TANZIA Hidaya wa Pepe Kalle afariki dunia jijini Arusha

TANZIA Hidaya wa Pepe Kalle afariki dunia jijini Arusha

Mbona Hidaya alishawahi kuripotiwa kufariki dunia miaka kadhaa nyuma hapa hapa JF, huyu ni Hidaya yule yule au Hidaya mwingine?
 
Mwanamama maarufu na mrembo Hidaya Khamis Mtumwa almaarufu Hidaya wa Pepe Kalle amefariki Dunia leo asubuhi jijini Arusha, msiba upo nyumbani kwake Kaloleni.

Hidaya alitamba miaka ya mwanzoni mwa 90 baada ya mkongwe wa mziki wa Rhumba Marehemu Pepe Kalle kumtungia wimbo wakumsifia.

Pia soma

Mama mrembo, aliyekuwa mke wa mwanamuziki Pepe kale amefariki leo nyumbani kwake jijini Arusha.

Marehemu ameacha watoto watatu wa kiume, wawili wanaishi Congo kwa baba yao.
Baada ya kifo cha pepe kale hidaya alirudi nyumbani kwao Arusha ambapo alikuwa akiishi hadi umauti ulipomkuta..

Hidaya aliimba Pepe Kale ama Kanda Bongoman?
Unforgetable
Peppe kalle jitu la miraba minne.wakati peppe kale amekuja kutumbuiza DAR akamnyakua huyu mrembo.Show ya pili ya pepe kalle Tanzania alifika Arusha kumrudia Hidaya na hapo iliporomoshwa bolingo moja matata sana HIDAYA .
Mtoto mpana Hidaya akampa zawadi ya nguo pana ya rangi ya blue (unaweza kuiita dera au bazzee )peppe kale aliivaa pale pale uwanjani Shekh Amri Abed...watu wakafoka kwa bashasha halafu pini kali la HIDAYA likappromoshwa ...dah hizi burudani hazipo tena duniani.
Siku hizi kina zuchu sijui simba sijui harmorapa wanatupigia kelele tu.
 
Ama kwa hakika mkuu
 
Back
Top Bottom