Huelewi mambo mengi kuhusu mifumo ya ulinzi wa anga inavyofanya kazi.
Hezbollah wakitaka kupiga sehemu za raia wanapiga.
Iron dome battery moja ina launchers 3 hadi 4 kila launcher ina interceptors 20, ina maana kama kama zote zina missiles na launchers ni 4 hapo ni interceptors 80.
Interceptors 80 tufanye zote zinaweza kuzuia missiles kwa usahihi japo si kweli, Hezbollah wanaweza kurusha Katyusha missiles hata 1000 kwenye eneo moja tu.
Unaelewa gharama ya missile moja ya interceptor ya iron dome? Ni usd 60,000 au zaidi..hapo hio missile moja ni sawa na Tshs 163 milioni piga mara 80...ni zaidi ya bilioni 13 Tshs.
Katysha missile moja gharama ni around $ 300 tu, Hezbollah wana Katyusha missile ambazo hazihesabiki, na hizi kwa hizi siku huwa wanazitumia ku confuse iron dome kabla ya kurusha missile zao zenye uwezo kupiga target wanazotaka.
Katusha zikirushwa 1000 Iron dome katika hilo eneo itakaukiwa interceptors kwa kutaka kuzuia kila missile, hapo ndipo zinatumwa missiles za ki stratejia kama fajr 3 au fajr 5 na kuangamiza makazi ya watu n.k
Licha ya hivyo iron dome imeshaonyesha mapungufu kwa kushindwa kuzuia baadhi ya miisiles za Iran na Hezbollah.
Hapo nimeeleza kwa ninavyofahamu mimi mvaa kobazi kutoka Kibondo, lakini ukweli Hezbollah wanaweza kushambulia makazi ya raia kwa wepesi zaidi na wanaweza pia kushambulia hizo iron dome kwa usahihi kwa mbinu zao na uelewa wao kuhusu air defense.
Kwenye vita na jeshi kama Hezbollah halafu unaanza kuleta story za air defense inaonyesha hujui chochote...