HESLB Mikopo kuunganishwa na NIDA, TIN, Passport na kadi za benki

HESLB Mikopo kuunganishwa na NIDA, TIN, Passport na kadi za benki

Mtazamo ubadilike mikopo itolewe kwa vijana wasomee ujuzi wasomee ujasiliamali vyuo vya maendeleo ya Jamii au veta,mkopo wa mwanachuo kikuu mmoja unaweza ukawapa wanaveta 70 ambao wataingia mtaani kuzalisha Ili kuchochea uchumi,, kuliko kupeleka elimu ya juu wakariri theory then wanarudi mtaani useless kuendesha boda boda na umachinga,huku Kodi zetu zimepotea.
Kurundika vyuo vikuu vingi nchini ni kuongeza idadi ya masikini nchini.
 
Sasa Passport inahusiana vipi na mkopo? Alaf mbona wanaolipa ni wachache hivyo kulinganisha na waajiriwa.
endelea na maswali ya ki-MATAGA siku Majembe auction Mart wakija hapo kuuza hicho kibanda cha urithi ndiyo utaelewa ninachotahadharisha hapa, haya mwenyewe naskia anaelekea INDIA akitokea NAIROBI, tuendelee na mfungo wa siku 21 na wenzetu TAG
 
USHUHUDA TOKA KWA YALIYOWAKUTA


Wengi waliosoma nje ya nchi kwa kulipiwa na bodi ya mikopo (HESLB) wanadaiwa fedha nyingi kulinganisha na waliosoma nchini. Nimeona jamaa ana mshahara 900K but anadaiwa 47M. Kwa mwezi atakatwa 143K, kwa mwaka 1.7M. Under "ceteris paribus" mwamba atahitji miaka 28 kumaliza deni lake. Lakini ukiongeza "rention fee" atahitaji miaka 35 kumaliza deni.

Assume ana mika 30 kwa sasa. Jumlisha 35 ya kulipa deni atakua na miaka 65. Umri wa kustaafu ni miaka 60. Maana yake atastaafu bila kumaliza kulipa deni. Ikitokea hivyo Bodi itaenda kukomba kiinua mgongo chake kumalizia deni (kama sheria inavyosema). Sasa jiulize je huku ni kumsaidia mtanzania au kumkomoa?

Kunapaswa kuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu mikopo ya elimu ya juu. Wazazi wanaoweza kusomesha watoto wao kwa kuwalipia ni vizuri wafanye hivyo, badala ya kuwaingiza kwenye mikopo hii inayoumiza. Pili, wazazi wasio na uwezo serikali iwape watoto wao ruzuku (bursary) si mikopo (loan).

Awamu ya kwanza na ya pili serikali iliwapa ruzuku wanafunzi wote wa elimu ya juu. Awamu zilizofuata zikaondoa ruzuku na kuleta mikopo. Nyerere na Mwinyi waliweza nini ambacho kimewashinda waliofuata?

Wakati wa Nyerere na Mwinyi wanafunzi wa vyuo vikuu walikula bure, kusoma bure, na kulala bure. Na bado walipewa pesa ya kujikimu. Kuna kipindi nchi ilipita kwenye hali ngumu kiuchumi Nyerere akapunguza bajeti ya mayai kwenye breakfast ya wanafunzi wa UDSM. Wakafanya mgomo. Akawaita Ikulu na kuwatia bakora.

Wakati ule mwanafunzi hana pressure ya ada, kula wala kulala. Anapewa pesa ya stationeries, field na research. Asubuhi anapewa breakfast yenye mapochopocho kibao (maziwa, mkate, mandazi, pancacke, chees, jam, mayai, juice, sambusa, sosage etc). Halafu wanapunguziwa mayai wanaamua kugoma. Nyerere akawatia bakora. Akawaambia msijifanye nyie ni muhimu kuliko watanzania wengine.

Sasa wale waliosomeshwa kwa ruzuku na kupata fursa zote hizo, ndio wameleta kitanzi kinaitwa mikopo ya elimu ya juu. Kitanzi hiki kimewatesa sana watoto wengi wa maskini. Hivi Nyerere nae angeweka mikopo hawa viongozi wa leo wangesoma? Nashauri MIKOPO ifutwe wanafunzi wapewe RUZUKU kama zamani. Rasilimali tulizonazo kama taifa zinatosha.!

Ndani hakukuwa na vyuo au ni kutafuta kujimwambafy?? Moto utawawakia na bado watakunywa sana banana
 
Ndani hakukuwa na vyuo au ni kutafuta kujimwambafy?? Moto utawawakia na bado watakunywa sana banana
1.Kuna kozi nyingi sana hapa ndani hakuna kabisa, yani kwa namna yeyote lazma ukasome nje ya nchi.

2. kusoma nje ama ndani ni uamuzi wa mtu, mfano oil and Gas juzi hapa ndio UDOM na UDSM wameleta ila watu walikuwa wanaifuata hiyo kozi south Afrika na UK.

