote wapate kurejesha kwa wakati.
[Binafsi nashauri Bodi iyatake makanisa yote, watu wanaofunga ndoa pia waangaliwe kama wameanza kulipa deni, mtu anafunga ndoa kwa gharama ya sherehe milioni 50 ila halipi 100 ya Bodi, hii ni dharau kwa Magufuli]
TLS na JUDICIARY wameshauriwa kuwabana mawakili binafsi ambao wengi ni wanufaika na hawalipi kabisa. Mawakili wakati wa ku-renew PRACTICING CERTIFICATES watapaswa kuambatanisha uthibitisho kwamba wameanza kulipa deni.
Law firms nyingi Dar es salaam zina hela sana lakini hawalipi.
Kwa wale wote ambao ni professions , vyama vyao vihakikishe haviwapi leseni mpaka wawe wameanza kulipa deni la BODI, mfano TLS, WAKANDARASI, MADAKTARI, WAHASIBU CPA, MAREFARII, BOXING, TFF
Kumbuka kuna watu wnakatwa 150,000 kwa mwezi na kuna watu wamejiajiri wanapata fedha nyingi hawakatwi kwakuwa BODI haijui walipo.WASISAHAU KUUNGANISHA NA MPESA SASA!!!
Huyu ni Mimi kabisa Mkuu, Kula ni shida, kupata Kodi ni shida hicho kiwango ni Kikubwa sanaSasa mfano mtu hajaajiriwa hiyo laki moja anatoa wapi?? Hiki kiwango sidhani kama kinalipika kwa mtu ambaye hana ajira, mfano kuna mtu baada ya kuhitimu kakaa more than 3 years hana ajira atalipaje??
Na jambo jingine hapa naona kama vile mawakili wamekuwa victimized tu sio kweli kwamba kila wakili anapesa, kuwadai loan board payments wakati wa kurenew certificates huo ni ukandamizaji uliopitiliza.
Wakati mwingine tusitumie mamlaka yetu kuonea wengine simply because we are in better positions than them.
Majembe Auction Mart wazee wa Kazi utawapa hayo majibu wakati ukifika.Sasa mfano mtu hajaajiriwa hiyo laki moja anatoa wapi?? Hiki kiwango sidhani kama kinalipika kwa mtu ambaye hana ajira, mfano kuna mtu baada ya kuhitimu kakaa more than 3 years hana ajira atalipaje??
Na jambo jingine hapa naona kama vile mawakili wamekuwa victimized tu sio kweli kwamba kila wakili anapesa, kuwadai loan board payments wakati wa kurenew certificates huo ni ukandamizaji uliopitiliza.
Wakati mwingine tusitumie mamlaka yetu kuonea wengine simply because we are in better positions than them.
usitukana ndugu, toa malalamiko kwa staha, huenda kuna sheria yao umekiuka , labda sijasema kwamba umekiuk.JF acheni uFala. Mnafuta baadhi ya nyuzi na comments sijui ili muwafurahishe nani.
usitukana ndugu, toa malalamiko kwa staha, huenda kuna sheria yao umekiuka , labda sijasema kwamba umekiuk.
Kwani sasa hivi wanaoumia wazazi au watoto?una point nzuri sana, watoto wangu nimesomesha huko Moshi kwa milioni 3 kwanini nije kuwakopea milioni moja ambayo watalipa kwa riba?
Tumezoea vya bure sasa vinatutokea puani.