Amani iwe nanyi wapendwa katika BWANA
Hawa Hezbollah hupigana kwa masilahi ya Nani
Hamas hupigana kwa maslahi ya nchi yao ya Palestine na hawa Hezbollah kwa masilahi yapi na ya nani
Mbona wanawaumiza walebanon
Kwani Israel na Lebanon zina ugomvi
Je, Hezbollah pale Lebanon ni akina nani je ni chama cha siasa au watu gan hawa
LONDON BOY
Hezbollah yupo Lebanon kwa maslahi ya Iran na ni "first line of defence" au "defencive asset" endapo Iran itashambuliwa huku ikisaidiwa kwa silaha kama makombora, vifaa vya kuongozea makombora hayo na kuunda mfumo wake wa kijeshi.
Pili, Hezbollah wamesema kwamba wao waunga mkono harakati za Hamas huko Gaza. Mashariki ya kati kuna kundi kubwa laitwa Axis of Resistance ambalo mfadhili wake mkuu ni Iran kwa makusudio ya kulinda maslahi yake popote pale yalipo kwenye ghuba ya uajemi.
Hawa AR wana makao Iraq, Syria, Lebanon, Yemen na Gaza.
Lebanon hawana "Say" kwani wale washia ambao wametokea Iran ndo watawala kwa sasa kwa kuwa na nguvu kijeshi na kiserikali, hivyo Lebanon pamoja na kuwa na jeshi lake lakini hawana nguvu yoyote dhidi ya Hezbollah.
Waliingia hapo Lebanon mwishoni mwa miaka ya 1980s na wakawa wajiita "the voice of Shiat Community" yaani wasemaji wakuu wa washia, na hapo Iran akapata mwanya wa kuwapa misaada ambayo baadae misaada hiyo ilizaa mwelekeo wa kisiasa na baadae kijeshi.
Hivyo Hezbollah pale Lebanon wameshika nafasi nyingi bungeni, serikalini na kwenye baraza la mawaziri na kwa kutumia nguvu yao kubwa ya kijeshi wamekuwa ni kama watemi fulani hivi na wao ndo watengenezaji sera ya mambo ya nje ya Lebanon ambayo ni pamoja na kutanganza vita!
Israeli shida yao na Lebanon ni kwa sababu Lebanon imewaruhusu hawa Hezbollah kuwa na eneo lote la kusini ambalo kwa Israeli ni tishio kiusalama khasa katika mji wake wa Haifa.
Nimekupa madini machache kidogo kukupa mwanga.