3.
 
Abdul Razaq Badru Mkurugenzi wa Bodi amefafanua kwamba mnufaika ataanza kulipa baada ya miezi 24 [miaka 2 ] kama hana ajira.
Baada ya hapo Deni linakuwa kwa 10% kila mwaka.

Watu ambao hawajaajiriwa kwenye sekta rasmi wanapaswa kurejesha 100,000/= au ASILIMIA KUMI 10% ya pato analolipia kodi kwa mwezi.

Kwa sasa BODI ina wanufaika 14,021 wanaorejesha mikopo yao.

Baada ya marekebisho ya Bodi ya mwaka 2016, ni wazi sasa Bodi itaunganisha mishahara, TIN, Passport na kadi za benki ili wanufaika wote wapate kurejesha kwa wakati.
[Binafsi nashauri Bodi iyatake makanisa yote, watu wanaofunga ndoa pia waangaliwe kama wameanza kulipa deni, mtu anafunga ndoa kwa gharama ya sherehe milioni 50 ila halipi 100 ya Bodi, hii ni dharau kwa Magufuli]

TLS na JUDICIARY wameshauriwa kuwabana mawakili binafsi ambao wengi ni wanufaika na hawalipi kabisa. Mawakili wakati wa ku-renew PRACTICING CERTIFICATES watapaswa kuambatanisha uthibitisho kwamba wameanza kulipa deni.

Law firms nyingi Dar es salaam zina hela sana lakini hawalipi.
Kwa wale wote ambao ni professions , vyama vyao vihakikishe haviwapi leseni mpaka wawe wameanza kulipa deni la BODI, mfano TLS, WAKANDARASI, MADAKTARI, WAHASIBU CPA, MAREFARII, BOXING, TFF
WASISAHAU KUUNGANISHA NA MPESA SASA!!!
 
WASISAHAU KUUNGANISHA NA MPESA SASA!!!
Kumbuka kuna watu wnakatwa 150,000 kwa mwezi na kuna watu wamejiajiri wanapata fedha nyingi hawakatwi kwakuwa BODI haijui walipo.
Ifike wakati nyie wazalendo mumsaidie Magufuli kwenye utambuzi wa watu hao ili fedha za maendeleo zipatikane.
 
Sasa mfano mtu hajaajiriwa hiyo laki moja anatoa wapi?? Hiki kiwango sidhani kama kinalipika kwa mtu ambaye hana ajira, mfano kuna mtu baada ya kuhitimu kakaa more than 3 years hana ajira atalipaje??

Na jambo jingine hapa naona kama vile mawakili wamekuwa victimized tu sio kweli kwamba kila wakili anapesa, kuwadai loan board payments wakati wa kurenew certificates huo ni ukandamizaji uliopitiliza.

Wakati mwingine tusitumie mamlaka yetu kuonea wengine simply because we are in better positions than them.
Huyu ni Mimi kabisa Mkuu, Kula ni shida, kupata Kodi ni shida hicho kiwango ni Kikubwa sana
 
Sasa mfano mtu hajaajiriwa hiyo laki moja anatoa wapi?? Hiki kiwango sidhani kama kinalipika kwa mtu ambaye hana ajira, mfano kuna mtu baada ya kuhitimu kakaa more than 3 years hana ajira atalipaje??

Na jambo jingine hapa naona kama vile mawakili wamekuwa victimized tu sio kweli kwamba kila wakili anapesa, kuwadai loan board payments wakati wa kurenew certificates huo ni ukandamizaji uliopitiliza.

Wakati mwingine tusitumie mamlaka yetu kuonea wengine simply because we are in better positions than them.
Majembe Auction Mart wazee wa Kazi utawapa hayo majibu wakati ukifika.
 
JF acheni uFala. Mnafuta baadhi ya nyuzi na comments sijui ili muwafurahishe nani.
 
JF acheni uFala. Mnafuta baadhi ya nyuzi na comments sijui ili muwafurahishe nani.
usitukana ndugu, toa malalamiko kwa staha, huenda kuna sheria yao umekiuka , labda sijasema kwamba umekiuk.
 
una point nzuri sana, watoto wangu nimesomesha huko Moshi kwa milioni 3 kwanini nije kuwakopea milioni moja ambayo watalipa kwa riba?

Tumezoea vya bure sasa vinatutokea puani.
Kwani sasa hivi wanaoumia wazazi au watoto?
Kama mzazi una pesa hata mtoto amalize chuo huwezi kumtegemea.

Tatizo watoto wa masikini tu hapa,ndiyo wanateseka.

Serikali iangalie background ya mdaiwa ndiyo ijue itamkata vipi na siyo wote masikini na matajiri wakatwe sawa.
 
Abdul Razak tuligoma naye UDSM 1994 hadi chuo kikafungwa.Tuligomea hii mikopo wakati huo ikiitwa "cost sharing".Tuliiona mapema kwamba italeta taharuki baadae....
 
Back
Top Bottom