Hezbollah yathibitisha 'ushindi' dhidi ya Israel baada ya usitishwaji mapigano

Israhell iliahidi kuangamizwa Kwa hizbullah mpaka sasa bado ipo waliahidi pia wakazi wa kaskazini kurudi ila mpaka sasa Hola mwisho wakasema kwamba hawaongei na magaidi ila wamekubali kuongea
 
Wangekua wanaweza si wangefanya israhell kapelekewa moto mpaka kakubali kukaa chini na magaidi
 
Wahuni tu bao Hezbulah...viongozi wao wengi wa juu wamelambishwa udongo huku miji yao hasa kusini ya Lebanon imeharibiwa vibaya majengo na miundombonu muhimu ya maji na umeme.
Wazayuni kama miji yao haija haribiwa mbona wamehama kaskazin
 
Alokwambia kama ushindi wa vitani Unapimwa kwa kufa watu wengi na uharibifu mkubwa nani
 
Kama kelele za nje hata kiongozi wa Hamas nae katolewa warranty yakukamatwa
 
hez walishawahi kufanya operation ndani ya israel au inarusha tu makombora kutokea kwa lebanon
 
Hizi tena ni chumvi, fuatilia ripot ya Hizibolla nini wamesema katika kile wamemtia hasara Israel

Ni wana jeshi 130, dron 20, ndege vita 0 n.k
 
Israhell iliahidi kuangamizwa Kwa hizbullah mpaka sasa bado ipo waliahidi pia wakazi wa kaskazini kurudi ila mpaka sasa Hola mwisho wakasema kwamba hawaongei na magaidi ila wamekubali kuongea
Hezbollah wameambiwa waondoke ktk mpaka kusini,na wananchi wa pande zote mbili Israeli na Lebanoni wanarudi ktk makazi Yao kama hueliwi BBC basi hata Aljezeera fungua update ufahamu naona Bado hujajua kinachoendelea

Israeli alikuwa tangu mwanzo alikuwa anapambana na Hamasi,Hezbolah akaja kimsaidia Hamas alikanywa hakusikia na akasema haachi mpaka Gaza iwe huru,akapondwa na yeye Sasa amekubali kutulia licha kwamba Hamas wamekabwa bado

Ila akitaka ateketee arudie Tena,wenzao wa Houth wamepewa kitu kizito mpaka wamepunguza kimbelembele

Iran aliahidi Israel akiingia Gaza itaingilia ataingia mazima nayeye kaona moto mkali kabaki kutuma mabomu kwa mbali anashidwa hata kuinua helkopta we bado huelewi kweli
 
Leo isbola wamepigwa kipigo cha haja,sasa sijui walikuwa wanawahadaa au vp.
Hezbollah walikiuka sharti la kutojipanga upya. Walikuwa wanakusanya silaha na kuzihifadhi nyumba mojawapo ya zilizosambaratishwa.
 
Lengo kuu la hezbollah lilikuwa ni kumshinikiza Israel aachane na vita ya Gaza kitu ambacho bado israel anaendelea kurusha mabomu gaza, hapa kafaeli hezbollah.

Hezbollah wamepoteza viongozi wao wote wakuu na waliobaki hawajulikani walipo kwa hofu ya kuuawa na Israel, hapa pia hezbollah wamefeli.

Lengo la Israel lilikuwa ni kuwatoa hezbollah mpakani, hapa israel kafaulu.

Sijajua mpaka sasa hezbollah wameshinda sehemu gani.
 
Hakuna hata kijiji kimoja Lebanon kuna jeshi la Israel walijaribu underground wakashindwa wenyewe na kuumizwa kuliko kuumizwa na kuuliwa, ile mission ilifeli, Hizbollah sio jeshi linaloishi magorofani, uko magorogani waliuwa raia tu hezbollah wako makini
 
Umeandika ukweli mtupu
Hezbollah ni pasua kichwa.
1. Wamesaini makubaliano bila kuyaelewa vizuri na kwa undani. Kwa mfano Hezbollah hatakiwi kuonekana kusini mwa mto Litani i.e. wamekubali kuhama na makorokoro yao kwenda Uhamishoni a.k.a. ukimbizini kaskazini ng'ambo ya mto mto Litani. Kwa lugha nyingine Israel amefanikiwa kumwondoa Hezbollah mpakani (kama lengo lilivyokuwa) mahali alipokuwa akipatumia kurusha makombora dhidi ya Israel.
2. Kimsingi Hezbollah haitambuliwi kama jeshi rasmi huko Lebanon kwa mujibu wa Cease fire Deal. Hezbollah ni kundi la kiharakati tuu na wamekatazwa kuishambulia Israel wakiwa ndani ya nchi/ardhi ya Lebanon na Jeshi rasmi la Lebanon (LAF)limepewa majukumu na mojawapo ni kuhakikisha hakuna mashambulizi yatakayotokea Lebanon dhidi ya Israel.
 
Mhhh! Mkuu; hadi tunaongea hapa leo 29/11/2024 bado Hezbollah anaendelea kuhesabu vifo vya wapiganaji wake. Inakadiriwa ni 4000+ halafu ww unasema wako makini? Yani kuhesabu 1,2,3,4,5,6.......imekuwa ni shughuli kwake. Mwisho wa siku atatoa figure ya uongo.
 
Lengo la Israel lilikuwa kuisambaratisha HAMAS huko Gaza. Hapa tunasubiri ifike mwisho kwani bado ngoma inapigwa.
Lengo la Hezbollah kumsaidia/Kumuunga mkono ndugu yake HAMAS dhidi ya Israel lakini badala yake Hezbollah ndo kapondwa hadi amekubali cease fire. Hezbollah kashindwa hapo.
Hezbollah hakuweza kuwasaidia hata kidogo Walebanon dhidi ya kichapo kutoka IDF badala yake nchi na miundo mbinu vimevurugwa i.e. kuwepo kwa Hezbollah huko Lebanon imekuwa ni hasara kubwa mno.
 
Ushabiki sometime unafanya akili zisifaanye kazi vzr. Hadi sasa pamoja na makubaliana ya kusitisha mapigano, Jeshi la israel liko ndani kusini ya Lebano na litakaa siku 60 ili kuondoa vifaa vya na Hezbullah waje hayo maeno. Sasa Ushindi ni Upi? Acheni kushabikia vita kuna watu hasa watoto wanakufa pasipo kujitakia.
Chunga sana maneno
 
Wamepunguza nini hakuna meli ya zayuni zinapita Red Sea 🌊 kule paka kaamua kusarenda kwa kuongea na hizbullah ambao awali alikataa katakataa kuongea nao hizbullah wapo kusini tokea 2006 makubaliano yaliwataka waondoke huko ila tumewaona wapo mpaka leo au unadhani kipengele cha kuondoka ni kipya
 
Nanukuu:
"Israeli alikuwa tangu mwanzo alikuwa anapambana na Hamasi,Hezbolah akaja kimsaidia Hamas alikanywa hakusikia na akasema haachi mpaka Gaza iwe huru,akapondwa na yeye Sasa amekubali kutulia licha kwamba Hamas wamekabwa bado"
Hiki kifungu πŸ‘† πŸ‘† nimekipenda.
Hezbollah alidandia mtumbwi wa vibwengo. Akayatimba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…